Kwa uzoefu
wangu wa kujifunza na kuweza kutumia lugha nne tofauti yaani Spanish, English,
Zulu na Xhosa nimejifunza kuwa kuna mambo ambayo yanarahisisha sana namna ya
kujifunza lugha. Hivi karibuni nilitumia mbinu hizo kujifunza lugha ya Spanish
kwa miezi mitano tuu.
Pia kama
mwalimu binafsi wa lugha ya nimeona wanafunzi wangu wengi wakikwama kupiga
hatua katika kujifunza English kwa namna
isiyo sahihi ya jinsi ya kujifunza wanayojaribu kufanya. Ndio maana nimeamua
kuandika makala hii kama muongozo kwa wanafunzi wangu wa English lakini pia
kushare na jamii kwa ujumla.
Ni ukweli
usiopingika kuwa kabla ya kujifunza kitu chochote ikiwemo kujifunza lugha ni
muhimu kujua namna ya kujifunza kitu husika, ili uweze kujifunza kwa ufanisi na
kwa urahisi.
Hata hivyo
elewa kuwa ninaposema kujifunza kwa urahisi, simaanishi kuwa basi kujifunza
kwako hakutakuwa kugumu.
Baadhi ya mambo katika lugha yatakuwa magumu hata
hivyo kwa mbinu sahihi na kwa bidii ya dhati, mchakato wako wa kujifunza
utakuwa rahisi zaidi kuliko bila kuwa na mbinu na ufahamu wa namna sahihi ya
kujifunza.
Hii ni sehemu ya kwanza ya makala hii .
Vifuatavyo
ni vipengele vya hizo mbinu za kujifunza lugha hususani lugha ya English.
1. Kudhamiria
kuweza:
Usianze au
kuendelea kujifunza kiingereza bila kujiaminisha na kudhamiria kuweza haswa kwa
ufasaha. Haitoshi tuu kutamani kuweza kiingereza, unahitaji nguvu ya dhamira ya
toka moyoni , na kujiaminisha kuwa wewe unaweza.
2. Kujiwekea
muda maalum wa kufikia kiwango fulani :
Haitoshi
tuu kudhamiria kuweza kuongea lugha ya kiingereza. Unahitaji kujiwekea malengo na mikakati ya kufikia hilo lengo na
iwe kufikia lengo fulani ndani ya muda maalum.
Njia bora
ya kujiwekea muda ni kuligawa lengo lako la kufahamu lugha katika vipengele
vidogo vidogo halafu unaweka malengo ya kufanikisha hivyo vipingele vidogo
vidogo ndani ya muda fulani.
Kwanza fahamu
picha kubwa ya yote unayotakiwa kujifunza, kisha jiulize yapi kati ya hayo
tayari unayajua au pengine una ‘idea’ nayo.
Hivyo weka malengo kwa kila kipengele kuendana na uwezo wako wa kuelewa.
Mfano ukishajua vipengele vyote mfano vya TENSES, jiulize ndani ya muda gani
utaweza kukamilisha tenses. Hivyo hivyo kwa
vipengele vingine .
Kutambua
viungo mbalimbali vinavyounda sentensi:
Kila
unachoandika, kuongea, kusikia au kusoma ni SENTENSI. Katika sentensi unaandika,
kusoma, kusikiliza au kuongea maneno. Hata hivyo ili kurahisisha watu kujifunza
lugha, maneno hayo yamegawanywa katika makundi , na hayo makundi yanafafanua
matumizi na kanuni kuhusu kila neno katika kundi husika.
Mfano sentensi hii :
Will you come to school ? - Je utakuja shule ?
Hapa tuna maneno matano, na
yanatoka katika makundi yafuatayo:
Verbs: Will na Come
Pronoun: You
Proposition: TO
Noun: School
Kufahamu kanuni zinazoongeza makundi haya zitakafunya ujue
kwanini hayo maneno yamepangiliwa hivyo yalivyo , mfano kwanini haikuwa COME
WILL TO SCHOOL YOU ?
Katika kujifunza kanuni hizi ndipo utakapojitofautisha wewe
na wale ambao wanadhani kujifunza lugha ni kujua maneno mengi.
Kuna watu wengi
wanajua maneno mengi ya kiingereza na ni wepesi wa kuchanganya kiswahili na
kiingereza wakati wa mazungumzo ila inapofika kuongeza kiingereza tuu kwa
mfululizo inakuwa ni tabu kwakuwa hawana ujuzi wa kuunda vema sentensi.
3.Kusoma kwa mpangilio:
Baada ya kufahamu kuwa lugha ina vipengele
kadhaa vinavyounda sentensi na kanuni zinazoongoza kila aina ya maneno , bila
kusahau nyakati –tenses, jiwekee utaratibu wa kusoma hatua kwa hatua kwani
vipengele vingi vinaendana.
Mfano kama haujaelewa vizuri tenses, itakupa shida kuelewa
active and passive voice, na reported speeches.
4. Kusoma kwa
mfululizo bila kukatisha:
Mbinu
nyingine ni kuhakikisha kuwa unajifunza lugha kwa muda maalum na kwa mfululizo.
Sio unajifunza kwa "manati" mara moja au mbili tuu ndani ya
mwezi.
Ili kufanikiwa kujifunza kwa urahisi na kwa haraka hakikisha unatenga muda walau mara tatu kwa wiki, na kwa muda wa walau masaa mawili kila siku na hakikisha unasoma hivi kwa muda mrefu mfano walau kwa miezi mitatu mfululizo kwa kasi hiyo hiyo ya kujifunza.
