Si
ajabu umeshasikia vyeo vifuatavyo afisa mahusiano, msemaji wa timu, afisa mawasiliano,
n.k. Hivyo ni baadhi ya vyeo vinavyoelenga katika kusimamia mahusiano ya asasi
na jamii yake. Hata hivyo fani ya usimamizi wa mahusiano na jamii (Public
Relations Management) haijapata umaarufu sana ukilinganisha na fani nyingine
kama vile udaktari, uhasibu, masoko, na uhandisi, ingawaje kwa kiwango kikubwa
usimamizi wa mahusiano na jamii ndio mhimili wa uhai wa asasi husika. Katika
makala hii tunaangalia maana ya mahusiano na jamii na manufaa ya kuzingatia
usimamizi ulio bora wa hayo mahusiano.
HII NI KWA WAJASIRIAMALI WA SASA NA WATARAJIWA. Part 2
Leo
tunaendelea na makala yetu ya mambo ya msingi kwa kila mjasiriamali kuyatilia
maanani ili kuweza kuwa na mafanikio endelevu. Elewa tunaposema mafanikio
endelevu tunamaanisha kuwa ni zaidi tuu ya kupata wateja leo, na kesho, bali
uwezo wa kuendeleza biashara kwa miaka mingi kwakuwa mjasiriamali anaweza kumudu
changamoto na matatizo yanayojitokeza katika fani hii ya ujasiriamali.
Tuangalie sasa points zilizobaki , yaani 6-11:-
6. Kujenga Mtandao sahihi na kuutumia
Tunasema
kujenga mtandao sahihi na kuutumia, na sio tuu kuwa na mtandao wa watu wasio na
tija kwako kwakuwa pengine hawana cha kukupatia, au wewe mwenyewe hauna maono
ya jinsi ya kuutumia mtandao wako. Chunguza vizuri mtandao wako unaweza kukuta
wapo wateja wako watarajiwa, wapo watu wanaoweza kukuuzia bidhaa, wapo watu
wanaoweza kukupa ushauri bora wa kiundeshaji, wapo watu wanaoweza kukusaidia
kifedha au hata watu wanaoweza kukuunganisha na watu wengine ambao watakuwa na
tija kwako. Ni kweli kuwa hakuna mtu ‘asiye wa umuhimu’, unatakiwa kuwaheshimu
watu wote, lakini pia ujue jinsi ya kutenda kazi zako na watu ili hata wale wanaoonekana
kuwa ‘sio wa muhimu’ waonekane wa muhimu. Hata hivyo waepuke wale
wanaokurudisha nyuma au wanaoweza kukurudisha nyuma.
7. Mahusiano na wateja
Biashara
yako ni sehemu ya maisha yako, basi hata wateja nao ni sehemu ya maisha yako na
ya biashara yako, hivyo ni muhimu kuweka mahusiano yenye tija na wateja
husika. Mahusiano ya wateja yanaanza
kabla hata hajanunua bidhaa toka kwako, iwe kupitia utafiti wako wa soko –
kutambua kwa undani mambo ya msingi yanayoweza kukufanya uuze bidhaa yako.
Mahusiano yanaendelea pale mteja anapokuja kununua bidhaa kwako, na
hayaishi tuu hapo anaponunua bidhaa bali
yanaendelea kwani ukiboresha mahusiano yako na mteja , anaweza kurudi tena
kununua bidhaa toka kwako atakapohitaji, au anaweza kuwaambia watu wengine.
Lakini pia mahusiano mazuri na wateja yanakuwezesha kujua namna unavyotakiwa
kuboresha shughuli zako pamoja na bidhaa zako. Hivyo jifunze kusikiliza kwa
ufasaha malalamiko ya wateja na kuyafanyia kazi, jitahidi kufuatilia taarifa
zinazokuwezesha kujua hisia zao kuhusu biashara yako. Katika kujenga mahusiano
bora na wateja, ni muhimu basi kuwa na mfumo mzuri wa kukusanya na kutumia
taarifa zinazohusu mwenendo wa wateja wako. Kuna program maalum za kompyuta
zinazokuwezesha kukusanya taarifa za wateja, hata hivyo waweza fuatilia
mitandao ya kijamii kama Facebook ili kutambua tabia, mabadiliko na mitazamo ya
wateja wako. Weka wazi mifumo ya kuwasiliana na wateja wako, mfano wateja
waweze wasiliana nawe kwa barua pepe, simu, kuonana ana kwa ana, au hata kwa
kuweka maoni yao katika kisanduku cha maoni.
8. Mahusiano na wanaokuuzia bidhaa/huduma
Unajenga
mahusiano bora na wanaokuuzia bidhaa au huduma ili kupata manufaa ya punguzo la bei, kuweza
kukopeshwa bidhaa baadae, na pia kuweza
kutambua mabadiliko au maboresho kwa upande wa wanaokuuzia bidhaa /huduma ambapo mabadiliko au maboresho hayo yanaweza
kuathiri uendeshaji wa shughuli za biashara yako. Mfano, chukulia kampuni X
unayoitegemea kwa ajili ya kupatia bidhaa fulani ambazo wewe huwa unauza , mara
ghafla unapata taarifa kuwa imesitisha utengenezaji wa bidhaa zake, hivyo
kujikuta wewe una athirika kwani ulikuwa unatarajia kupata bidhaa hizo toka
kwake, na haukuwa umejipanga kifedha kununua kwa kampuni nyingne ambayo kwa
kawaida huuza bidhaa kwa bei ya juu zaidi.
Laiti kama ungekuwa unafuatilia taarifa za kampuni husika unayoitegemea
, ungekuwa tayari umejipanga iwe kununua kwa muuzaji mwingine kwa bei ya juu,
au hata kufanya utafiti wa kutosha wa sehemu nyingine ya kununua bidhaa husika
kwa bei nafuu.
9. Makubaliano /mikataba
Kuna
mikataba au makubaliano kadhaa ambayo mjasiriamali utakutana nayo kama vile
makubaliano na watu unaotaka kushirikiana nao kuanzisha biashara, makubaliano
na wateja wako, makubaliano na wafanyakazi, makubaliano na wanaokuuzia
bidhaa/huduma n.k. La msingi hapa
ukumbuke kulinda maslahi yako, na uhakikishe unaelewa vema vipengele vyote vya
makubaliano, na ikibidi makubaliano hayo yawe katika maandishi na yashuhudiwe
na mwanasheria. Hakikisha mfano wewe na washirika wako wa biashara mnakubaliana
kuhusu mgawanyo wa majukumu yenu, jinsi mtakavyogawana faida, jinsi mtakavyo
suluhisha migongano mbalimbali, jinsi mtakavyochangia mtaji wa biashara na namna
ya mfumo wa uongozi wa biashara yenu.
Wengi huacha kuweka mikataba kwa kuwa tuu eti wanaaminiana. Kama wewe ni
mmoja wao unaofikiria hivyo, tambua kuwa mkataba sio kwa sababu ya
kutoaminiana, bali ni namna ya kuweka msisitizo wa kuelewana kwenu, na pia mnataka
mambo yenu yaende vema, na inapotokea kutokuenda sawa, basi muwe na pa kuanzia
katika kutafakari jinsi ya kuboresha
mambo yenu.
10. Utafiti
Kabla
ya kufanya maamuzi ya msingi katika biashara yako kama vile kuajiri wafanyakazi
wapya, kununua mashine mpya, kuzalisha bidhaa au huduma mpya, ni muhimu sana kuwa na uchambuzi usio na mashaka
unaotetea maamuzi yako ya kufanya hivyo unavyotaka kufanya. Uchambuzi huo ndio tunaouita utafiti. Fanya
utafiti kuhusu mfanyakazi unayetaka kumuajiri – mfano kupitia interview,
kuwasiliana na waajiri wake wa awali, kutafuta historia ya maisha ya mfanyakazi
mtarajiwa n.k. Hii itakuwezesha kujua kweli mfanyakazi au wafanyakazi unaoajiri
kweli wataweza kutimiza yale unayokusudia wafanye. Hali kadhalika, unapotaka
kufanya shughuli za kimasoko, inabidi ufanye utafiti ili kutambua kama kweli
shughuli hizo zitaendana na hali ya soko, na kama kweli zitaleta tija kwako.
Kumbuka rasilimali ulizonazo ni chache , hivyo ni muhimu uwe na nidhamu katika
kuzitumia, na njia mojawapo ya kuwa na nidhamu ni kufanya utafiti kama kweli
matumizi yako ya rasilimali yataleta tija. Utafiti sio lazima uwe wa gharama
kubwa, waweza fanya utafiti kwa kusoma tuu makala na habari mbalimbali toka
vyanzo tofauti, au kwa kuongea na wateja/wafanyakazi.
11. Usimamizi wa taarifa
Wataalamu
wanasema katika ulimwengu wa teknolojia tulio nao sasa, mafanikio ya biashara
yanachangiwa na aina bora ya taarifa
ambazo wamiliki/watendaji wa biashara wanazo, na ambazo wanaweza kuzitumia.
