Showing posts with label Jifunze Kiingereza. Show all posts
Showing posts with label Jifunze Kiingereza. Show all posts

MAMBO YA KUFAHAMU KUHUSU PRESENT CONTINUOUS TENSE

present continuous tense
''I am looking at you''. Mfano wa sentensi ya present continuous tense


Tenses katika Kiingereza ni muhimu sana kwani kutunga sentensi kunahitaji sana ujue upo kwenye tense ipi ili sentensi utakazotunga zilete maana unayokusudia. Kwa leo tuangalie mambo ya msingi kujua kuhusu Present Continuous Tense.  Katika kujifunza Present Continuous Tense na tense zote katika Kiingereza unapaswa kuzingatia haya tutakayosoma.

Utangulizi Kuhusu Present Continuous Tense:
Kwenye Kiswahili, tense hii ya Present Continuous Tense hutambulishwa na  kiashiria cha NA, mfano niNAkula, waNAimba, waNAlalamika. Kwa watu wengi tuzungumziapo Present Continuous Tense hufikiria tuu kuwa ni ile tense ambayo huonyesha matukio yanayoendelea wakati sentensi zake zikitajwa. Mfano nikisema I am singing – niNAimba, basi lazima niwe ninafanya hilo tukio la kuimba.
Hata hivyo tunapoenda kuangalia kazi za Present Continuous Tense, utaona kuwa tense hii ambayo kwa Kiswahili inatafsirika kama Wakati Uliopo Katika Hali ya Kuendelea ,  huwa ina kazi nyingi Zaidi ya kusema tuu tukio linaendelea.

Kazi za Present Continuous Tense:
Present Continuous Tense ina kazi zifuatazo:
1. Kuonyesha tukio linaendelea wakati sentensi inatajwa.
Mfano: I am teaching you now- Wakati huu nina kufundisha.
2. Kuonyesha mchakato wa tukio fulani unaendelea. Hii ina maana kuwa sio lazima kila tutumiapo Present Continuous tukio liwe linaendelea wakati sentensi inatajwa. Ila unaweza itumia Kama tukio lipo kwenye mchakato wa kufanyika.
Mfano : This year I'm helping people from Tanga - Haina maana kuwa wakati huu naongea ndio nawasaidia watu toka Tanga ila ninachomaanisha ni kuwa hilo swala la kuwasaidia watu ninalifanya.
3. Kazi ya tatu ya Present Continuous ni kuonyesha kuwa tukio fulani limeamuliwa kufanyika wakati ujao
Mfano: I am cooking rice tomorrow - (Nimeamua nitapika wali kesho).

Kutunga Sentensi za Kiingereza kwa kutumia Present Continuous Tense
Kutunga sentensi inapaswa ujue kuwa MATUKIO yote yawe na ING yaani kwa mfano go iwe going, eat iwe eating, play iwe playing.
Halafu utumie Auxiliary Verbs zifuatazo:
Kwa he, she na it tumia IS
Kwa they, we, you na I tumia ARE
Kwa I tumia AM
Mfano:
I am eating - Ninakula

She is eating- Anakula
We are eating – tunakula

Kuuliza Swali Katika Present Continuous Tense
Anza na Auxiliary Verbs Kisha mtendaji halafu tukio.

Mifano ya kuuliza maswali kwenye Present Continuous Tense:
(i) Je unapika ?
Mtendaji ni YOU, tukio Ni Cook na Auxiliary Verb ya YOU ni ARE hivyo itakua:
Are you cooking ?

(ii)Je wanaimba ?
Mtendaji ni wao - they, tukio ni Sing, na Auxiliary Verb ya they Ni Are hivyo itakua:
Are they singing ?

(iii)Je ninalia ?
Mtendaji Mimi -I , auxiliary verb ya I ni AM na tukio Ni Cry hivyo itakua
Am I crying ?

