MAMBO YA KUFAHAMU KUHUSU PRESENT CONTINUOUS TENSE

present continuous tense
''I am looking at you''. Mfano wa sentensi ya present continuous tense


Tenses katika Kiingereza ni muhimu sana kwani kutunga sentensi kunahitaji sana ujue upo kwenye tense ipi ili sentensi utakazotunga zilete maana unayokusudia. Kwa leo tuangalie mambo ya msingi kujua kuhusu Present Continuous Tense.  Katika kujifunza Present Continuous Tense na tense zote katika Kiingereza unapaswa kuzingatia haya tutakayosoma.

Utangulizi Kuhusu Present Continuous Tense:
Kwenye Kiswahili, tense hii ya Present Continuous Tense hutambulishwa na  kiashiria cha NA, mfano niNAkula, waNAimba, waNAlalamika. Kwa watu wengi tuzungumziapo Present Continuous Tense hufikiria tuu kuwa ni ile tense ambayo huonyesha matukio yanayoendelea wakati sentensi zake zikitajwa. Mfano nikisema I am singing – niNAimba, basi lazima niwe ninafanya hilo tukio la kuimba.
Hata hivyo tunapoenda kuangalia kazi za Present Continuous Tense, utaona kuwa tense hii ambayo kwa Kiswahili inatafsirika kama Wakati Uliopo Katika Hali ya Kuendelea ,  huwa ina kazi nyingi Zaidi ya kusema tuu tukio linaendelea.

Kazi za Present Continuous Tense:
Present Continuous Tense ina kazi zifuatazo:
1. Kuonyesha tukio linaendelea wakati sentensi inatajwa.
Mfano: I am teaching you now- Wakati huu nina kufundisha.
2. Kuonyesha mchakato wa tukio fulani unaendelea. Hii ina maana kuwa sio lazima kila tutumiapo Present Continuous tukio liwe linaendelea wakati sentensi inatajwa. Ila unaweza itumia Kama tukio lipo kwenye mchakato wa kufanyika.
Mfano : This year I'm helping people from Tanga - Haina maana kuwa wakati huu naongea ndio nawasaidia watu toka Tanga ila ninachomaanisha ni kuwa hilo swala la kuwasaidia watu ninalifanya.
3. Kazi ya tatu ya Present Continuous ni kuonyesha kuwa tukio fulani limeamuliwa kufanyika wakati ujao
Mfano: I am cooking rice tomorrow - (Nimeamua nitapika wali kesho).

Kutunga Sentensi za Kiingereza kwa kutumia Present Continuous Tense
Kutunga sentensi inapaswa ujue kuwa MATUKIO yote yawe na ING yaani kwa mfano go iwe going, eat iwe eating, play iwe playing.
Halafu utumie Auxiliary Verbs zifuatazo:
Kwa he, she na it tumia IS
Kwa they, we, you na I tumia ARE
Kwa I tumia AM
Mfano:
I am eating - Ninakula

She is eating- Anakula
We are eating – tunakula

Kuuliza Swali Katika Present Continuous Tense
Anza na Auxiliary Verbs Kisha mtendaji halafu tukio.

Mifano ya kuuliza maswali kwenye Present Continuous Tense:
(i) Je unapika ?
Mtendaji ni YOU, tukio Ni Cook na Auxiliary Verb ya YOU ni ARE hivyo itakua:
Are you cooking ?

(ii)Je wanaimba ?
Mtendaji ni wao - they, tukio ni Sing, na Auxiliary Verb ya they Ni Are hivyo itakua:
Are they singing ?

(iii)Je ninalia ?
Mtendaji Mimi -I , auxiliary verb ya I ni AM na tukio Ni Cry hivyo itakua
Am I crying ?

Kukanusha Katika Present Continuous Tense

Kukanusha katika Present Continuous Tense kufanyike kwa kutumia kanuni ifuatayo:
Mtendaji + Auxiliary Verb+ not + Verb

Mifano ya Kukanusha katika Present Continuous Tense :
(i) Mimi siimbi
I +am+no+ singing
Yaani I am not singing

(ii)Hatupiki
We are not cooking

HITIMISHO: Kama nilivyodokeza pale awali kuwa nyakati(tenses) katika English ni mada muhimu sana. Na natumaini katika Makala hii umepata mwanga wa mambo gani ya msingi ya kujua kwa kila aina ya tense utakayojifunza.
Ili ujifunze Zaidi kuhusu tenses, nakushauri ujipatie kitabu nilichoandika ninachochambua tenses zote kwa kina, na mifano kibao. Zaidi sana katika kitabu hicho utajifunza pia kuhusu Passive Voice, Conditional Sentences na Indirect Speech. Kitabu ni tshs. Elfu KUMI tuu. Tuwasiliane kwa WhatsApp 0623 029 683 ujipatie hicho kitabu.


Share:

6 comments: