JINSI YA KUWA NA JINA NA NEMBO (LOGO) KALI

Unapofikiria kuanzisha biashara au asasi ya aina yoyote, kuna mambo mawili makubwa ni lazima uyaamue kwa usahihi ili kukuza umaarufu wa shughuli yako, na pia kuleta hamasa kwa wafanyakazi wako. Mambo hayo mawili tunayoyazungumzia katika makala hii ni JINA na NEMBO (LOGO).
Wataalamu wa masoko na mahusiano ya kijamii, wanataja mambo yafuatayo kuwa ya msingi katika kuamua nini hasa jina au nembo ya biashara au asasi yako viwe:-

Taswira unayotaka kuijenga kwa jamii: 
Jina na nembo huwakilisha vile ambavyo watu wanatakiwa wafikirie kuhusu asasi yako. Mfano jina kama Studio Mastered Sound (SMS) la kampuni ya kutengeneza headphones la 50CENT inalenga kuipa jamii taswira kuwa bidhaa za kampuni hiyo zina ubora wa juu wa sauti katika kutumia hizo headphones za kampuni ya SMS Audio.
Pia ukiangalia nembo ya shirika la usambaji wa vifurushi la FedEx, utaona katika ya E na X kuna alama ya mshare, hivyo kuashiria uhakika, umakini na uharaka wa wasafirishaji hao wa vifurushi.
Au pia angalia nembo ya duka kubwa la mtandaoni la bidhaa mbalimbali liitwalo AMAZON. Angalia kamshare kahiyo nembo inaonyesha toka A mpaka Z, hivyo kutaka jamii iamini kuwa kuna website hiyo ina kila aina ya bidhaa unazotaka kununua ukiwa mtandaoni.
Waweza pia jifunza kutoka katika nembo ya Volkswagen, yenye herufi V na W. Herufi V inawakilisha Voks – Watu, na neno  Wagen maana yake gari. Hivyo nembo inamaanisha Gari la Watu. Lengo hapa ni kuiambia jamii kuwa kampuni hii inalenga katika kutengeneza magari yenye kutimiza haswa mahitaji ya watu.

Mambo ya msingi ya kiutendaji unayotaka watendaji wajue:
Majina na logo pia hutumika kueleza mkakati wa muda mrefu wa asasi husika na kutoa maelekezo kwa wafanyakazi au watendaji kuhusu mambo ya msingi ya kufuata ili kufikia malengo ya kampuni. Mara nyingi hii huendana na muono wa waanzishaji wa asasi au biashara husika.
Mfano, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vilivyonukuliwa na wikipedia, jina Toyota lilichaguliwa na waanzishaji wa kampuni maarufu ya kutengeneza magari ya Toyota Motor Corporation ya Japan, kama kielelezo cha jinsi walivyotaka kutofautisha biashara yao na mambo yao binafsi – kwani jina la familia ya wamiliki waanzishaji wa Toyota Motors Corporation ni TOYODA na hapo kabla magari yao yaliitwa Toyoda, ila kwakuwa Toyoda inamaanisha kilimo cha mpunga, wakaamua kuitofautisha kwa kuita TOYOTA, neno ambalo pia linamaanisha bahati, hivyo kuonyesha . Hivyo badala ya kuita TOYODA wakaamua kuita Toyota. Hali hii inamaanisha kuwa watendaji walitakiwa wawe na uelewa wa kuwa TOYOTA inaenda kuwa kampuni kubwa zaidi na inaenda kufanya mabadiliko makubwa ya kiteknolojia, na kwamba ni jambo kubwa kufanya kazi katika kampuni hiyo (bahati).
Nembo ya TOYOTA inayoonyesha vijiduara vitatu, vinavyowakilisha mteja, bidhaa na teknolojia na fursa zisiyo na kikomo. Hivyo watendaji wanatakiwa kuzingatia mambo haya katika kuleta mafanikio ya mteja.