Kukanusha Katika Present Continuous Tense

Kukanusha katika Present Continuous Tense kufanyike kwa kutumia kanuni ifuatayo:
Mtendaji + Auxiliary Verb+ not + Verb

Mifano ya Kukanusha katika Present Continuous Tense :
(i) Mimi siimbi
I +am+no+ singing
Yaani I am not singing

(ii)Hatupiki
We are not cooking

HITIMISHO: Kama nilivyodokeza pale awali kuwa nyakati(tenses) katika English ni mada muhimu sana. Na natumaini katika Makala hii umepata mwanga wa mambo gani ya msingi ya kujua kwa kila aina ya tense utakayojifunza.
Ili ujifunze Zaidi kuhusu tenses, nakushauri ujipatie kitabu nilichoandika ninachochambua tenses zote kwa kina, na mifano kibao. Zaidi sana katika kitabu hicho utajifunza pia kuhusu Passive Voice, Conditional Sentences na Indirect Speech. Kitabu ni tshs. Elfu KUMI tuu. Tuwasiliane kwa WhatsApp 0623 029 683 ujipatie hicho kitabu.


Share:

JINSI YA KUSALIMIANA KATIKA ENGLISH


Salamu katika Kiingereza
Kusalimiana ni jambo la msingi sana katika lugha yoyote. Makala hii inakupa ufahamu kuhusu mambo ya msingi ya kufahamu na kuzingatia kuhusu kusalimia katika English. Utajifunza salamu katika kiingereza zipoje na jinsi ya kujibu.
Kwanza kabisa elewa kuwa LUGHA yoyote ni sehemu ya utamaduni wa wale wanaoitumia lugha hiyo. Hivyo basi kwakua tamaduni zipo tofauti ndivyo ilivyo hata kwenye matumizi ya lugha.
Mfano:
1.Kwenye English hakuna salamu maalum kwa mtu mzima au aliyekuzidi rika kama ilivyo kwa Kiswahili kuwa tuna SHIKAMOO kwa watu wazima au waliotuzidi rika.
Hivyo kwa mfano salamu ya GOOD MORNING (Gud moning) ambayo tafsiri yake ni ‘’ZA ASUBUHI” ni kwa watu wa marika yote. Hata HOW ARE YOU? ( Hau a yu ?) ambayo tafsiri yake ni ‘’U HALI GANI ?” ni kwa watu wa marika yote.
2. Kuna mazungumzo  katika Kiswahili  ambayo hayapo katika English. Mfano kwenye Kiswahili tunayo “Umeamkaje ?”, hatuna sentensi yenye tafsiri hii ya moja kwa moja katika English. Badala yake tumia HOW DID YOU SLEEP (Hau did yu slip?) ambayo ukiitafsiri moja kwa moja kwa Kiswahili itakua  ‘’ULILAJE?’’ila haifai kuitafsiri moja kwa moja.
3. Elewa kuwa kama ilivyo kwenye Kiswahili kua kuna aina ya salamu ambazo hutumika tuu kwa watu wa rika zako au watu wako wa karibu, hivyo hivyo kwenye English zipo salamu ambazo nazo ni za watu wa rika yako au watu wako wa karibu. Salamu hizi huitwa INFORMAL GREETINGS.
Tambua hata hivyo kuwa Informal Greetings za Kiswahili sio lazima zitafsirike moja kwa moja kwa English.
Mfano: Kwenye Kiswahili huwa tunasema MAMBO? kwenye English sema WHAT’S UP? (Wats ap?) ukiitafsiri moja kwa moja hiyo what’s up itamaanisha KIPI KIPO JUU?

Baada ya hayo tuangalie sasa salamu mbalimbali katika English.

KUSALIMIANA ASUBUHI:
Good morning ( Gud moning)  -  ZA ASUBUHI
Jibu: Good morning, how are you? (Gud moning, hau a yu?) -ZA ASUBUHI, UHALI GANI?
I am fine, thanks. How are you too? (Am fain, thenks, hau a y utu?)  - MZIMA , ASANTE. UHALI GANI NAWE? Au ingeweza kusemwa hivi:
I am fine, thanks.  How did you sleep ? (Am fain, thenks, hau did yu slip?)  MZIMA , ASANTE. UMEAMKAJE?
Ukiulizwa HOW DID YOU SLEEP? Jibu hivi :  GREAT ! (Gret) - (VIZURI SANA) au kama haujamka vema, basi NOT WELL (Not wel) kwamba  SIKUAMKA VIZURI.
Au kama unataka kuelezea kuwa mambo sio mazuri wala sio mabaya, ili mradi siku zinaenda unaweza sema.
I CAN’T COMPLAIN  ( I kent komplein) – SIWEZI LALAMIKA