Taarifa hizi ni kama vile mwenendo wa wateja, mwenendo wa wafanyakazi, mwenendo
wa washindani wa biashara, mwenendo wa mabadiliko ya teknolojia, mabadiliko ya
kijamii, na kisiasa n.k. Mjasiriamali inabidi uwe na uwezo wa kuendana na
wakati kwa kupata na kutumia taarifa sahihi ili usiachwe nyuma na washindani
wako, au wateja wasikukumbie kwakuwa haukidhi mabadiliko wanayoyahitaji.
HII NI KWA WAJASIRIAMALI WA SASA NA WATARAJIWA part 1
Wengi
wetu tuna ndoto za kujiajiri na kufanya biashara. Au pengine tumeshajaribu
kufanya ujasiriamali lakini tunajikuta tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele
kimafanikio. Je, ni nini hasa kinafanya
wengine wafanikiwe katika ujasiriamali na wengine wasote na hata kukimbia
ujasiriamali ? Katika makala hii tunaangalia mambo muhimu 11 ambayo kama
mjasiriamali atayazingatia ataweza kujikuta
anakabiliana na changamoto za ujasiriamali na hatimaye kuwa na mafanikio
endelevu.
1. Malengo na mikakati ya muda mrefu:
Ni
kweli kuwa lengo kuu la ujasiriamali ni kuingiza ziada ya mapato ili biashara
iweze kujiendesha, kupanuka, na kuwalipa ipasavyo waanzishaji au muanzishaji wa
biashara. Hata hivyo, haitoshi tuu
kutamani kuwa na biashara kubwa bila
kuwa na mikakati ya kufikia huko. Hivyo
ni muhimu kuweka bayana , ikiwezekana katika maandishi malengo ya muda mrefu ya
biashara yako , na ufafanue mambo utakayotakiwa kufanya kufikia huko, aina ya
watu unaotakiwa kuwa nao ili kufikia huko, mfumo wa uendeshaji unaotakiwa kuwa
nao ili kufikia huko unakotaka kufikia, na uhakikishe pia watendaji /
wafanyakazi ulio nao wanalielewa hilo.
2. Malengo na mikakati ya muda mfupi mfupi:
Malengo
na mikakati ya muda mrefu haitoshi,
inabidi uweke pia malengo ya muda mfupi mfupi. Mfano malengo ya muda mrefu
yanaweza kuwa ni malengo ya miaka mitano ijayo, ila inabidi uweke malengo ya
muda mfupi mfupi, mfano malengo na mikakati ya kila mwezi, malengo ya kila robo
ya mwaka, malengo ya kila mwaka n.k .
Kumbuka
pia kuwa , kwasababu kuna mabadiliko ya mara kwa mara katika jamii, teknolojia
, mazingira ya biashara n.k inabidi uwe tayari ku ‘adjust’ malengo na mikakati
yako ili iendane na mabadiliko hayo.
3. Sheria zinazoongoza biashara:
Ni
muhimu kwa mjasiriamali, kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu sheria za nchi na
taratibu zinazosimamia shughuli husika kwani kutokutambua sheria vema, kama
vile sheria za kodi, sheria za vibali vya biashara, sheria za uandikishaji wa
biashara kunaweza kumfanya mjasiriamali kuingia gharama zisizotarajiwa na
zisizo na sababu. Mfano kushindwa kwa
mjasiriamali asiyetunza vitabu vyake kwa mujibu wa maelekezo ya sheria za kodi
anaweza kujikuta anapata faini au hata biashara yake kufungiwa. Kwa kampuni
kutokupeleka kwa msajili wa makampuni taarifa za kila mwaka za maendeleo ya
kampuni ( Annual Return) kunaweza kuwa na matokeo ya faini zisizo na sababu. Pia
kwa mjasiriamali aliyeajiri wafanyakazi kadhaa inabidi afahamu vipengele muhimu
vya sheria zinazosimamia mikataba ya kazi kwani mfano mfanyakazi anapofukuzwa bila kupewa ‘notice’
ya muda unaotakiwa kisheria, mfanyakazi
huyo anaweza kudai fidia, na pia kuna aina nyingine ya malipo ambayo mfanyakazi
anapaswa kulipwa wakati ameachishwa kazi. Hivyo kama mjasiriamali hakujiandaa
ipasavyo kufanya malipo hayo, hali ya kifedha ya biashara inaweza kutetereka.
4. Mipango na mikakati ya fedha
Ni
muhimu kwa mjasiriamali kutambua namna ya kusimamia vema maswala ya fedha ,
kwani bila lengo ni kupata mapato yanayoleta ziada, na ili kupata mapato ni
lazima kuingia gharama kadhaa. Hivyo mjasiriamali lazima awe na mbinu sahihi
za kudhitibi matumizi ili kweli
matumizi hata kama ni madogo basi kweli
yalete ziada ya kutosha kwa biashara. Mjasiriamali inabidi adhibiti matumizi
kwa kuweka miongozo imara ya jinsi biashara yake itakavyolipia gharama fulani,
aweke mikakati ya jinsi ambavyo atahakikisha kweli mapato yote yanajulikana, na
yanawekwa kwenye maandishi, na aweke mikakati ya jinsi ya kutunza taarifa za
fedha. Ziwepo mbinu za kuchochea mapato makubwa , na shughuli za kimasoko
zinazoendana na hili zisimamiwe kwa ufanisi, mfano kutoa punguzo la bei, kutoa
ofa mbalimbali kwa wateja, kutoa zawadi
n.k vyote hivyo vinaweza kutumika kuchochea mapato, hata hivyo ni muhimu kuwepo
muongozo sahihi wa mambo hayo, ili kweli yalete ziada ya mapato.
5.Masoko
Ni muhimu
mjasiriamali atambue maana halisi na mbinu bora za kufanya shughuli za kimasoko
(marketing). Shughuli za masoko hazianzi pale tuu mjasiriamali anapokamilisha
bidhaa yake, hivyo anaanza kutafuta wateja. La hasha, shughuli za kimasoko
zinajumuisha utafiti wa nini wateja wanataka, wanataka kivipi, na wanaweza
kulipia kivipi, na wapate wapi bidhaa husika.
Kuelewa wateja vema ni shughuli ya kwanza na ya muhimu kwa kila
mjasiriamali. Kisha mjasiriamali anazalisha bidhaa inayoendana na matakwa ya
wateja (mfano bidhaa iendane na ujazo unaohitajika na wateja, aina ya radha
inayotakiwa na wateja, rangi na muonekano unaotakiwa na wateja n.k). Kisha
baada ya kuwa na bidhaa sahihi , mjasiriamali anaweka bei inayoendana na soko ,
bei hiyo pia iendane na mikakati yake mingine ya kibiashara, halafu anafanya
shughuli za kuwataarifu wateja bidhaa yake husika, na sio tuu kuwataarifu, bali mjasiriamali ni
lazima atutumie mbinu za kuwafanya kweli wateja waone wanahitaji bidhaa husika
kutoka kwake yeye mjasiriamali.
Tutaendelea na points nyingine kesho....
PASSIVE AGGRESSIVE: AINA YA TABIA INAYOWATESA WENGI
Inakera
sana unapomuambia mtu afanye jambo fulani na ukitarajia alifanye kwa ufanisi wa
kiwango fulani, ila matokeo yake ni kinyume kwakuwa mtu huyo pengine asifanye
kabisa au akafanya jambo hilo kwa kiwango duni
tofauti na uwezo wake. Pia inakera inapokubidi urudie rudie kumueleza
jambo mtu , na mtu huyo haonyeshi kukubali kubadilika ili kufanya
unayomuelekeza. Hali hii huwwasababishwa na mambo mengi ikiwemo tabia ya
passive aggressive.
Passive
aggressive ni aina ya tabia ambapo mtu huonyesha ukaidi usio wa moja kwa moja,
badala yake hutumia vitendo kuwasilisha ujumbe wake wa kukataa jambo fulani.
Mfano
, mtu anapewa kazi afanye na anatakiwa kuikamilisha kwa muda fulani, ila mtu
huyo anapinga kufanya kazi hiyo, lakini hataki kueleza kupinga kwake kwa mtu
aliyempa kazi. Badala yake atakubali kazi, lakini hatoifanya kwa muda
uliopangwa,au kwa ufanisi unaotakiwa.
Watu
wenye tabia ya passive aggressive, huwa tunawaita wakaidi, hata hivyo wao
wenyewe ukiwadadisi kuhusu wayafanyayo kama kweli wanafanya kwa makusudi hawatokubali , watatoa sababu mbalimbali kama
vile kusahau, kutokujua, kufikiria sivyo ndivyo, n.k.
Wataaalamu
wa tabia wanasema tabia ya passive aggressive hutokana na udhaifu wa watu wenye
tabia hiyo kutokuweza kujielezea, kuwa na hofu ya kujieleza, au kutaka kufanya
ushindani . Hii inamaanisha kuwa watu hawa wana mapungufu katika uwezo wa
kuwasiliana vema na watu watu wengine.
Wataalamu
wa tabia, wanaongeza pia kuwa tabia hii ya passive aggressive huchangiwa na
mambo mengi ikiwa pamoja na malezi ambapo mtoto hapewi nafasi ya kuelezea hisia
zake.Pia uwezo wa kutotawala hasira na kutokuweza kuelezea hasira, mara nyingi
huwa tunasema ‘kubaki na jambo moyoni’.
Mambo
mengine yanayochangia tabia hii ni
kutokuwa na uwezo wa kuchambua tatizo husika ambalo mtu anakumbana nalo, hivyo
kujikuta anabaki kulaumu wengine au kuona wengine ndio chanzo cha matatizo ,
uwezo mdogo wa kutambua na kukubali mapungufu binafsi na kuwajibika kutokana na
hali ya maisha inayomkumba mtu.
Hitimisho:
Tumeona
kuwa tabia ya passive aggressive inakera sana, na inarudisha nyuma maendeleo
hususani kama unamtegemea mtu afanye jambo halafu yeye ndiye ana tabia ya
passive aggressive , basi itakuwa ‘imekula kwako’.
Kwa
wale ambao wana tabia ya passive aggressive, wapo kwenye hatari ya kupoteza
kazi kwani hakuna bosi anayetaka kuwa na
mtu anayepinga maamuzi . Tabia ya passive aggressive ni mbaya pia hata kwa
mahusiano na watu wengine ikijumuisha mpenzi
wako, kwani inakera na mtu hawezi kuendelea kuvumilia tabia kama hiyo
inayojirudia rudia.
Kama
una tabia ya namna hii njia rahisi ya kujirekebisha ni kukubali kwanza kuwa
tabia hii ni tatizo. Jifunze kujieleza kama unahisi huwezi kufanya jambo
fulani. Pia heshimu mtazamo wa wengine
na usiweke mtazamo hasi kila unapoambiwa
jambo.
BUSARA HII KATIKA MATUMIZI YA MUDA INA MANUFAA MAKUBWA
Kuna sababu nyingi zinazotofautisha watu
waliofanikiwa na wasiofanikiwa, lakini zaidi sana sababu ya utofauti huo ipo
katika MUDA. Ndio, sababu ni MUDA, muda
toka mtu ameamua kutenda anayohitajika kutenda ili afanikiwe, muda ambao mtu
anaweza kuvumilia, muda ambao mtu ameamua kupoteza bila kuwa na mkakati maalum,
muda unaotumika kufanya jambo la msingi, Muda wa kusubiria wakati muafaka wa
kufanikiwa kwako utimie n.k. Makala hii inachambua namna unavyoweza kujiongoza
vema kutumia muda ili kuleta mabadiliko chanya katika maisha yako.
Jambo la msingi zaidi kwanza:
Hii
inaonekana ni rahisi kusema kuliko kutenda kwa sababu wengi wetu hukumbwa na
kigugumizi katika kutambua jinsi ya kupanga mambo yetu kwa ngazi za umuhimu ili
lile la muhimu zaidi au la msingi zaidi lianze. Matokeo yake ni kujikuta
tunatumia muda mwingi kufanya mambo machache yasiyo na uzito mkubwa kwetu, na kuyapa muda mdogo yale mambo yaliyo na
uzito hasa kwetu. Kanuni rahisi ya
kukuweza kupanga mambo kwa ngazi za umuhimu ni kupima mambo kwa vigezo
vifuatavyo:-
Uwezekano
wa kuhairisha jambo: Je ni lazima jambo husika lifanyike muda huu ? Je
inawezekana kuliahirisha na kufanya baadae ? Je athari za kuahirisha ni zipi ?
Linganisha
faida za sasa na za baadae : Je, jambo hili na lile lipi litakunufaisha zaidi
sasa ? Je lipi litakunufaisha baadae ? Pia linganisha faida ya sasa na faida ya
baadae, jambo lipi linakupa faida zaidi?
Linganisha
rasilimali zinazotakiwa kutumika : Jiulize jambo lipi linatumia zaidi
rasilimali kuliko nyingine, na je unaweza kufanikisha kwa ufanisi zaidi jambo
gani kwa kutumia rasilimali unazoweza kupata.
Hivyo
basi , kanuni hii ya kufanya jambo la msingi zaidi kwanza, inatuhitaji tusiwe
watu wa kukurupuka, badala yake tuwe wachambuzi wa maisha na yale tunayokumbana
nayo ili tujipange vema. Wengi wetu hujipa moyo kwa kusema, “aah lakini hili jambo nifanyalo ni la muhimu”.
Wakati kinachotakiwa ni kufanya ‘la muhimu ZAIDI’
Muda ulivyo tabibu:
Kuna msemo usema “
unaposhinda, mheshimu uliyemshinda, na
unaposhindwa pia mheshimu aliyekushinda”.
Msemo huu una maana kubwa sana kuwa muda ni dawa au tabibu wa mambo
mengi. Wapo wengi waliokuwa matajiri wameporomoka, na wapo wengi waliokuwa
masikini wamekuwa matajiri. Hivyo kwa wewe uliye katika hali duni , usijione
kuwa basi hapo ulipo ndio mwisho. Kumbuka muda ndio kila kitu, na kwakuwa muda
bado upo, wewe unao uwezo wa kubadilika na kuwa juu, ukiweka nia, na juhudi ya
dhati. Kwa wewe ambaye upo na maisha ya
kuridhisha, usiwadharau wengine, hata wewe ni muda tuu ndio unakufanya ujihisi
hivyo ulivyo. Huu ni muda wako, kwani hata wewe , au waliokufanya hapo ulipo
nao walikuwa na muda wa kusota.
Kila jambo ni tokeo la juhudi na muda
uliotumika: Kutana na bwana PM,
mwenye umri wa miaka38, kwa sasa anasoma masomo ya ngazi ya cheti katika chuo kimoja binafsi jijini Dar es
salaam. Bwana PM alipomaliza kidato cha nne, hakufaulu, na hakukuwa na uwezo
katika familia yake ya kumpeleka masomo ya ziada. Alikaa mtaani kwa miaka
kadhaa ,kisha baadae akapata kibarua na kufanya kazi kwa miaka kadhaa. Mara kwa
mara alijikumbusha azma yake ya kujiendeleza, lakini kila wakati akawa
akijiambia hayupo tayari. Miaka imepita na sasa ana familia ya watoto wawili,
kisha anafikiria kuwa inabidi aonyeshe mfano kwa watoto wake kwa kujiendeleza
kusoma. Alifanya mitihani ya ku resit na
akapa credit za kumfanya aendelee masomo ya cheti. Bwana PM amefikia hapo alipo
kwa juhudi zake mwenyewe na muda alioutumia. Kama angefanya maamuzi mapema ya
kuanza kujisomesha, hivi leo angejikuta yupo mbali, kwani yeye mwenyewe anasema
miaka 6 nyuma alikuwa anapata kipato cha kutosha kujiendeleza kusoma, ila
alidhani hakuwa tayari kusoma.
Picha kubwa ya maisha:
Fikiria
kwa muda mfupi, aina gani ya maisha ulikuwa ukipenda uishi, je ni hayo uliyo
nayo sasa. Je, unadhani hapo ulipo ndipo ambapo ulitamani kuwa miaka 5 au 10
iliyopita? Je, mke au mume , au mpenzi uliye naye, ndio wa aina ile uliyowahi
kuifikiria na kujiambia kuwa utakuja kuwa na mtu wa aina hiyo ? Majibu kwa
walio wengi wetu ni kuwa, vile tulivyo leo, vitu au watu tulionao karibu,
maeneo tunayoishi, kazi tunazofanya, n.k sio vile ambavyo tuliwaza kuwa navyo.
Hata hivyo, sio kwamba maisha yamefikia mwisho. Hata kama hatujafikia vile
tuliwaza au kutamani kuwa, ni wazi kuwa maisha yanaendelea, na tuna imani ya
kufanya makubwa zaidi. Hili ni somo kubwa sana kuwa hatuna haja ya kujiona ni
bora zaidi ya wengine, kuwadharau wengine, au kuwakatisha tamaa wengine hasa
pale tunapodhani ‘tumekwisha toka
kimaisha’ kwakuwa hata hivyo tulivyo leo sio kwamba tulifikia kwa mikakati au
formula ya aina moja. Pengine tunao waona wapo chini yetu, ni kwamba nao
wanapitia na kujaribu mikakati fulani fulani ambayo mingine itafanikiwa,
mengine haitofanikiwa. Wengine hawafanikiwi kwa sababu ya watu kama wewe
unayewaangalia walio chini yako kama
‘washindani ‘ wako kimaisha, wakati kiukweli kila mtu ana picha ya peke yake ya kutoka
kimaisha.
Imani na matendo:
Jambo
la msingi ni kuamini kuwa unaweza kutimiza hilo unalolitaka. Imani peke yake
haisaidii, fanya matendo hasa yanaendeana na imani yako. Huwezi kumkuta padri
anaswalisha msikitini wala shekhe anaswalisha kanisani, kwakuwa Imani na
Matendo havitokuwa sawa, hivyo basi usitegemee kama imani yako ni kufanikiwa,
lakini matendo yako – ikiwa pamoja na kule kusoma kwako, mikutano yako na aina
ya watu ulio nao karibu haviendani na yale unayotamani kuwa.
USIPITWE NA MABADILIKO HAYA YA TEKNOHAMA
Maendeleo
katika teknolojia ya mawasiliano hususani kwa vifaa vya matumizi ya mkononi kama
vile simu yanazidi kuongezeka. Tunapoelekea ni kuwa watabaki watu wachache sana
watakaotumia kompyuta za mezani (desktop computer), na hata laptop zinaelekea
kupungua watumiaji, badala yake, watu wanaingia zaidi katika matumizi ya
kompyuta ndogo na zinazohamishika toka sehemu moja kwenda nyingine. Katika
makala yetu ya leo tunaangalia maendeleo makubwa tunayoyatarajia katika
teknolojia ya mawasiliano:
Spidi kubwa ya mawasiliano:
Katika kurahisisha mawasiliano, wataalamu wamegundua teknolojia ya LTE ( Long Term Evolution) ambayo pia huitwa
4G (4th Generation) ambayo ndio inayoelezwa kuwa tegemeo la kuifanya
dunia iwe na mawasiliano ya kasi kubwa zaidi na kutokana na uwezo huo, basi
vifaa vingi vitaweza kuunganishwa kupitia internet, na zaidi sana kuwezesha
simu kufanya matumizi mengi ambayo yanafanyika sasa kupitia kompyuta kama vile
kuangalia movie, kudownload movies hata za ukubwa wa 2GB, au hata kuangalia
Youtube, n.k. Soma zaidi kuhusu teknolojia ya LTE katika makala yetu kwa
kubofya hapa.
Kuchaji simu bila kutumia waya:
Makampuni
kadhaa kama vile ZTE, Google , AT & T, Starbucks na Nokia yamewekeza katika
utafiti wa kuwa na teknolojia
itakayowezesha watumiaji wa simu kuchaji simu zao bila ya kuzichomeka ukutani .
Kwa taarifa zilizopo kwenye mtandao wa Youtube, tayari Nokia wameshatoa simu
zinazoweza kuchajiwa bila waya (wireless charging). Simu hizo za Nokia ni Nokia
Lumia 920 na Nokia Lumia 820. Kampuni ya LG pia imetoa simu zake za LG Nexus 4
zinazotumia teknolojia ya wireless charging.
Website
maalum za kuonekana kwenye simu:
Katika
mabadiliko haya tunayoendana nayo ambapo watu wengi zaidi watatumia simu kuliko
kompyuta, kuna haja basi ya kuwezesha websites ziwe na muonekano kama wa kwenye
kompyuta za kawaida kwa watazamaji watakaotumia simu. Website hizo huitwa
Mobile website. Kumbuka , kwa website kuwa Mobile website sio kwamba tuu eti
inaweza kuonekana kwenye simu, hapana bali inakuwa imetengenezwa maalum kuwa na
muonekano bora kwenye simu.
Pia tazama
muonekano wa MBUKE TIMES blog kwa mobile version yake, hapo chini.
Kushoto ni mobile version, na kulia ni Mbuke Times ya 'kawaida' yaani haijatengenezwa bado maalum kwa kuonekana kwenye simu |
Hitimisho
Mabadiliko
yote haya yanamaanisha kuwa maisha yetu yanaenda kubadilika sana. Kuna ajira
mpya na kuna watakaopoteza ajira au wateja. Mfano program mpya zinaendelea
kubuniwa ili kurahisisha matumizi ya
simu ikiwa ni pamoja na kuwezesha simu kutype documents, kusave, kuprint, kama
ambavyo watu wanafanya kwa kutumia desktop computer au laptops. Kwa wabunifu na
watengenezaji wa website, wanatakiwa wajiboreshe katika kujua mabadiliko haya
makubwa kwani tayari kuna muongozo wa jinsi ya kuprogram website ziendane na
teknolojia za simu.
Wamiliki
wa website na blogs wataanza kwa wingi kubadilika kuelekea kutumia teknolojia
itakayofanya websites na blogs zao zionekane vema kupitia simu.
Waweza jisomea zaidi:
ZTE commits to wireless mobile charging
Nokia Wireless Charging
Five Mobile Technology Trends to watch in 2013
8 Tools to create mobile version of your website
Standards for web applications on mobile from WC3.
KWANINI INASEMWA PAPA MPYA ANAMILIKI TIMU YA SOKA?
Jina
la timu ni San Lorenzo de Almagro, maskani yake ni Buenos Aires, huko
Argentina. Timu hiyo inapatikana kwa website ifuatayo www.sanlorenzo.com.ar . Kisa cha watu
kusema timu hii inamilikiwa na papa mpya, Papa Francis, ambaye jina lake halisi
ni Jorge Mario Bergoglio, ni kutokana na
ukweli kuwa Papa Francis, ni mmoja wa wajumbe wa umoja unaomiliki timu hiyo, na
yeye mwenyewe ana kadi ya uanachama wa timu hiyo.
Zaidi
sana, hivi karibuni baada ya Papa huyo mpya kutangazwa, timu hiyo kongwe
iliyoanzishwa rasmi kama klabu mwaka 1908, ilianza kutumia jezi maalum zenye
picha za Papa huyo.
San
Lorenzo de Almagro, pamoja na kushinda mataji 10 makubwa katika ligi daraja la
kwanza huko Argentina, haijawahi kushinda mashindano makubwa ya
kimataifa,achilia mbali mashindano ya bara la America ya kusini. Ndio maana
Lucas Roldan, mshabiki wa timu pinzani ya Boca Juniors amenukuliwa na nesn.com
akiibeza San Lorenzo kuwa , kuchaguliwa kwa Papa huyo , ndio ushindi wa kipekee
wa kimataifa wa timu ya San Lorenzo.
Timu
ya San Lorenzo de Almargo, inahusishwa na kanisa katoliki kwakuwa hapo mwanzo
vijana walikuwa wakicheza mitaani, lakini padri Lorenzo Massa, aliwaonea huruma
vijana wa mitaani hivyo akawaita wacheze kwenye uwanja wa kanisa, na inasemwa
kuwa yeye mwenyewe padri Lorenzo, ambaye baadae alikuja kutangazwa kuwa
Mtakatifu, aliwahi kununua magoli ya uwanja huo, na alikuwa akiwafundisha dini
wachezaji hao.
Habari
hii ni kwa uchambuzi toka:
www.nesn.com
ZITAMBUE NAFASI ZA KAZI 'FEKI' ZA ONLINE
Umekua
ukitamani kupata nafasi ya kufanya kazi, na kwa bahati nzuri siku isiyo na jina
unapofungua inbox ya email account yako
unakutana na habari ya nafasi ya kazi , ambayo kiukweli inavutia kama
barua pepe hii hapa:
“MARRIOTT HOTEL CANADA HAS EMPLOYMENT OPPORTUNITIES FOR AN EXOTIC
CANDIDATES IN DIFFERENT SKILLS,SEND YOUR CURRENT CV/RESUME AND APPLICATION
LETTER IN MICRO SOFT. (marriothotel_cn@hotmail.com)”
Bila
shaka jambo la kwanza utakalofanya ni kutafuta wapi CV yako ipo, kisha fasta
unatuma hiyo CV, ukisubiria wakujibu kwa kukueleza pengine aina ya kazi
unayoweza kuapply.
Jambo
la msingi unapopata email kama hiyo sio kuharakisha kuijibu. Email zozote zenye
kueleza ‘ofa’ fulani ni vizuri kufanya uhakiki kabla ya kuzijibu. Kuna nafasi
za kazi feki kama hizo hapo, na zaidi sana kuna matapeli wengine wa kwenye
mtandao humu wanaoweza kukuingiza mjini kwa jinsi mbalimbali iwe kwa dili la
kupata schorlaship, vyuo, misaada ya fedha n.k.
Email
nyingine za nafasi za kazi feki zinaweza kuwa na maneno kama:
"After registering your Direct Deposit confirmation, please respond back to this email with your ideal interview date/time. Remember, you need your Direct Deposit account info prior to your interview, as we will be processing your payment information at that time."
Mbaya
zaidi ni kuwa, kuna wakati unaweza kweli kutuma CV, yako ukajibiwa ujaze fomu
ambayo inapatikana katika website fulani. Hapo kuna mawili, moja ukajikuta
ukiwa kwenye hiyo website yako ya kujaza fomu, ukahamishwa na kupeleka kwenye
website nyingine itakayokuwa feki.
Au pili ukafanikiwa kweli kujaza fomu na
hata ukapata kazi, ambayo ni kazi ya kufanya kwa mtandao. Baada ya wiki moja au
mbili au hata mwezi kampuni hiyo unayofanya kazi ikakuambia imekutumia hundi.
Na kweli ukapata details zote za hiyo hundi. Ila baada ya muda wakasema wamefanya
makosa, katika kiasi fulani, hivyo inabidi urudishe kwa kumtumia mtu mwingine
ambaye walikuwa wamemlenga.
Hata hivyo ukweli ni kuwa hizo hundi walizokutumia
ni feki, na kwamba utakapotuma fedha zako binafsi, ukiwa unasubiri kwa hamu
kupokea mshiko wako, utajikuta unaambiwa na benki yako cheki ni feki.
Jihadhari,
kumbuka msemo wa kiingereza usemao “ If a deal is too good to be true, think
twice”. Usione haya kushurikisha wengine, ukiona email kama hizo. Uchoyo wa
kuwaambia watu vitu unavyohisi ‘dili’ unaweza kukuponza.
