Picha na footer.com |
Huu ni muendelezo wa makala kuhusu mbinu za kujifunza lugha ya kiingereza. Tafadhali pitia pia sehemu ya kwanza ya makala hii. BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KWANZA.
Lengo la makala hii ni kukupatia ufahamu wa kuwa kujifunza lugha ya kiingereza si tuu kujifunza kanuni za lugha hiyo na kuongea, ila unahitaji pia kuwa na mpangilio wa namna ya kujifunza ili uweze kujifunza kwa haraka na kwa urahisi.
6. Kufahamu
miundo mbalimbali ya sentensi na kanuni za kufuata katika kila muundo:
Unapojifunza
lugha unatakiwa kukumbuka kuwa kila unachoandika, kuongea, kusikia au kusoma ni
SENTENSI. Hata hivyo sentensi
zimegawanywa katika makundi tofauti tofauti ili kukusaidia kujua kanuni sahihi
kwa kila kundi la sentensi. Angalia hapa chini aina ya sentensi na matumizi yake.
Kwa mtazamo wa lengo kuu ujumbe
unaotolewa katika sentensi:
Sentensi ya maelezo chanya : Anaimba vizuri. He is singing well.
Sentensi ya kukanusha. Haimbi vizuri. He is
not singing well.
Sentensi ya kuuliza. Je anaimba vizuri ? Is he singing well ?
Sentensi za kutoa amri na sentensi za kuomba: Sit down ! May I sit ?
Kwa mtazamo wa nani
uhusiano kati ya mtendaji na anayetendewa
Active
Voice :
Mfano : He is writing a
letter Yeye anaandika barua.
Passive Voice : Mfano
a letter is being written by him. Barua inaandikwa na yeye.
7. Mbinu za kujifunza maneno mapya:
Ni wazi
kuwa kujifunza maneno mapya bila
kuyakumbuka hakutokusaidia kuelewa hivyo wakati unakutana na neno jipya fanya
jitihada ya kutafuta kitu cha kukumbusha
neno hilo jipya ulilojifunza. Fanya kulinganisha au kuhusanisha neno
husika na neno fulani mfano kama neno PURE ni geni kwako, basi sema aah PURE
nafahamu neno lingine linaloitwa hivyo ambalo ni KANDE ila kwa kipare. Hivyo
unasema PURE (Halisi kwa kiingereza) inaweza pia kuwa KANDE kwa kipare.
Mbinu
nyingine ni kuangalia namna ya kuongezea maneno mengine ya lugha husika
yanayoendana na neno moja jipya ulilojifunza. Mfano kama kwako neno SHUT (Kufunga) ni geni kwako, basi fikiria maneno
mengine kama vile OPEN (Fungua), au
jiulize neno hilo linaweza kutumika na maneno mengine yapi mfano MLANGO
(DOOR), DIRISHA (WINDOW). Hivyo unakua
umehusanisha kitendo cha kushut na vitu vinavyotumika na hicho .
Hitimisho:
Kwa ujumla
wake makala hii imekuonyesha kuwa kujifunza English ni zaidi ya kusikiliza, na
kusoma , unahitajika wewe mwenyewe kuingia hasa katika mchakato wa kuelimika
kwa kufanya bidii kujikumbusha na kurahisha namnaya kuelewa unachosoma.
Pitia
masomo ya KIINGEREZA katika ukurasa maalum wa KIINGEREZA. BOFYA HAPA
Kwa msaada
wa maelekezo binafsi ya kufahamu vema lugha ya kiingereza. Wasiliana nami kwa
WhatsApp +57 301 297 1724 au kwa John.myungire@gmail.com
0 comments:
Post a Comment