KUSALIMIANA MCHANA
Kwa mchana waweza salimia hivi:
Good afternoon ( Gud aftanun) – HABARI YA MCHANA ?
Kuitikia: Good afternoon, how are you? ( Gud aftanun, haw are yu?) – HABARI YA MCHANA, WAENDELEAJE?
Kumbuka , katika English , hata kama mlikwisha salimiana asubuhi, bado mchana waweza kutumia salamu hiyo hiyo niliyoielezea hapo juu.

KUSALIMIANA USIKU
Good evening ( Gud ivining) – HABARI YA JIONI ?
Kuitikia: Good evening, how are you? ( Gud ivining, haw are yu?) – HABARI YA MCHANA, WAENDELEAJE?
I am fine, thanks. How are you too? (Aiem fain, thenks, hau a y utu?)  - MZIMA , ASANTE. UHALI GANI NAWE?
Jibu: I’m great , how was your day ? (Am gret, hau woz yua dei ?) – NIPO POA SANA,  JE SIKU YAKO ILIKUA VIPI ?
Jibu: It was great, thanks. ( It woz gret, thenks) – ILIKUA POA SANA , ASANTE

Kumbuka kusalimiana hata kama ni usiku tumia Good evening kama ilivyoelekezwa hapo juu. Ila kama ni kuagana au kumtamkia mtu usiku mwema ndio utumie GOOD NIGHT.

TUWASILIANE: Kwa masomo zaidi ya English tuwasiliane kwa WhatsApp 0623 029 683 au nipigie kwa namba hiyo hiyo tuzungumze zaidi namna gani nitakusaidia uweze English vema.

Share:

TABIA 9 KATIKA KUTUMIA ENGLISH AMBAZO SI NZURI HATA KIDOGO

Kama unajifunza English au undataka kutumia vizuri English jitahidi sana utumie kanuni na taratibu sahihi za uandishi na uongeaji wa kiingereza. Katika makala hii fupi nitakukumbusha mambo 9 ambayo hutakiwi kuyafanya ili usionekane unatumia vibaya English.

Katika English kuna tabia sugu ambazo ni mbaya kweli kweli ngoja nizitaje hapa chini.
1. Kutokutumia alama za maandishi kwa usahihi. Mfano pa kuweka kiulizo usiweke kiulizo. Au kutumia alama ya kushangaa wakati huhitajiki kuitumia au kuzitumia nyingi bila sababu. Ushawahi ona mtu karibu kila aandikacho humalizia na !!!!!!!
2. Kutumia vifupi vya maneno isivyopaswa mfano Its Friday badala ya It's Friday
3. Kutokutumia herufi kubwa ipasavyo mfano tunasoma kuwa proper nouns zote ni lazima ziandikwe kwa herufi kubwa ila utakuta mtu kaandika jina lake au la mkoa kwa herufi ndogo
4. Kutokutumia maneno ya kuonyesha ustaarabu kama vile please, would, may, can. Usipotumia haya utajikuta ukionekana kama vile unatoa amri au sio mstaarabu.
5. Kuandika I kwa herufi ndogo mfano: John and i are friends.
6. Kutokutumia salamu kwa ufasaha kulingana na aina ya mtu unayewasiliana nae. Mfano hufai kumsalimia boss wako au mwalimu wako HEY!
7. Katika kuongea kuna ile tabia ya mtu kujilazimisha kuiga lafudhi kama vile ni mtu wa nchi fulani matokeo yake anasikika kama kero kwa huyo anayeongea nae. Jitahidi uongee taratibu na utamke maneno kwa ufasaha lakini sio utake kuonekana wewe kuwa ni mmarekani au mwingereza kwa mfano.
8. Kutokufanya punctuation ipasavyo mfano penye kutakiwa comma usiweke comma. Mfano mzuri katika picha hapa ya post hii DON'T TEACH JOHN ina maanisha usimfundishe mtu aitwaye John, waka Don't teach, John ina maana kuwa mtu aitwaye John ndio anaambiwe asifundishe.
9. Kutokufanya juhudi kuandika maneno ya English kama yanavyotakiwa kuandikwa badala yake kufanya mazoea ya kuandika English kama Kiswahili au kuiga maneno ya watu mfano Thanks kuandika TX.