Utazitambua
nafasi za kazi feki kwa mambo kadhaa kama yafuatavyo:
- Zinahitaji wewe kutanguliza malipo fulani
- Zinahitaji maelezo yako binafsi ya kifedha- mfano namba ya akaunti yako ya benki
- Ukitafuta kwa kutumia Google mfano, hauoni website ya kampuni husika inayotoa ajira
ATAKAYELETA MAENDELEO YA KWELI BONGO
Tanzania kama taifa, tuna matatizo mengi yanayosababisha kuwa na maendeleo duni, mojawapo ya matatizo hayo ni:
1.
Kutokukubali kuwa yawezekana sie wenyewe mmoja mmoja ni sehemu ya
tatizo, badala yake tupo na bidii ya kuwaonyesha wengine vidole badala
ya kuchukua hatua ya kujirekebisha sie wenyewe kwa kiwango cha mapungufu
yetu.
Mfano, mtu analalamika hakuna
fursa za kutosha za biashara, ila hafanyi utafiti wa kutosha wa
biashara , kuboresha ufahamu wake, kutafuta wataalamu haswa wa fani
husika, au hata kutafuta ushirika na wafanyabiashara wengine, badala
yake anamaliza waganga wa kienyeji.
2.Wengi wetu tumesha 'surrender' kwa udhaifu wetu na udhaifu uliopo katika jamii yetu, tunajionea 'poa' tuu. Si ajabu kusikia mtu akisema ''aaa, ndio bongo yetu hiyo, tumeshajizoeleaga utumbo huu".
Unaenda ofisi ya mtu, au hata baa, unapata huduma mbovu, haulalamiki, haukosoi, unaishia tuu kusema....aaa hii ndio bongo.
3.Tunajadili zaidi matatizo kuhusu suluhu ya matatizo. Na zaidi sana, wengi tunashindana katika namna tunavyolifahamu tatizo. Ikifika kuchukua maamuzi, na utekelezaji. Tunakuwa na visingizio kibao.
Ni
kama ile habari ya Panya kumkamata Paka, wakafanya mkutano wamkamate,
ugumu ukaja namna ya kuanza kumshambulia paka. Nani aanze kumfuata.!
Wakaishia kutegeana.
Hata waliposema twendeni wote kwa pamoja, kila mmoja akawa anasita kuwa mwengine anaweza asiende halafu 'ikawa imekula kwake'.
4. Wengi wetu tunajali sana faida ya muda mfupi, kuliko faida ya muda mrefu. Hivyo hata katika kujiajiri binafsi, hatufanyi vema, hatuna biashara au asasi endelevu. Na kwakuwa tayari tuna mapungufu haya, tunaogopa hata kuwasaidia wenzetu kwani tunaishi kiushindani zaidi, na ushindani wenyewe ni wasasa zaidi sio wa muda mrefu.
Kuwa na EGO, ni kuzuri, ila EGO, inayokuangamiza na kudidimiza mambo endelevu hata ya kwako binafsi kweli ni tatizo.
Hili
swala la kujali faida ya muda mfupi lipo hata kwa wanafunzi, hususani
wanafunzi wa asasi za elimu ya juu. Badala ya kutilia maanani kuelewa
kwa undani mambo wanayojifunza, kutafuta ujuzi na kubobea katika mambo
fani zao, wapo baadhi huwa wameshajiandaa kumaliza tuu, kupata cheti, au
kwa lugha rahisi ya mtaani 'gamba'. Hivyo elimu anayoipata mtu,
haimsaidii kujiajiri, hamsaidii kubuni mikakati ya kujikwamua kutoka
katika hali aliyonayo.
5.
Wengi wetu tunafikiria zaidi yale tusiyokuwa nayo, badala ya kufikiria
tunatumiaje yale ambayo tayari tunayo. Kijana aliyemaliza elimu ya chuo
kikuu, anawaza kuwa hawezi kupata kazi kwakuwa tuu hana 'refa', au
hawezi kujiajiri kwa kuwa hana mtaji. Hata hivyo kijana huyo huyo,
amesahau kuwa kama anao uelewa wa kutosha wa mambo aliyosomea, anaweza
kuomba kujitolea kwa asasi kadhaa zilizopo, au kwakutumia marafiki zake
ambao anachat nao kila siku kwa mtandao angeweza kufanya mambo ya
msingi. Yeye mwenyewe pia angeweza kubuni jambo ambalo lingeonyesha
kweli ana uwezo wa kipekee wa fani yake, hivyo 'kuforce' kukubalika
katika soko la ajira. Kijana huyo anayelalamika hana ajira wala hawezi
kuanza ujasiriamali, ameacha kutumia vema mikutano anayohudhuria iwe
shughuli za kidini, za kiukoo, au hata sherehe za marafiki, kutafuta
wadau wanaoweza 'kununua' ujuzi wa kipekee alionao kijana huyo. Hata
huko kutafuta kazi, amekuwa akitafuta kazi kwa njia moja tuu, ya
magazeti. Amesahau kuwa mitandao ya kijamii, kuenda moja kwa moja kwa
waajiri, kutumia mawakala wa ajira, na hata kujitolea kwa asasi fulani
kungeweza kumsaidia kufanya mabadiliko.
6.
Wengi wetu tunasubiri mabadiliko ya pamoja. Kama mfano hapo juu wa paka
na panya, wengi wetu tunafahamu matatizo tuliyonayo katika nchi yetu,
tunafahamu hata sababu ya kuwepo kwa matatizo hayo, hata hivyo tuna kila
sababu ya kujiona hatuwezi kuchukua hatua sisi kama sisi mmoja mmoja.
Kwa mtazamo wa wengi , suluhu ya matatizo yetu itatokana na maamuzi ya
wengi, itatokana na serikali, itatoka kwa chama fulani.
Kwa
tafakari hiyo hapo juu, MBUKE TIMES inaamini kuwa pamoja na kuwa wapo
wadau wengi wa kuleta maendeleo katika nchi yetu, kuna mtu wa pekee wa
kuleta maendeleo ya kweli, maendeleo endelevu katika nchi yetu ya
Tanzania. Mtu huyo ni WEWE.
Jiulize
unafanya nini kushinda mapungufu yako, unafanya nini kuzuia mambo yasiyo
yasiyoleta maendeleo ,yanayoharibu jamii yetu ? Unalalamika kuhusu
wanawake na kuporomoka kwa maadili nchini, ila wewe ndio unatoa
kipaumbele kuweka picha za utupu za wanawake katika akaunti yako ya
Facebook na kwa blog yako.JINSI YA KUWA NA JINA NA NEMBO (LOGO) KALI
Unapofikiria
kuanzisha biashara au asasi ya aina yoyote, kuna mambo mawili makubwa ni lazima
uyaamue kwa usahihi ili kukuza umaarufu wa shughuli yako, na pia kuleta hamasa
kwa wafanyakazi wako. Mambo hayo mawili tunayoyazungumzia katika makala hii ni
JINA na NEMBO (LOGO).
Wataalamu
wa masoko na mahusiano ya kijamii, wanataja mambo yafuatayo kuwa ya msingi
katika kuamua nini hasa jina au nembo ya biashara au asasi yako viwe:-
Taswira unayotaka kuijenga kwa jamii:
Jina na nembo huwakilisha vile ambavyo watu wanatakiwa wafikirie kuhusu asasi
yako. Mfano jina kama Studio Mastered Sound (SMS) la kampuni ya kutengeneza
headphones la 50CENT inalenga kuipa jamii taswira kuwa bidhaa za kampuni hiyo
zina ubora wa juu wa sauti katika kutumia hizo headphones za kampuni ya SMS
Audio.
Pia
ukiangalia nembo ya shirika la usambaji wa vifurushi la FedEx, utaona katika ya
E na X kuna alama ya mshare, hivyo kuashiria uhakika, umakini na uharaka wa
wasafirishaji hao wa vifurushi.
Au
pia angalia nembo ya duka kubwa la mtandaoni la bidhaa mbalimbali liitwalo
AMAZON. Angalia kamshare kahiyo nembo inaonyesha toka A mpaka Z, hivyo kutaka
jamii iamini kuwa kuna website hiyo ina kila aina ya bidhaa unazotaka kununua
ukiwa mtandaoni.
Waweza
pia jifunza kutoka katika nembo ya Volkswagen, yenye herufi V na W. Herufi V
inawakilisha Voks – Watu, na neno Wagen maana yake gari. Hivyo nembo inamaanisha Gari la
Watu. Lengo hapa ni kuiambia jamii kuwa kampuni hii inalenga katika kutengeneza
magari yenye kutimiza haswa mahitaji ya watu.
Mambo
ya msingi ya kiutendaji unayotaka watendaji wajue:
Majina
na logo pia hutumika kueleza mkakati wa muda mrefu wa asasi husika na kutoa
maelekezo kwa wafanyakazi au watendaji kuhusu mambo ya msingi ya kufuata ili
kufikia malengo ya kampuni. Mara nyingi hii huendana na muono wa waanzishaji wa
asasi au biashara husika.