Ili kufanikiwa kujifunza kwa urahisi na kwa haraka hakikisha unatenga muda walau mara tatu kwa wiki, na kwa muda wa walau masaa mawili kila siku na hakikisha unasoma hivi kwa muda mrefu mfano walau kwa miezi mitatu mfululizo kwa kasi hiyo hiyo ya kujifunza.
Kwanini unahitaji kujifunza kwa mfulululizo ? Ni kwa sababu kujifunza
lugha kunahitaji sana kukumbuka na kuhusanisha uelewa wa vipengele tofauti vya
lugha.
Hivyo kujifunza mfululizo kunatuma ujumbe kwa ubongo wako kuwa hayo
unayojaribu kuhifadhi katika kumbukumbu yako ni ya muhimu, hivyo nao unatenga
nafasi ya kukusaidia kuyapata haraka unapohitaji –yaani kumbukumbu ya haraka.
Kumbuka pia
hata kama unasoma na yanakua magumu, ukiendelea kurudia mara kwa mara jambo
lile lile baada ya muda unajikuta umeshajenga aina fulani ya kumbukumbu na
uwezo wa kuhusanisha yale uliyojifunza zamani na taarifa mpya ya jambo hilo
hilo husika.
5. Kufahamu matumizi ya nyakati na kanuni zake :
Mbinu hii
inahusu vitu viwili muhimu sana, kwanza kujua uwepo wa nyakati na matumizi yake
yaani je katika hali ipi unatumia present tense, au past tense, au future
tense, halafu kitu kingine cha pili cha muhimu sana ni kujua kanuni
zinazoongoka namna ya utungaji wa sentensi katika kila aina ya nyakati.
Hitimisho:
Hii ilikuwa sehemu ya kwanza ya makala hii ya mbinu za kujifunza kwa haraka na kwa urahisi lugha ya kiingereza. Usikose kusoma sehemu ya pili.
Kwa ujumla
wake makala hii imekuonyesha kuwa kujifunza English ni zaidi ya kusikiliza, na
kusoma , unahitajika wewe mwenyewe kuingia hasa katika mchakato wa kuelimika
kwa kufanya bidii kujikumbusha na kurahisha namnaya kuelewa unachosoma.
Pitia
masomo ya KIINGEREZA katika ukurasa maalum wa KIINGEREZA. BOFYA HAPA
Kwa msaada
wa maelekezo binafsi ya kufahamu vema lugha ya kiingereza. Wasiliana nami kwa
WhatsApp +57 301 297 1724 au kwa John.myungire@gmail.com
kaka vp me nilikua natak kujifunza kingeleza vzr cpo vzr sana na lugha iyo naitaj msaada wako nipo dar es salaam
ReplyDeleteTHANKS ALOT
ReplyDelete
ReplyDeletePendekeza tovuti hii www.letspal.com
Nimependa sana haya makala nami nimuhitaji wa kujifunza lugha ya kiingireza
ReplyDeleteNimependa sana makala hii nami ni muhitaji was kufahamu vizuri lugha ya kiingeleza
ReplyDeleteNimependa Sana imeeleza vyema na mm nataman kujifunza
ReplyDeleteSuhaylat cosmeticsbrand
ReplyDeleteNimependa hii makala nahitaji kujua vzru yaan sina uwezo wa kujiamin kuongea mbele za watu utanisaidiaje
ReplyDeleteHabari kaka nimekuelewa Sana mbinu zako Nina uhitaji mkubwa Sana wa kujifunza kingeza nahitaji Sana msaada wako ili kulifanikisha hili
DeleteNimependa sana makala yako na mimi ni mhitaji wa kunifunza
DeleteTestimomy on how I got my loan
ReplyDeleteI live in UK London and i am a happy woman today? and i
told my self that any lender that rescue my
family from our poor situation, i will refer
any person that is looking for loan to him,
he gave me happiness to me and my family, i
was in need of a loan of $250,000.00 to
start my life all over as i am a single
mother with 3 kids I met this honest and GOD
fearing man loan lender that help me with a
loan of $250,000.00 U.S. Dollar, he is a GOD
fearing man, if you are in need of loan and
you will pay back the loan please contact
Mr. Anthony Mitchell
via EMAIL : applicantonline3@gmail.com
Habari kwakwwli nimependa hii makala ninachoomba nahitaji kukijua kingereza vizuri na kukitumia pia naomben msaad sana juu ys hil kwani pia najikuta sina ujadir ila naamini kupitia kwenu nitaweza
ReplyDeleteI JUST GOT MY 5.2 BTC I AM THE HAPPIEST PERSON RIGHT NOW, THANKS TO DARK WEB ONLINE HACKERS FOR SAVING MY LIFE, IF YOU ARE INTERESTED IN MAKING GOOD PROFIT IN BITCOIN MINING AND YOU ARE LOOKING FOR A GENUINE HACKERS TO EARN FOR YOU I WILL ADVISE YOU ALL TO CONTACT DARK WEB ON EMAIL: DARKWEBONLINEHACKERS@GMAIL.COM WHATSAPP +18033921735 THEY ARE GENUINE AND LEGIT THEY HAVE PUT SMILE ON MY FACE
ReplyDeleteI JUST GOT MY 5.2 BTC I AM THE HAPPIEST PERSON RIGHT NOW, THANKS TO DARK WEB ONLINE HACKERS FOR SAVING MY LIFE, IF YOU ARE INTERESTED IN MAKING GOOD PROFIT IN BITCOIN MINING AND YOU ARE LOOKING FOR A GENUINE HACKERS TO EARN FOR YOU I WILL ADVISE YOU ALL TO CONTACT DARK WEB ON EMAIL: DARKWEBONLINEHACKERS@GMAIL.COM WHATSAPP +18033921735 THEY ARE GENUINE AND LEGIT THEY HAVE PUT SMILE ON MY FACE
ReplyDelete