Share:

JIFUNZE ENGLISH: JINSI YA KUFUPISHA MANENO KWA USAHIHI KATIKA ENGLISH

Kanuni za kufupisha maneno katika English
Ni kawaida kuona watu wengi wakitumia vifupi katika English bila kuzingatia kanuni za lugha ya English. Matokeo ya kutotumia vifupi hivyo kwa usahihi ni kupoteza maana iliyokusudiwa.
Katika makala hii tuangalie namna sahihi ya kuandika vifupi kwa usahihi kama vile you’re, it’s , we’re, they’re,  that’s n.k.
I am kifupi chake sahihi ni I’m na sio AM kama wengi ambavyo huandika. Elewa kuwa AM ni auxiliary verb au verb to be kutegemeana na wapi imetumika , na hutumika mwanzoni peke yake endapo tuu unataka kuandika  swali. Mfano: Am Iate ? Hapa ni swali je nimechelewa ?


Kinachotokea unapochanganya vifupi katika English
Ni kwamba wengi wanapochanganya  hivyo vifupi ni kwamba huandika maneno mengine ambayo hubeba maana tofauti. Hii hutokea kwakua maneno ambayo wengi huchanganya hutamkika kwa ufanano mkubwa . Angalia mifano hapa chini:


They are kifupi chake sahihi ni They’re ila wengi huchanganya na kuandika Their.  Hata hivyo their ina maana ya YAO au CHAO, VYAO, wakati They’re  sahihi ina maana ya Wao ni.


It is kifupi chake sahihi ni It’s  ila wengi huchanganya na kuandika Its. Hata hivyo Its maana yake YAKE, WAKE n.k, wakati It’s sahihi ina maana ya Yeye ni .

You are kifupi chake sahihi ni You’re  hata hivyo wengi huandika Your. Hata hivyo  Your ina maana ya Yako, wako au Chako, wakati You’re iliyo sahihi ina maana ya Wewe ni .


That is kifupi chake sahihi ni That’s hata hivyo wengi hukosea kwa kuandika Thats. Hakuna neno thats, hivyo kuacha mtu aonekane


Will not kifupi chake sahihi ni Won’t , hata hivyo kwa makosa wengi huandika wont bila kuwa apostrophe , hata hivyo hilo neno wont lisilo na apostrophe humaanisha kitu tofauti kabisa yaani tabia  fulani ambayo mtu kaizoea.


Shall not kifupi chake sahihi ni Shan’t , hata hivyo wengi huandika kimakosa bila kuweka apostrophe hivyo kuwa shant ambayo inaweza kumaanisha kukosea, au kujisaidia kwenye nguo au mtu aliyejisaidia kwa nguo yake.


Vifupi vyenye kubeba maana tofauti tofauti hata vikiandikwa kwa usahihi katika English
Inabidi kuwa makini na maneno yenye apostrophe na S kwa sababu huweza kuwa na maana tofauti. Jinsi ya kujua maana sahihi ni wewe kusoma kwa umakini sentensi nzima na mazingira ya sentensi kujua maana halisi iliyokusudiwa. Angalia mifano hapa chini:
She’s .. inaweza kuwa She is, She has au She was
Mifano: She’s gone to school - hapa She’s inasimama badala ya She has .
She’s eating .. hapa she’s inasimama badala ya She is.
She’s on the phone when I came in. Hapa She’s inasimama badala ya She was.


Zingatia hilo tulilolisoma hapo juu  kwa maneno He’s , It’s .