Mfano,
kwa mujibu wa vyanzo vya habari vilivyonukuliwa na wikipedia, jina Toyota
lilichaguliwa na waanzishaji wa kampuni maarufu ya kutengeneza magari ya Toyota
Motor Corporation ya Japan, kama kielelezo cha jinsi walivyotaka kutofautisha
biashara yao na mambo yao binafsi – kwani jina la familia ya wamiliki
waanzishaji wa Toyota Motors Corporation ni TOYODA na hapo kabla magari yao
yaliitwa Toyoda, ila kwakuwa Toyoda inamaanisha kilimo cha mpunga, wakaamua
kuitofautisha kwa kuita TOYOTA, neno ambalo pia linamaanisha bahati, hivyo
kuonyesha . Hivyo badala ya kuita TOYODA wakaamua kuita Toyota. Hali hii
inamaanisha kuwa watendaji walitakiwa wawe na uelewa wa kuwa TOYOTA inaenda
kuwa kampuni kubwa zaidi na inaenda kufanya mabadiliko makubwa ya kiteknolojia,
na kwamba ni jambo kubwa kufanya kazi katika kampuni hiyo (bahati).
Nembo
ya TOYOTA inayoonyesha vijiduara vitatu, vinavyowakilisha mteja, bidhaa na
teknolojia na fursa zisiyo na kikomo. Hivyo watendaji wanatakiwa kuzingatia
mambo haya katika kuleta mafanikio ya mteja.
Urahisi wa jina au logo kukumbukwa:
Ni
muhimu kwa jina kuwa rahisi kukumbukika vichwani mwa watu, ndio maana kuna
majina kama Google, Yahoo, Adobe,
Microsoft, Apple, Toyota, Sony, Nokia, VODACOM, MTN, n.k. Mbinu rahisi ya
kufanya jina likumbukike ni kuhakikisha unakuwa na jina fupi. Ndio maana jina
kama ADOBE, jina tuu la mto unaopita nyuma ya nyumba ya Mwanzilishi wa kampuni
hiyo John Warnock ya ADOBE. Aliamua kuiita hivyo ili kurahisisha kutamkika na
kukumbukwa. Au chukulia mfano jina ADIDAS, linatokana na jina la mmiliki wa
kampuni hiyo Adolf (Adi) Dassler.
Upekee na Mvuto: Ili kuvutia watu
kuangalia na kujua zaidi kuhusu asasi yako, ni vema kuwa na jina na nembo ya
kipekee na yenye mvuto.
Hitimisho la makala hii ni kuwa, inabidi tutambue kuwa nembo na majina yanabeba mambo mengi ya msingi katika uendeshaji na mafanikio ya asasi husika. Hivyo wamiliki wa biashara au asasi nyingine zisizo za kibiashara ni muhimu wachukue maamuzi sahihi katika kuchagua nembo na majina. Rangi na mambo mengine kama vile michoro ya nembo inawakilisha mambo kadhaa ya msingi. Hata kama unampa mtu kazi ya kubuni jina au nembo ya asasi yako, ni vizuri kuwa na ufahamu huu kuwa nembo na jina utakalolipata kweli lisadifu malengo makuu, uendeshaji wa asasi yako , na iwe rahisi kukumbukwa. Hii inajumuisha pia majina ya blog, websites, na hata barua pepe.
Hitimisho la makala hii ni kuwa, inabidi tutambue kuwa nembo na majina yanabeba mambo mengi ya msingi katika uendeshaji na mafanikio ya asasi husika. Hivyo wamiliki wa biashara au asasi nyingine zisizo za kibiashara ni muhimu wachukue maamuzi sahihi katika kuchagua nembo na majina. Rangi na mambo mengine kama vile michoro ya nembo inawakilisha mambo kadhaa ya msingi. Hata kama unampa mtu kazi ya kubuni jina au nembo ya asasi yako, ni vizuri kuwa na ufahamu huu kuwa nembo na jina utakalolipata kweli lisadifu malengo makuu, uendeshaji wa asasi yako , na iwe rahisi kukumbukwa. Hii inajumuisha pia majina ya blog, websites, na hata barua pepe.
MAUJANJA YA MSINGI KATIKA MICROSOFT WORD 2010
Inawezekana unaandika taarifa ndefu yenye kuhitaji uweke namba za kurasa tofauti ili kuleta mvuto na uelewa
fasaha wa taarifa husika. Mfano ungependa kurasa zinazoonyesha Yaliyomo (Table of
contents) , Shukrani (Acknowledgement), Orodha ya vifupisho ( List of abbreviations)
, na Ufupisho wa taarifa (Abstract), n.k ziwe na namba za kirumi (I, ii, iii,n.k), halafu
sura (chapters) za taaarifa yako ziwe katika namba za kiarabu/namba za kawaida yaani
1, 2, 3, …nk.
Makala hii inaangalia jinsi ya kuweka page numbers za kirumi
na pia za kawaida, mfano ukurasa wa kwanza mpaka wa tano ziwe (i) –(v), halafu
kurasa zinafuata namba zianzie 1, 2, 3,……n.k.
Tuchukulie mfano unataka kuwa na page numbers za kirumi kwa
ukurasa wa kwanza mpaka wa tano, unachotakiwa kufanya nenda hadi ukurasa wako
wa tano, chini ya huo ukurasa wa tano,
weka cursor mwisho kabisa wa maneno yote, kisha ingia PAGE LAYOUT, halafu chagua, Breaks, halafu bofya
sehemu ya Section Breaks iliyoandikwa
Next Page.
Baada ya kubofya hiyo section break ya Next Page , nenda moja kwa moja kwenye Insert, kisha Page
Numbers, na kuchagua chaguo la Bottom ili namba zako zikae chini ya kurasa. Kisha
bofya style unayotaka number iwe, bila shaka unataka namba ikae katikati.
Ukishapata page number iliyokaa kati, sasa unahitaji kufanya
mabadiliko kidogo ya hiyo namba ili iwe ya kirumi. Kufanya mabadiliko nenda sehemu
ya Format Page numbers kama unavyoona katika picha.
Unaweza kuipata sehemu ya Format Page numbers kwa kubofya pia INSERT kisha
PAGE NUMBERS, halafu angalia katika menu zinazotelemka, utaiona hiyo Format Page
Numbers.
Ukiwa katika Format Page Numbers , angalia menu Number format, kisha chagua namba za kirumi, na
kubofya OK.
Hapo tayari umeweka namba zako za kirumi toka ukurasa wa kwanza
mpaka wa tano. Ili kuendelea na mtindo mwingine wa namba yaani 1, 2, 3, ….. kwa
ukurasa unaofuata yaani ukurasa wa SITA, na kuendelea, nenda ukurasa wa sita, au
wowote ule baada ya huo wa tano, kisha bofya INSERT, halafu PAGE NUMBERS, kisha
fanya uchaguzi kadri utakavyo kama namba hizo zikae juu au chini, na kama zikae
pembeni kulia, au katikati. Ukishafanya uchaguzi, bofya OK, na hapo tayari kazi
yako imeisha.
KUTOKA KUAJIRIWA MPAKA KUJIAJIRI: MAMBO 8 MUHIMU YA KUZINGATIA
Kuna
sababu mbalimbali kwanini mtu atake kuajiri, badala ya kuajiriwa, mfano
kipato kidogo anachopata katika kazi husika, hitaji la kutaka uhuru
zaidi binafsi wa kufanya kazi, hitaji la kuweza kutoa ajira kwa wengine
na zaidi sana kuweza kutumia vema kipaji na uwezo wa kuzalisha ambao
katika kazi ya sasa mtu hapati nafasi ya kufanya hivyo.
Kujiajiri
ni jambo linalohitaji maandalizi ya muda mrefu na kuna mambo ya msingi
kuyafahamu, haiwezekani tuu , ukaacha kazi na kusema ok, acha nijiajiri.
Makala hii inachambua mambo ya msingi ya kujiandaa na kuyafahamu kabla mtu hajaamua kuacha kuajiriwa.
Mkakati ni muhimu: Wazo au ndoto isiyo
na mkakati wa kuitimiza ni upuuzi yaani ndoto hiyo au wazo hilo halina maana, hivyo basi ndoto yako ya
kujiajiri siku moja, ni lazima iwekewe mkakati wa kuifanikisha ikiwa ni pamoja
na muda hasa wa lini utaitimiza hiyo ndoto.
Katika kuweka mkakati huu wa
kutimiza ndoto yako, fanya utafiti wa kina kuhusu mipango yako binafsi ya
maisha, mtazamo wako kuhusu maisha, mpenzi/mke wako, familia yako, na hali ya
jamii kwa ujumla inavyoenda kama vile mabadiliko ya hali ya kisiasa,
teknolojia, na uchumi.
Tengeneza malengo ya aina ya shughuli unayotaka kuifanya
ukiacha kuajiriwa, na pima uwezekano wa shughuli hiyo kufanyika kweli na kama
itakulipa. Utambue pia aina ya watu na rasilimali nyingine utakazozihitaji, na
jinsi utakavyozipata.
Unahitaji fedha: Ndio, unahitaji kiasi
cha fedha za kutosha kununua vifaa na malighafi za kutengenezea bidhaa yako.
Pia unahitaji fedha za kuwalipa wafanyakazi wako, na zaidi sana , unahitaji
fedha za kuendesha maisha yako na familia yako , kwa kipindi fulani kabla ya
biashara kuanza kukulipa mshahara. Hivyo kabla haujaacha kibarua chako,
hakikisha umetengeneza bajeti ya kutosha na una akiba ya kutimiza mahitaji ya bajeti
yako. Usingependa uache kazi halafu uanze kuwa omba omba kwa rafiki na jamaa,
au uanze kujuta.
