![]() |
''I am looking at you''. Mfano wa sentensi ya present continuous tense |
Tenses katika Kiingereza ni muhimu sana kwani kutunga sentensi
kunahitaji sana ujue upo kwenye tense ipi ili sentensi utakazotunga zilete
maana unayokusudia. Kwa leo tuangalie mambo ya msingi kujua kuhusu Present
Continuous Tense. Katika kujifunza
Present Continuous Tense na tense zote katika Kiingereza unapaswa kuzingatia
haya tutakayosoma.
Utangulizi Kuhusu Present
Continuous Tense:
Kwenye Kiswahili, tense hii ya Present Continuous Tense hutambulishwa na kiashiria cha NA, mfano niNAkula, waNAimba, waNAlalamika. Kwa watu wengi tuzungumziapo Present Continuous Tense hufikiria tuu kuwa ni ile tense ambayo huonyesha matukio yanayoendelea wakati sentensi zake zikitajwa. Mfano nikisema I am singing – niNAimba, basi lazima niwe ninafanya hilo tukio la kuimba.
Kwenye Kiswahili, tense hii ya Present Continuous Tense hutambulishwa na kiashiria cha NA, mfano niNAkula, waNAimba, waNAlalamika. Kwa watu wengi tuzungumziapo Present Continuous Tense hufikiria tuu kuwa ni ile tense ambayo huonyesha matukio yanayoendelea wakati sentensi zake zikitajwa. Mfano nikisema I am singing – niNAimba, basi lazima niwe ninafanya hilo tukio la kuimba.
Hata hivyo tunapoenda kuangalia kazi za Present Continuous Tense,
utaona kuwa tense hii ambayo kwa Kiswahili inatafsirika kama Wakati Uliopo
Katika Hali ya Kuendelea , huwa ina kazi
nyingi Zaidi ya kusema tuu tukio linaendelea.
Kazi za Present Continuous Tense:
Present Continuous Tense ina kazi zifuatazo:
1. Kuonyesha tukio linaendelea wakati sentensi inatajwa.
Mfano: I am teaching you now- Wakati huu nina kufundisha.
2. Kuonyesha mchakato wa tukio fulani unaendelea. Hii ina
maana kuwa sio lazima kila tutumiapo Present Continuous tukio liwe linaendelea
wakati sentensi inatajwa. Ila unaweza itumia Kama tukio lipo kwenye mchakato wa
kufanyika.
Mfano : This year I'm helping people from Tanga - Haina
maana kuwa wakati huu naongea ndio nawasaidia watu toka Tanga ila
ninachomaanisha ni kuwa hilo swala la kuwasaidia watu ninalifanya.
3. Kazi ya tatu ya Present Continuous ni kuonyesha kuwa
tukio fulani limeamuliwa kufanyika wakati ujao
Mfano: I am cooking rice tomorrow - (Nimeamua nitapika wali
kesho).
Kutunga Sentensi za Kiingereza kwa kutumia Present
Continuous Tense
Kutunga sentensi inapaswa ujue kuwa MATUKIO yote yawe na ING
yaani kwa mfano go iwe going, eat iwe eating, play iwe playing.
Halafu utumie Auxiliary Verbs zifuatazo:
Kwa he, she na it tumia IS
Kwa they, we, you na I tumia ARE
Kwa I tumia AM
Mfano:
I am eating - Ninakula
She is eating- Anakula
We are eating – tunakula
Kuuliza Swali Katika Present
Continuous Tense
Anza na Auxiliary Verbs Kisha mtendaji halafu tukio.
Mifano ya kuuliza maswali kwenye Present Continuous Tense:
(i) Je unapika ?
Mtendaji ni YOU, tukio Ni Cook na Auxiliary Verb ya YOU ni
ARE hivyo itakua:
Are you cooking ?
(ii)Je wanaimba ?
Mtendaji ni wao - they, tukio ni Sing, na Auxiliary Verb ya
they Ni Are hivyo itakua:
Are they singing ?
(iii)Je ninalia ?
Mtendaji Mimi -I , auxiliary verb ya I ni AM na tukio Ni Cry
hivyo itakua
Am I crying ?
Kukanusha Katika Present
Continuous Tense
Kukanusha katika Present Continuous Tense kufanyike kwa
kutumia kanuni ifuatayo:
Mtendaji + Auxiliary Verb+ not + Verb
Mtendaji + Auxiliary Verb+ not + Verb
Mifano ya Kukanusha katika Present Continuous Tense :
(i) Mimi siimbi
(i) Mimi siimbi
I +am+no+ singing
Yaani I am not singing
(ii)Hatupiki
We are not cooking
HITIMISHO: Kama nilivyodokeza pale awali kuwa nyakati(tenses)
katika English ni mada muhimu sana. Na natumaini katika Makala hii umepata
mwanga wa mambo gani ya msingi ya kujua kwa kila aina ya tense utakayojifunza.
Ili ujifunze Zaidi kuhusu tenses, nakushauri ujipatie kitabu
nilichoandika ninachochambua tenses zote kwa kina, na mifano kibao. Zaidi sana
katika kitabu hicho utajifunza pia kuhusu Passive Voice, Conditional Sentences
na Indirect Speech. Kitabu ni tshs. Elfu KUMI tuu. Tuwasiliane kwa WhatsApp
0623 029 683 ujipatie hicho kitabu.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteThanx alot
ReplyDeleteThanks
ReplyDeleteThank you
ReplyDeleteHotels near Las Vegas Casino, NV, United States - Mapyro
ReplyDeleteThe following hotels with casinos 문경 출장마사지 in Las Vegas, NV on 수원 출장마사지 MapYRO Casinos near 계룡 출장안마 or close baoji titanium to Las Vegas 밀양 출장마사지 Casino.
Ushuhuda Wangu Wa Dhati 💖
ReplyDeleteBaada ya baba yangu mdogo kuniacha kwa miezi saba ndefu, nilivunjika kabisa. Alinifungia kwenye mitandao yote ya kijamii, akasafiri mbali, na hakukuwa na njia ya kumfikia. Nilikaribia kukata tamaa juu yetu, lakini ndani kabisa nilijua singeweza kupata mtu yeyote ambaye angenipenda na kunitendea jinsi alivyonitenda.
Siku moja, bosi wangu kazini aliona jinsi nilivyokuwa na huzuni na akanitambulisha kwa Dk. Dk. Dawn alisikiliza hadithi yangu na akaahidi kwamba mpenzi wangu atanirudia ndani ya siku tatu. Kusema kweli, sikuamini mwanzoni—lakini kwa mshangao mkubwa zaidi, siku ya tatu simu yangu iliita. Ilikuwa ni yeye! Alikuwa akilia na kuomba msamaha, akisema hataniacha tena.
Tangu siku hiyo, uhusiano wetu umekuwa wenye nguvu na mzuri zaidi kuliko hapo awali. Amekuwa akinipenda na kunijali sana mimi na mtoto wetu, na sasa tunafunga ndoa baada ya miezi miwili tu! ❤️
Shukrani zote kwa Dk. Dawn, ambaye kwa kweli aliwezesha jambo lisilowezekana. Ninampendekeza kwa moyo wote kwa yeyote anayekabiliwa na changamoto katika:
Masuala ya mahusiano au ndoa
Ugonjwa au magonjwa
Ugumba au matatizo ya bahati nasibu
Kesi za mahakama au kurejesha mali
Dk. Dawn kweli hutatua matatizo kwa ufanisi na hurejesha furaha katika maisha ya watu.
Wasiliana na Dr. Dawn kwenye WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com