Mifano zaidi ya vifupi
Picha ifuatayo inaonyesha mifano zaidi ya vifupi zaidi katika English. Soma kwa umakini vifupi kama vile  vifupi vya Should have, would have, could not, would not n.k
Mifano ya kufupisha maneno katika English

Kama umeinjoi somo hili tafadhali share na wengine wajifunze zaidi huko Facebook au kwa WhatsApp. Na kama unataka kujifunza zaidi tuwasiliane kwa WhatsApp +57 301 297 1724 au kwa email john.myungire@gmail.com tuna group maalum la WhatsApp utakaloweza kufanya mazoezi ya unachokijua na wengine na kupata kurekebishwa.
Pia tuna mwalimu ambaye ataweza kukufundisha wewe mwenyewe binafsi kwa kukubaliana muda na namna ya kusoma. Hauna haja ya kutoka kwako au ofisini kumfuata mwalimu. Utaweza soma yote kupitia simu yako ya mkoni. Tuwasiliane ujue zaidi utaratibu huu wa mwalimu wa English upoje.

Share:

JIFUNZE ENGLISH:MAMBO 6 YA KUFANYA ILI KUJIFUNZA ENGLISH KAMA HUJUI KABISA

Badala ya kuita kichwa cha habari jinsi ya kujifunza English kama hujui tungeweza pia kusema jinsi ya kujifunza lugha yoyote ya kigeni kwa mara ya kwanza kwani utakayosoma hapa ni mambo ambayo hata mie niliyafuata nilipojifunza lugha nne za kigeni zikiwemo English na Spanish. Kanuni au mbinu utakazosoma hapa ndizo ambazo nimekua nikizifuata kwa miaka zaidi ya 10 nikifundisha English kwa watu wa viwango tofauti vya elimu ikiwemo wale walioishia elimu ya shule ya msingi, walioshia sekondari na wale wa vyuo vikuu.nitakupatia



1.Fahamu  kila lugha ina muundo wake maalum
Elewa kuwa lugha unayoongea wewe Kiswahili ina muundo tofauti na namna tofauti za kuandika na kumaanisha mambo. Lugha yoyote ni sehemu ya tamaduni ya wazawa wa lugha hiyo hivyo kufahamu lugha inabidi uielewe lugha husika kwa mtazamo wa hiyo lugha sio kama wewe unavyoielewa lugha yako ya Kiswahili.
Hapa namaanisha kuwa fahamu aina za maneno na kanuni zinazohusika na maneno hayo. Mfano I am going to school . Kwanza fahamu katika sentensi hii kuna maneno MATANO yaani 1. I  2. AM 3. GOING 4. TO  5. SCHOOL. Haya maneno  yanaangukia katika aina mbalimbali za maneno. Kwenye English tuna aina hizi za maneno nouns, pronouns, adjectives, adverbs, verbs, prepositions, conjunctions na interjections. Kufahamu hatua kwa hatua jinsi kila aina ya maneno hapo juu inavyomaanisha na inatumikaje ni muhimu sana ili uweze kujua utatumiaje maneno.
Tumesema English ina muundo tofauti kwani kuna namna tofauti za kuunda sentensi kwahiyo usipojua vema utajikuta ukitaka kutafsiri neno kwa neno toka English kwenda Kiswahili na usiweze kuleta maana sahihi. Au utataka kutafsiri Kiswahili kwenda English neno kwa neno na usipate maana iliyo sahihi.
Kwahiyo mwanzoni kabisa mwa kusoma lugha yeyote, kama English ni kufahamu na kukubali kuwa kuna utofauti mkubwa hivyo basi ukubali kuielewa lugha nyingine kama ilivyo na sio kutaka kuifananisha lugha nyingine na lugha yako.
Nasema hivi kwa sababu kwa mfano katika sentensi I am going to school - tafsiri yake sahihi kwa Kiswahili ni kuwa NINAENDA SHULE. Hapa tunaona kabisa kwenye Kiswahili tuna maneno mawili tuu, wakati kwenye English sentensi hiyo hiyo imeandikwa kwa maneno matano.