Network ni muhimu: Kumbuka katika
kujiajiri kwako, utahitaji wateja, washirika, wafanyakazi na hata washauri
mbalimbali ili mambo yako yaende vizuri. Hivyo, wakati ukiwa umeajiriwa ndio
wakati wako muafaka wa kutengeneza na kupanua wigo wako wa watu unaowafahamu na
waliokaribu nawe.
Kumbuka
kuendeleza mawasiliano kwani watu hawapendi kuona wewe unataka
kuwatumia tuu kisha unawatupa. Endeleza mawasiliano walau hata kwa
salamu tuu. Zaidi sana, heshimu watu wote, hata usiowafahamu au wale
unaodhani 'sio watu muhimu'.
Jenga taswira
nzuri kwa jamii kwa lugha fasaha, picha na matukio mengine, usifanye watu wakufikirie vibaya.
Usipitwe na wakati: Hakikisha kuwa
unafuatilia taarifa za matukio, dili na watu wanaohusiana na aina ya shughuli
unayopanga kuifanya wakati utakapojiajiri. Hii itakusaidia kupata uzoefu na
kusoma alama za nyakati, na pengine kutambua fursa nyingine zaidi.
Endelea
kujifunza zaidi kuhusu kazi yako, watu na jamii kwa ujumla kwani kujiajiri kunahitaji
uzoefu zaidi, na zaidi sana uwezo wa kupambana na changamoto nyingi ambazo
nyingine haujawahi kukutana nazo kabisa, ila taarifa za awali na kujua jinsi
mambo yanavyoenda kwa ujumla katika jamii vitakufanya ushinde changamoto.
Maana halisi ya biashara: Baada ya
kuacha kuajiriwa, hautarajii kuwa mtu wa ‘kuganga njaa’ yaani kufanya biashara
ili mradi tuu hela iingie, lakini haujui mwelekeo wa biashara yako upoje, na
wala hakuna mkakati wa kuikuza na kuimarisha biashara husika.
Biashara inahusu
kutimiza mahitaji ya watu, kwahiyo ili mradi utakuwa na uwezo mkubwa wa
kutimiza mahitaji ya watu, na kuendelea kuhamasisha watu zaidi kuja kwako uweze
kutimiza mahitaji yao , basi biashara itakua, na itaendelea kuwa endelevu.
Kinyume cha hapo, ushindani utakutoa katika biashara kwani wateja watakambilia
kwa wengine. Biashara sio tuu kupata wateja, ni vile kuweza kuendelea kupata
wateja na kuendelea kupanua biashara.
Inabidi uipende shughuli husika
unayoifanya, na uweze kutimiza mahitaji ya wateja kupitia biashara husika.
Muda
wako mwingi utautumia katika shughuli yako mpya utakayojiajiri hivyo, kama
ambavyo kazi uliyonayo pengine ‘inakuboa’, hakikisha ajira yako binafsi ‘haikuboi’.
Umuhimu wa wafanyakazi:
Watendaji wa
shughuli husika za biashara yako utakayoianzisha ni muhimu wawe wenye
ujuzi na
uzoefu wa kutosha wa kufanya shughuli husika, na uweke mikakati ya
kuwapatia
nyenzo zote muhimu za kufanyia kazi ikiwemo teknolojia na mazingira
mazuri ya
kazi. Hivyo basi wakati unajiandaa kujiajiri tilia maanani hili katika
bajeti
yako ya kuajiri. Usingependa wafanyakazi wao wajisikie vibaya kama vile
wewe
ulivyojisikia vibaya katika ajira yako fulani (pengine ajira yako ya
sasa). Muda huu ambao umeajiriwa, ndio muda pia muafaka wa kusaka
'vipaji'- yaani watu ambao utafanya nao kazi utakapojiajiri.
Inakuhusu wewe : Mafanikio yako katika
kujiajiri yanategemea mambo mengi ila zaidi sana yanakutegemea wewe. Je, nini
hasa sababu yako ya kutaka kujiajiri?
Ni kweli una bidhaa au huduma haswa ya
kupeleka sokoni itakayokufanya iendeshe maisha yako na kuiendeleza biashara
husika au ni hasira tuu za jinsi bosi wako anavyokuchulia hapo ofisini kwako,
au kwakuwa mshahara uliopo sasa haukutoshi. Je, mipango yako mingine ya maisha
ipoje?
Ndoto zako za kusoma, au kuishi sehemu tofauti tofauti, pengine mkoa
mwingine tofauti na uliopo sasa, au pengine hata nchi husika. Je, yote hayo
yanaathiri vipi mipango na mikakati yako ya kujiajiri, bila kusahau msukumo
toka kwa familia yako.
Ndoto sahihi: Ni kweli kuwa upo sahihi
kufikiria au kuota kufanya biashara kubwa na yenye mafanikio sana, lakini
kumbuka mafanikio hayaji kwa usiku mmoja, na hata kama yatakuja kwa usiku
mmoja, inahitajika kazi ya muda mrefu kuyafanya yawe endelevu.
Hivyo basi,
usingoje wakati ‘muafaka’ wa wewe kuwa na kiasi kikubwa cha fedha au kwamba ‘umeyaset’
vema mambo yote.
Anza kidogo kidogo, kubali kufanya makosa, na tambua kuwa hata
kama utafanya uchambuzi na uchunguzi wa kutosha kuhusu soko, jamii na
teknolojia, hali halisi unayoenda kukumbana nayo inaweza kuwa tofauti na ile
uliyojifunza wakati wa uchambuzi au uchunguzi wako kwakuwa hicho unachoenda
kufanya ni kipya hakikufanyiwa uchambuzi, bali unakifanya kutokana na uchambuzi
uliofanya hapo awali.
Kuna mtu mwingine atakuja kutumia makosa au mafanikio yako kupanga
mambo yake.
ILIVYO KUSAFIRI KWA BARABARA DAR- JOBERG (AFRIKA KUSINI)
Hakuna
shaka kuwa Afrika Kusini ndio nchi iliyoendelea zaidi katika bara la Afrika.
Pengine ungependa kuitembelea ili kujionea ilivyo hasa mji maarufu wa
Johannesburg. Makala hii inachambua mambo kadhaa unayoweza kukumbana nayo kama
utasafiri kwa njia ya barabara hususani kwa njia ya kupanda mabasi kutoka Dar
es salaam hadi Johannesburg aka Joberg aka Egoli. Mojawapo wa sababu za
kusafiri kwa basi ni kujionea kwa macho
nchi nyingine kama vile Zambia, Msumbiji, au Zimbabwe. Wengine hufikiria swala
la kupunguza gharama ya nauli kwa kupanda
basi badala ya kupanda ndege ambayo ni gharama zaidi. Makala hii
inaangalia safari ya Dar-Joberg kupitia Harare, Zimbabwe.
Siku za kusafiri: Safari nzima kutoka Dar es salaam mpaka Joberg
ni ya siku nne(4). Siku nne hizo ni kama ifuatavyo, kutoka Dar- Harare, Zimbabwe
siku tatu, na kutoka Zimbabwe mpaka Joberg ni siku moja. Kumbuka kuwa sio
kwamba siku zote hizo basi litakuwa likitembea. Kuna muda wa mapumziko ya
msosi, kuchimba dawa, na masaa kadhaa ya kusubiri abiria wagonge mihuri ya viza
kwani basi likifika mpakani husimama na kuwataka abiria wote washuke ili waweze
kukaguliwa.
Wakati mwingine abiria hutakiwa kushusha mizigo yao yote, hata
iliyopo kwenye buti ili ikaguliwe. Hivyo muda mwingi hupotea wakati basi
halitembei.
Nauli: Kwakuwa hakuna basi la moja kwa
moja kutoka Dar es salaam mpaka Joberg, tarajia kulipa nauli ya Dar es salaam –
Harare, Zimbabwe, halafu kutoka Zimbabwe unapanda basi lingine la moja kwa moja
hadi Joberg. Hata hivyo unaweza amua kupanda Dar - mpaka Lusaka, halafu kutoka Lusaka ukaamua
kupitia nchi nyingine mfano ukaingia kwa Afrika Kusini kwa boda ya Msumbiji.
Makala hii inajadili njia ya kupitia Harare Zimbabwe.
Kutoka
Dar – Harare, Zimbabwe waweza lipa kwa fedha za kitanzania au kwa dola,
kuendana na makubaliano yako na watu wa mabasi pale Ubungo Bus Terminal. Nauli
ya Dar – Harare ni kati ya Dola za Kimarekani 80 -100. Wakati nauli ya Harare,
Zimbabwe mpaka Joberg, Afrika Kusini ni kati ya Dola za Kimarekani 50-100
kutegemeana na msimu wa mwaka, kwani wakati wa sikukuu bei hupanda sana. Hivyo
kwa hesabu za haraka haraka kwa makadirio ya juu, nauli kutoka Dar-Joberg ni
jumla ya Dola za Kimarekani 200 ila inaweza kuwa hadi Dola za Kimarekani 150.
Kumbuka hii ni nauli ya kwenda tuu.
