JINSI YA KUSALIMIANA KATIKA ENGLISH


Salamu katika Kiingereza
Kusalimiana ni jambo la msingi sana katika lugha yoyote. Makala hii inakupa ufahamu kuhusu mambo ya msingi ya kufahamu na kuzingatia kuhusu kusalimia katika English. Utajifunza salamu katika kiingereza zipoje na jinsi ya kujibu.
Kwanza kabisa elewa kuwa LUGHA yoyote ni sehemu ya utamaduni wa wale wanaoitumia lugha hiyo. Hivyo basi kwakua tamaduni zipo tofauti ndivyo ilivyo hata kwenye matumizi ya lugha.
Mfano:
1.Kwenye English hakuna salamu maalum kwa mtu mzima au aliyekuzidi rika kama ilivyo kwa Kiswahili kuwa tuna SHIKAMOO kwa watu wazima au waliotuzidi rika.
Hivyo kwa mfano salamu ya GOOD MORNING (Gud moning) ambayo tafsiri yake ni ‘’ZA ASUBUHI” ni kwa watu wa marika yote. Hata HOW ARE YOU? ( Hau a yu ?) ambayo tafsiri yake ni ‘’U HALI GANI ?” ni kwa watu wa marika yote.
2. Kuna mazungumzo  katika Kiswahili  ambayo hayapo katika English. Mfano kwenye Kiswahili tunayo “Umeamkaje ?”, hatuna sentensi yenye tafsiri hii ya moja kwa moja katika English. Badala yake tumia HOW DID YOU SLEEP (Hau did yu slip?) ambayo ukiitafsiri moja kwa moja kwa Kiswahili itakua  ‘’ULILAJE?’’ila haifai kuitafsiri moja kwa moja.
3. Elewa kuwa kama ilivyo kwenye Kiswahili kua kuna aina ya salamu ambazo hutumika tuu kwa watu wa rika zako au watu wako wa karibu, hivyo hivyo kwenye English zipo salamu ambazo nazo ni za watu wa rika yako au watu wako wa karibu. Salamu hizi huitwa INFORMAL GREETINGS.
Tambua hata hivyo kuwa Informal Greetings za Kiswahili sio lazima zitafsirike moja kwa moja kwa English.
Mfano: Kwenye Kiswahili huwa tunasema MAMBO? kwenye English sema WHAT’S UP? (Wats ap?) ukiitafsiri moja kwa moja hiyo what’s up itamaanisha KIPI KIPO JUU?

Baada ya hayo tuangalie sasa salamu mbalimbali katika English.

KUSALIMIANA ASUBUHI:
Good morning ( Gud moning)  -  ZA ASUBUHI
Jibu: Good morning, how are you? (Gud moning, hau a yu?) -ZA ASUBUHI, UHALI GANI?
I am fine, thanks. How are you too? (Am fain, thenks, hau a y utu?)  - MZIMA , ASANTE. UHALI GANI NAWE? Au ingeweza kusemwa hivi:
I am fine, thanks.  How did you sleep ? (Am fain, thenks, hau did yu slip?)  MZIMA , ASANTE. UMEAMKAJE?
Ukiulizwa HOW DID YOU SLEEP? Jibu hivi :  GREAT ! (Gret) - (VIZURI SANA) au kama haujamka vema, basi NOT WELL (Not wel) kwamba  SIKUAMKA VIZURI.
Au kama unataka kuelezea kuwa mambo sio mazuri wala sio mabaya, ili mradi siku zinaenda unaweza sema.
I CAN’T COMPLAIN  ( I kent komplein) – SIWEZI LALAMIKA

KUSALIMIANA MCHANA
Kwa mchana waweza salimia hivi:
Good afternoon ( Gud aftanun) – HABARI YA MCHANA ?
Kuitikia: Good afternoon, how are you? ( Gud aftanun, haw are yu?) – HABARI YA MCHANA, WAENDELEAJE?
Kumbuka , katika English , hata kama mlikwisha salimiana asubuhi, bado mchana waweza kutumia salamu hiyo hiyo niliyoielezea hapo juu.

KUSALIMIANA USIKU
Good evening ( Gud ivining) – HABARI YA JIONI ?
Kuitikia: Good evening, how are you? ( Gud ivining, haw are yu?) – HABARI YA MCHANA, WAENDELEAJE?
I am fine, thanks. How are you too? (Aiem fain, thenks, hau a y utu?)  - MZIMA , ASANTE. UHALI GANI NAWE?
Jibu: I’m great , how was your day ? (Am gret, hau woz yua dei ?) – NIPO POA SANA,  JE SIKU YAKO ILIKUA VIPI ?
Jibu: It was great, thanks. ( It woz gret, thenks) – ILIKUA POA SANA , ASANTE

Kumbuka kusalimiana hata kama ni usiku tumia Good evening kama ilivyoelekezwa hapo juu. Ila kama ni kuagana au kumtamkia mtu usiku mwema ndio utumie GOOD NIGHT.

TUWASILIANE: Kwa masomo zaidi ya English tuwasiliane kwa WhatsApp 0623 029 683 au nipigie kwa namba hiyo hiyo tuzungumze zaidi namna gani nitakusaidia uweze English vema.

Share:

4 comments:

  1. Nijimbo zuri Sana kuanzisha hii program

    ReplyDelete
  2. Có 500 triệu nên làm gì, kinh doanh gì giàu nhanh năm 2022?
    Có 500 triệu nên làm gì? 500 triệu không phải là số tiền nhỏ, nhưng cũng không quá lớn để bạn đầu tư mạo hiểm. Có 500 triệu nên kinh doanh gì ở nông thôn? Có 500 triệu nên đầu tư vào đâu? Để trả lời những câu hỏi, hãy cùng chúng tôi tìm hiểu ngay trong bài viết này nhé.
    Tiìm hiểu ngay tại: https://nhatnamvilla.com/co-500-trieu-nen-lam-gi-kinh-doanh-gi-2022/

    ReplyDelete
  3. Kitu kizuri sana kuanzisha kitu kama hiki jaman itasaidia sana wale ambao hatuelewi kingereza vizuri

    ReplyDelete