ENGLISH COURSE NA MBUKE




UNATAFUTA NAMNA RAHISI NA YA HARAKA YA KUJIFUNZA ENGLISH ?
Unataka kujua English vema kiasi kwamba uweze kujiamini kweli kweli sio tuu kuongea hata kuandika English iliyonyooka? Siri ya mafanikio ni rahisi. Uzifahamu vema kanuni za English na ufanye mazoezi mengi ili uweze kuzitumia kanuni hizo za English na uweze kujua maneno mengi ya English.

Na hicho ndicho utakachokipata katika English Course ya Mbuke, ambayo ni ya kipekee sana.

Kwanza maelekezo utayapata katika lugha unayoielewa vema, yaani maelekezo ya msingi utapewa kwa lugha ya Kiswahili, ila usidanganyike, sio kwakua utapewa maelekezo kwa njia ya Kiswahili basi hautoitumia English. Hapana. Lengo la kupewa maelekezo ya msingi kwa Kiswahili ni kukufanya uelewe vema misingi ya English kama vile past participle ni nini, auxiliary verbs, aina za tenses n.k.

Ukifundishwa kwa English wakati wewe misingi na vipengele vya msingi huvielewi ni kama kukuongezea mzigo mwingine. Yaani kwanza ujue maana ya maneno tutakayotumia kukuelekeza halafu ndio uelewe hivyo vipengele unavyoelekezwa.

Mfano: Mwalimu anataka kukueleza kuhusu Passive Voice, atakuelekeza kuwa hii ni namna ya kuandika sentensi ambapo msisitizo huwa kutoa taarifa ya mtendewa kupokea tukio Fulani. Mfano Maria analipwa = Maria is being paid. Tunaona hapa tunasisitiza kuwa Maria anapokea tukio la kulipwa yaani yeye ni mtendewa katika hiyo shughuli ya malipo.

Passive Voice ni tofauti na Active Voice ambapo huko kwenye active voice msisitizo huwa ni kuelezea kufanya tukio kwa mtendaji. Mfano : Maria analipa = Maria is paying.  Hapa Maria ni mtendaji wa tukio la kulipa , yaani yeye ndio anatoa fedha.

Umeona: Vipengele au nadharia kama hizo za English yaani Passive Voice na Active Voice kama zikielezewa kwa English na wewe ndio una shida ya uelewa wa English, somo litakua gumu zaidi.

Pili Usihofu, kwani ukishapita kujua misingi ya English ni wewe na mwalimu kutumia English wakati wote. Hapo sasa ni kazi ya mwalimu kuhakikisha katika topics za juu Zaidi unaweza kutumia misingi ya English uliyojifunza na kuielewa vema wakati anakuelekeza kwa kutumia English.

Tatu: Tuna namna rahisi sana ya wewe kujifunza popote ulipo kwani masomo yote ya English tunayatoa kupitia WhatsApp. Yes , ni WhatsApp hiyo hiyo unayoitumia kuchat na watu mbalimbali, waweza itumia kuchat na mwalimu wa English wa Mbuke, naye akakutumia AUDIO, PICHA na MAELEZO YA MAANDISHI ya  kuchat wewe na yeye  mpaka uelewe vema English.

Haupati picha mtu anawezaje kweli kujifunza kupitia WhatsApp na akaelewa? 
Andika ujumbe mfupi wa maandishi sasa kwa mwalimu wetu huko WhatsApp 0623 029 683 naye mwalimu atakuelekeza topic moja ya muhimu kwako, na utaona lazima tuu utaelewa. Mwalimu atakufundisha topic moja bure kabisa.

UTACHANGIA NINI KWA COURSE HII?
Topic moja utafundishwa bure, ila kwa ajili ya kupata maelekezo ya muda mrefu na uweze vema English utapanga muda na mwalimu na atakuambia makadirio ya muda gani unahitaji ili uweze vema English. Mafunzo hayo ya muda mrefu mfano miezi miwili au mitatu si bure.

Utachangia kidogo.
Kwa kila wiki nne utatoa tuu tshs. ELFU 25, na tena waweza kutoa kwanza elfu 15 kisha baada ya wiki mbili ukamalizia elfu 10. Hata hivyo tunapendelea mwanafunzi atoe tuu yote elfu 25 ili abaki kujikita na kusoma bila kuwaza deni.

USHAHIDI KAMILI KWAMBA HATA WEWE UNAWEZA
Baadhi ya Wanafunzi Waliosoma English hapa Mbuke wanasemaje?

Tuwasiliane WhatsApp +255 623 029 683