Urahisi wa jina au logo kukumbukwa:
Ni muhimu kwa jina kuwa rahisi kukumbukika vichwani mwa watu, ndio maana kuna majina kama Google, Yahoo,  Adobe, Microsoft, Apple, Toyota, Sony, Nokia, VODACOM, MTN, n.k. Mbinu rahisi ya kufanya jina likumbukike ni kuhakikisha unakuwa na jina fupi. Ndio maana jina kama ADOBE, jina tuu la mto unaopita nyuma ya nyumba ya Mwanzilishi wa kampuni hiyo John Warnock ya ADOBE. Aliamua kuiita hivyo ili kurahisisha kutamkika na kukumbukwa. Au chukulia mfano jina ADIDAS, linatokana na jina la mmiliki wa kampuni hiyo Adolf (Adi) Dassler.

Upekee na Mvuto: Ili kuvutia watu kuangalia na kujua zaidi kuhusu asasi yako, ni vema kuwa na jina na nembo ya kipekee na yenye mvuto.

Hitimisho la makala hii ni kuwa, inabidi tutambue kuwa nembo na majina yanabeba mambo mengi ya msingi katika uendeshaji na mafanikio ya asasi husika. Hivyo wamiliki wa biashara au asasi nyingine zisizo za kibiashara ni muhimu wachukue maamuzi sahihi katika kuchagua nembo na majina. Rangi na mambo mengine kama vile michoro ya nembo inawakilisha mambo kadhaa ya msingi. Hata kama unampa mtu kazi ya kubuni jina au nembo ya asasi yako, ni vizuri kuwa na ufahamu huu kuwa nembo na jina utakalolipata kweli lisadifu malengo makuu, uendeshaji wa asasi yako , na iwe rahisi kukumbukwa. Hii inajumuisha pia majina ya blog, websites, na hata barua pepe.
Share:

21 comments:

  1. Naimani nembo ni utambulisho wako wa kitu unacho kifanya iwe biashra na mambo mengine

    ReplyDelete
  2. Natamani kujua kutengeneza jina ila nakuta ninalolibuni limeshatumiwa na watu wengine sasa nifanjeje! Au nilitumie tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. usisite endelea kutafuta Jina zuri, unaweza kutumia hata Hilo lkn kwa kubadilisha maneno baadhi, Lakin nzuri ni kupata Jina ambalo ni geni masikioni kwa watu itapendeza

      Delete
    2. Kati ya Mambo ya kuepuka Ni kutengeneza nembo inayofanana na kampuni jingine unataka kujifunza zaidi piga simu namba: 0754465961

      Delete
  3. Naipataje Logo itakayo faa kwenye mafuta ya nywele

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimtumie jina unalotaka na jinsi unavyowazia iwe,nitakutengenezea kwa gharama kidogo tu. Email; eurobusinessinter@outlook.com

      Delete
    2. Gharama ni kiasi gani but samahani

      Delete
    3. Nahitaji logo ya kampuni taasisi

      Delete
  4. Nahitaji logo ya biashara yangu naipataje?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama kuna mtu anahitaji kutengenezewa logo ya biiashara yake nzuri anichek kwa email richardjhn74@gmail.com

      Delete
  5. Nahitaji kutengeneza logo ya biashara yangu nawezaje?

    ReplyDelete
  6. Nahitaji nembo na jina la buashala

    ReplyDelete
  7. Aisee nimependa sana maelekezo yenu,nataman na mm pia nitengeneze logo yangu je nifanyeje?

    ReplyDelete
  8. Natafuta log ya kampuni na jina

    ReplyDelete
  9. SAJILI BIASHARA YAKO UKIWA NA SHAROSE ENTERPRISE

    HUDUMA ZETU
    1. Kufanikisha usajili wa kampuni yako au jina la biashara
    2. Kufanikisha Usajili wa Trademark ya biashara yako
    3. Kuupdate kampuni yako, au kufanya mabadiliko yoyote
    4. Kufatilia vibali vya biashara.
    5. Kutengeneza Company profile, logo.
    6. Kuandika Sera za Kukopeshea(lending policy).
    7. Kuandaa Business Plan
    8. Kutoa Mafunzo ya Uendeshaji wa Kampuni

    TUNAPATIKANA
    Bunju B, Dar es salaam

    MAWASILIANO
    Facebook Page: Sharose Enterprise
    Piga simu: 0755 440 118
    WhatsApp: 0755 440 118
    E-mail: info@sharoseenterprise.co.tz
    Instagram: sharoseenterprise

    ReplyDelete