Fedha za kigeni: Nchi tofauti zina
sarafu tofauti hivyo jiandae kutumia sarafu tofauti kufanya manunuzi ya
mahitaji yako ukiwa nchi husika. Mfano kwa nchini Zambia utatumia KWACHA, ukiwa
Zimbabwe, sarafu kuu ya kutumia ni Dola ya Kimarekani, wakati utakapoingia
nchini Afrika Kusini sarafu kuu ni RAND.
Unaweza
kusafiri na kiasi chako cha kutosha cha fedha za kigeni za nchi tofauti kama
tulivyotaja hapo juu, au ukaamua kuenda kununua kiasi cha fedha za kigeni
unachohitaji utakapofika katika nchi husika. Mfano ukiwa Lusaka Zambia, utaweza
kununua KWACHA kwa wauzaji wa fedha za kigeni hata pale pale kwenye kituo kikuu
cha mabasi cha Lusaka. Sio tuu KWACHA, waweza nunua pia hata Dola za
Kimarekani. Waweza pia fanya manunuzi ya fedha za kigeni ukiwa Harare, Zimbabwe
au hata Joberg katika maduka ya mabadilishano ya fedha za kigeni.
Vyakula na Gharama zake: Katika nchi zote utakazotembelea tarajia
kukuta vyakula unavyovifahamu kama vile ugali, wali, chipsi, kuku na nyama ,
hivyo usiogope sana kwamba hautopata misosi unayoipenda (Hata hivyo radha na
mapishi vinaweza kuwa tofauti na vya bongo). Vinywaji pia vipo vya kawaida,
kama soda na bia, hata hivyo pamoja na ukweli kuwa safari ni ndefu, hauruhusiwi
kunywa bia ukiwa kwenye basi. Nchini Zimbabwe unaweza kupata msosi mzuri
kwa kuanza Dola za Kimarekani 8-15, pia waweza lipa kwa RAND ukiwa Zimbabwe. Nchini Zambia unahitaji walau
KWACHA 35000. Ukiwa Afrika Kusini , msosi wa kawaida unaweza kupata kwa RAND30 na kuendelea.
Kumbuka msosi hapa unajumuisha na kinywaji pia.
Menu katika mojawapo ya mgahawa nchini Zambia |
Mambo ya Uhamiaji:Kati ya mambo
yanayochosha katika safari ya Dar- Joberg ni kuvuka mipaka ya nchi ambapo
utatakiwa kuonyesha hati ya kusafiria (passport) ili igongwe muhuri wa viza.
Kwanza kuna mpaka wa Tanzania na Zambia, halafu
kuna mpaka wa Zambia na Zimbabwe, na hatimaye kuna mpaka wa Zimbabwe na
Afrika Kusini. Ni lazima uwe na passport halali ya nchi yako ili uweze
kuionyesha igongwe muhuri wa VIZA, na
zaidi sana inabidi uwe na kadi ya chanjo ya homa ya manjano. Pia tambua kuwa ukifika mipakani kuna muda mrefu wa kusubiri mpaka passport
yako ipate kugongwa muhuri. Unaweza kujikuta umesimama kwenye foleni ya mpakani
kwa muda hata wa Masaa Matatu! Pia tarajia vurugu au hali ya kutokuwa na subira
ya wasafiri wengine wakati wa kusubiri. Kwa bahati nzuri hakuna malipo kwa
mtanzania kuingia au kutoka nchini Afrika Kusini, isipokuwa usizidishe siku 90
za kukaa kwako nchini humo.
Mambo ya Lugha: Lugha inayotumika sana
na abiria wengi kutoka Dar es salaam mpaka Zambia ni Kiswahili kwani wengi wao
ni Watanzania au watu kutoka Zambia ambao wanajua jua kwa kiwango walau kidogo
jinsi ya kuzungumza kiswahili. Unapoingia Zimbabwe hali inaanza kubadilika
kwani wengi hapo huzungumza Kiingereza kama lugha kuu ya Mawasiliano. Hata
hivyo ukiwa stendi kuu ya mabasi utaweza kuona waTanzania wengine waishio
Zambia au wafanyao kazi kwenye mabasi kutoka Tanzania kama vile Tawqa na Falcon. Kutoka
Zimbabwe mpaka Joberg , lugha kuu ni kiingereza, hata hivyo si ajabu kusikia
abiria wengi wakizungumza lugha nyingine zaidi ya kiingereza, mfano Kishona au
Kindebele kwani tarajia abiria wengi kuwa ni Wazimbabwe wanaoenda Afrika
Kusini. Mambo ya lugha yanaanza kubadilika zaidi utakapoingia Afrika Kusini,
kwani yapo makabila mengi, na kuna lugha 11 maalum kwa mawasiliano, kiingereza
ni mojawapo tuu ya hizo lugha rasmi.
Wenyeji
wengi hutumia lugha zao asili ambazo pia ni lugha rasmi kama vile ki Xhosa, ki
Zulu, ki Tswana, ki Afrikans, kiSutu, n.k.
Ukiingia Afrika Kusini: Ni mwendo
wa masaa karibu nane hadi kumi kutoka ‘BODA’ ( mpaka) wa Afrika Kusina na
Zimbabwe mpaka kufika Mji Mkuu wa Afrika Kusini Pretoria. Kutoka Pretoria,
unatumia kati ya nusu saa hadi dakika 45 kufika Joberg.
Ukiwa Joberg unaweza bado kutembelea miji
mingine mingi maarufu nchini Afrika Kusini kwa kutumia basi, mfano kutoka
Joberg- Durban ni masaa Sita hadi Saba. Kutoka Joberg – Cape Town, ni zaidi ya
Masaa 24. Kutoka Joberg kwenda Port Elizabeth ni wastani wa masaa 20. Huduma ya malazi katika
nyumba za wageni ni kati ya RAND 250 hadi R400 kutegemeana na eneo.
Na nyumba za wageni nyingine unaweza
kuhitajika kushare room na wageni wengine, yaani unaweza kulipa R250 na kuwekwa
katika chumba ambacho mpo wageni wawili au watatu jumla. Kuna hoteli pia ambazo
bei zake ni juu zaidi, pengine kuanzia R400 kwenda juu.
HISIA KALI ZA MAFANIKIO YA CRISTIANO RONALDO
Story ya mafanikio ya Cristiano Ronaldo iliyosambazwa katika mitandao mbalimbali imekuwa gumzo kwa jinsi ambavyo inagusa hisia za watu wengi. Baada ya kusoma makala hii, jiulize jee unaamini kama kweli Ronaldo mwenyewe alisema maneno haya, na kama alisema nini unajifunza. Ifuatayo ni tafsiri ya maneno yanayodaiwa kuwa Ronaldo ametaja kuwa ni siri kubwa ya mafanikio yake ya kujulikana katika soka:
“Inabidi nimshukuru rafiki yangu wa zamani, Albert Fantrau kwa mafanikio yangu. Tulicheza pamoja katika timu moja katika mashindano ya U-18. Wakati kocha wa Sporting Lisbon alipokuja kuitembelea timu yetu alisema “ Yoyote anayefunga magoli mengi katika mechi atapata nafasi ya kuingia katika academy yetu”
“Inabidi nimshukuru rafiki yangu wa zamani, Albert Fantrau kwa mafanikio yangu. Tulicheza pamoja katika timu moja katika mashindano ya U-18. Wakati kocha wa Sporting Lisbon alipokuja kuitembelea timu yetu alisema “ Yoyote anayefunga magoli mengi katika mechi atapata nafasi ya kuingia katika academy yetu”
"Katika mechi tuliyocheza, timu yetu
ilifunga magoli 3 -0. Mie nilianza kufunga goli la kwanza, Albert akaja kufunga
goli la pili, na goli la tatu lilikuwa muhimu sana kwetu.
Albert alikuwa ameshawatoka mabeki
na golikipa, nami nilikuwa nyuma yake. Alichotakiwa kufanya yeye ni kufunga
tuu, ila alinipatia pasi mie, nikafunga, nikapata nafasi ya kuenda Sporting
Lisbon Academy.
Baada ya mechi nikamuuliza kwanini
alifanya vile, na akanijibu kuwa “ Wewe ni mchezaji bora zaidi kuliko mie”
Na hata waandishi wa habari
walipomhoji Albert nyumbani kwake, Albert alikubali kuwa CR7 alisema kweli. Na Albert
akaongeza kuwa siku hiyo aliyomuachia CR7 afunge goli, ndio siku aliyoiacha
fani ya soka na akabaki hana ajira mpaka leo.
Waandishi wakataka kujua imekuaje
sasa anamiliki nyumba ya kifahari na gari bomba tuu. Na anaonekana kuwa mtu
tajiri. Mali zote anapata toka wapi ?. Albert akajibu “Vyote hivi vinatoka kwa
Ronaldo”.
Chanzo: http://soccer.indonewyork.com
N:B
Habari hiyo hapo juu haina uthibitisho wa moja kwa moja toka
Cristiano Ronaldo mwenyewe. Website nyingi zinazoandika maelezo hayo, hazielezi
wazi Ronaldo alisema lini maneno hayo, ingawaje ni kweli kuwa Ronaldo ana
rafiki ambaye kwa sasa hana ajira naitwa Albert Fantrau.