2. Dhamiria kuweza English kwa ufasaha
Dhamira yako  ndio itakayoamua namna gani utajifunza na kuweka bidii katika English. Kama unajifunza English ila kichwani unajiambia kuwa hauwezi na hauihitaji kuijua kwa undani basi hivyo ndivyo utakavyoishia kwani kusoma ni kugumu na kama hauna dhamira ya kutosha, hautoweza kujituma na kuvumilia ugumu utakaokumbana nao.
Epuka marafiki ambao wanabeza ujuaji wa English kikweli kweli. Epuka maneno ya waliokata tamaa ya kujifunza English kwa ufasaha. Hujui kwanini wanasema wanayosema. Pengine wao hawakufahamu mbinu rahisi za kujifunza English, pengine toka mwanzo hawakuwa na mikakati ya kutosha, muda wa kutosha na wengine ni uvivu wa kujituma zaidi pale mambo yanapokua magumu katika kujifunza. Hivyo wao sio wewe. Kama unataka kujua English jitume wewe kama wewe, jiambie hiyo ni changamoto na wewe unaweza kabisa kuishinda.

3.Jizoeshe kusikia na kusoma English iliyo sahihi
Kama tulivyoona hapo awali kuwa lugha tofauti zina miundo tofauti ya jinsi ya matumizi ya maneno hivyo basi ukijizoesha kusikia na kusoma English iliyo sahihi  utaweza kuzoea kusikia muundo wa sentensi  na muelekeo wake.
Mfano utagundua kuwa kumbe katika English kama unataka kumuuliza mtu ameamkaje utasema tuu “How did you sleep ?” na sio kama ambavyo ungeweza sema kwa tafsiri ya moja kwa moja ya Kiswahili kwenda English: “ How have you woken up ?”
Mfano mwingine badala ya kumuita mpishi COOK wewe ukamuita COOKER, kwa sababu tuu umejiambia kama anayefundisha (teach) ni TEACHER basi anayepika (cook) ni COOKER. Au kwa mfano ukataka kusema “mambo madogo madogo” ukasema kwa English  “small small things” kitu ambacho hakipo badala yake sema tuu “minor things”.

4. Tafuta msaada wa maelekezo
Kukosea kuandika na kuzungumza kunaweza kuwa tatizo kubwa sana ila utakapokua na mwalimu au mtu wa kukusaidia kukuweka sawa ni hatua njema ya mafanikio yako katika English.
Mwalimu mzuri  atakusaidia sio tuu kujua kanuni za English bali pia kukuboresha katika kuzoea uandishi wa English kama English na sio kutafsiri toka Kiswahili kwenda English.
Kumbuka hapa Mbuke Times tunaendesha mafunzo ya English tena kupitia mtandao kiasi kwamba wewe na mwalimu wako mtaweza kuwasiliana na atakueleza kanuni zote za English na muundo wa English . Huna haja ya  kutoka nyumbani kwako au ofisini, popote ulipo utaweza kusoma kwani masomo yanaendeshwa kupitia WhatsApp, Skype , Facebook na Imo.
Wasiliana nasi kwa namba WhatsApp na Imo +57 301 297 1724 tukuelekeze namna ya kuanza masomo haya. Au tucheki kwa email: john.myungire@gmail.com

5. Soma maelezo toka vyanzo mbalimbali
Pamoja na kwamba sisi hapa Mbuke Times tumeandika kitabu chetu kabisa cha English kiitwacho: English: Mbinu na Kanuni za Kuijua, ambacho kina maelekezo ya kanuni zote za msingi na mbinu za kuijua English, bado tunasisitiza wanafunzi wetu watafute kusoma vitabu tofauti na kufanya mazoezi tofauti.
kitabu_mbinu_kanuni_za_kujifunza_english_haraka

La msingi ni kuwa kusoma vitabu au kutembelea websites tofauti tofauti huchangia kuelewa kwa urahisi English kwani utakua unajizoesha kuona English ikitumika katika maeneo tofauti tofauti.
Hata hivyo, kama ndio kwanza unaanza kujifunza English , jikite kwenye kitabu kimoja ili upate mtazamo wa jumla wa English , kisha kadri unavyoendelea kujifunza ndio uongeze idadi ya vitabu au websites unazotembelea kujifunza English.




