JIFUNZE KIINGEREZA:SIMPLE PRESENT TENSE

Picha na footer.com
Simple Present Tense hutumika kuelezea matendo ambayo hufanywa mara kwa mara , kila siku, hurudiwa rudiwa mfano kila wiki, kila mwaka au taarifa ambazo ni za kweli kwa ujumla kama vile jua kuzama n.k.

Kanuni kuhusu vitendo (Verbs): 
Vitendo katika simple present tense hufuata kanuni zifuatazo:
Kama watendaji ni I, WE, YOU, au THEY, basi vitendo huwa katika hali yake ya kawaida ya asili bila ya kubadilisha kitu, mfano KULA- EAT, PIKA-COOK, SOMA- READ, ANDIKA- WRITE, SAFISHA - CLEAN.
Ila kama watendaji wa vitendo husika ni kati ya HE, SHE , IT , basi vitendo huongezewa S au ES, kutegemeana na aina ya neno. Mfano  EATS,  COOKS, READS, WRITES, CLEANS
Mfano ya sentensi katika present simple tense:
I eat –Mimi hula.
She reads–Yeye husoma (mwanamke)
He cooks –Yeye hupika (mwanaume)
They  talk – Wao huzungumza
Sasa tuangalie namna ya kuandika sentensi katika miundo ile minne tuliyosoma sehemu ya utangulizi

Sentensi za maelezo chanya : Hizi hutoa taarifa bila kukanusha wala kuuliza swali.
Mfano wa sentensi ya maelezo chanya katika simple present tense
They  talk – Wao huzungumza

Jinsi ya kuandika sentensi za maelezo chanya katika simple present tense:
Katika muundo wa sentensi hizi, hakikisha mtenda anatajwa mwanzoni, kisha kufuatia KITENDO  chenye kuongezewa S au ES kama mtenda ni wa HE, SHE, IT, na kama mtendaji wa kitendo ni wa I, YOU, WE, THEY, basi weka tuu kitendo katika hali yake halisi bila S wala ES.
Mfano:
I WRITE– Mimi husoma
She WRITES –Yeye husoma (mwanamke)
He SINGS- Yeye huimba (mwanaume)
We SING – Sisi huimba

Sentensi za kukanusha : Hizi hutoa taarifa za kukanusha wala tukio.
Mfano wa sentensi ya maelezo ya kukanusha katika simple present tense
-He does not sing. Yeye haimbi.

Jinsi ya kuandika sentensi za kukanusha katika simple present tense :
Katika muundo wa sentensi hizi, hakikisha mtenda anatajwa mwanzoni, kisha kufuatia na DOES kama mtendaji wa kitendo anatoka kundi la HE,SHE, IT, ila kama mtendaji anatoka kundi la THEY, I, WE, YOU, basi tumia neno DO. Ukishafanya hivyo ongezea neno NO baada ya DOES au DO kisha taja kitendo ila sasa vitendo VYOTE vitakuwa katika hali ya kawaida bila kuongezewa S au ES haijalishi ni kundi lipi la mtendaji wa tendo.
Mfano:
He does not sing. –Yeye huwa haimbi
They do not sing – Wao huwa hawaimbi
I do not read – Mie huwa sisomi
She does not read. Yeye  huwa hasomi. Ni makosa kusema  She does not READS.

Sentensi za kuuliza chanya: Hizi huuliza swali katika hali chanya.
Mifano ya sentensi ya kuuliza chanya katika simple present tense
Does  he sing well ? -- Je yeye huimba vizuri ?
Do they sing well ? Ye wao huimba vizuri ?

Jinsi ya kuandika sentensi za kuuliza chanya katika present continuous tense :
Katika muundo wa sentensi hizi, hakikisha mtenda HATAJWI mwanzoni, , Hivyo basi ANZA na DOES kama mtendaji wa kitendo anatoka kundi la HE,SHE, IT, ila kama mtendaji anatoka kundi la THEY, I, WE, YOU, basi tumia neno DO. Ukishafanya hivyo mtaje mtenda,  kisha taja kitendo ila sasa vitendo VYOTE vitakuwa katika hali ya kawaida bila kuongezewa S au ES haijalishi ni kundi lipi la mtendaji wa tendo.
Mifano Zaidi: 
Does he teach ? Je yeye hufundisha ?
Do I teach ? Je mimi hufundisha ?
Do I go to school  ? Je mimi huenda shule  ?
Do you go to school ? Je wewe huenda shule ?
Does she go to school ? Je yeye huenda shule ?
Sentensi ya kuuliza kwa kukanusha: Hizi huuliza swali katika hali ya kukanusha.
Mifano ya sentensi za kuuliza kwa kukanusha katika simple present tense
Doesn’t he  play football?  Je yeye huwa hachezi mpira wa miguu?
Don’t you  play football ? Je wewe huwa hauchezi mpira wa miguu ?

Jinsi ya kuandika sentensi za kuuliza kwa kukanusha katika present perfect tense :

Katika muundo wa sentensi hizi, hakikisha mtenda HATAJWI mwanzoni, , Hivyo basi ANZA na DOES kama mtendaji wa kitendo anatoka kundi la HE,SHE, IT, ila kama mtendaji anatoka kundi la THEY, I, WE, YOU, basi tumia neno DO, kisha ufuatiwe na NOT. Ukishafanya hivyo mtaje mtenda,  kisha taja kitendo ila sasa vitendo VYOTE vitakuwa katika hali ya kawaida bila kuongezewa S au ES haijalishi ni kundi lipi la mtendaji wa tendo.
Does + not = Doesn’t
Do + not = Don’t

Mifano zaidi:
Doesn’t he  play everyday ?  Je huwa hachezi kila siku ?
Don’t we  like mangoes?  Je huwa hatupendi maembe ? 

Hitimisho:
Pitia aina nyingine za tenses kama tulivyoona hapa Mbuke Times, kwa kubofya link hapa chini


Share:

0 comments:

Post a Comment