6. Fanya mazoezi ya English mara nyingi sana
Kujifunza English kunaweza kuwa kugumu sana ukizingatia na ukweli kuwa kwanza ni lugha nyingine na tamaduni tofauti. Kuna kanuni nyingi na maneno mapya ya kuyafahamu. Yote haya kuyafahamu yanataka muda na marudio ya mara kwa mara ili yakae kichwani. Usipokua na nafasi ya kufanya marudio marudio utasahau na hivyo utaona kuwa kusoma English ni shida.
Jitume usome mara kwa mara kwa bidii zote utaweza. Katika hili utaona umuhimu wa mwalimu binafsi maana atakusaidia kukupatia mazoezi ya mara kwa mara na kukusahihisha.  Kuwa na mwalimu kutakufanya uwe na nidhamu ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara, ila ukijiachia wewe mwenyewe utapitisha tuu muda wa kusoma.
Kumbuka Mbuke Times itakupatia mwalimu binafsi wa kukuelekeza , kukupatia mazoezi na kukusahihisha. Tucheki kwa WhatsApp +57 301 297 1724 au kwa email john.myungire@gmail.com
Share:

JIFUNZE ENGLISH: TOFAUTI 6 KATI YA AMERICAN ENGLISH NA BRITISH ENGLISH

Ninaishi na mama wa kimarekani ambapo kwakua tumezoea kuongea English mbili tofauti yaani yeye American English na mie British English huwa tunajikuta tukibaki hatuelewani mara nyingi mpaka mmoja afafanue anamaanisha nini. Kwa kadri miaka inavyozidi kuenda kutokuelewana kati yangu na mama yangu huyu wa kufikia kunapungua kwani kila mmoja anajifunza utofauti wa lugha aliyezoea mwingine na hivyo kujiboresha katika kumuelewa.
Kabla wewe halijakukuta lililotukuta sisi, nataka nikusaidie kukuelezea utofauti ambao tumeuona kuhusu American English na British English ila kwanza tuanze kueleza huwa tunamaanisha nini tukisema American English , na je tunamaanisha nini tukisema British English.

American English ni nini ?
Ni aina ya kiingereza ambacho huzungumzwa nchini Marekani. Kumbuka hata ndani ya Marekani kwenyewe kuna namna tofauti tofauti ambapo English hutumika kutegemeana na jimbo au asili ya watu, mfano English ya watu wa kusini ya Marekani ni tofauti ukilinganisha na English ya watu wa maeneo mengine kama vile Kaskazini au Magharibi mwa Marekani.

British English ni nini ?
Ni aina ya kiingereza ambacho hutumika nchini Uingereza .Hata  nchini Uingereza pia watu wa maeneo tofauti tofauti ya Uingereza huwa na utofauti wa hapa na pale katika kuzungumza, mfano mtu wa Liverpool anaweza kuwa na aina tofauti ya matamshi ukilinganisha na mtu wa Manchester.

Kutegemeana na nchi imetaliwa au imekubali kwa kiasi kikubwa utamaduni wa Markeani au wa Uingereza , nchi au mahali husika hukumbwa na matumizi makubwa ya British au American English. Mfano kwakua tulitawaliwa sana na waingereza nchini Tanzania huwa tunatumia zaidi British English. Wakati hapa nchini Colombia wamepokea sana utamaduni wa kimarekani hivyo hata English inayofundishwa hapa mara nyingi ni American English.

Tofauti kati ya American English na British English ni kama ifuatavyo:

1.Matamshi:
Katika American English T hutamkwa kama L mfano little  itatamkwa lilo, beautiful - itatamkwa byuliful.
Pia kumbuka kuwa katika American English mara nyingi hutamka kila r katika neno wakati katika British English hutamka r endapo tuu ni herufi ya kwanza katika neno.

2.Uandikaji wa maneno.
Kuna maneno mengi katika American na British English ambayo huwa yana maana sawa hata hivyo huandikwa tofuati. Angalia mfano hapa chini.
utofauti_maneno_american_vs_british_english


3.Misamiati tofauti kati ya American na British English
Kuna maneno katika American English ni tofauti kabisa na jinsi maneno hayo yanavyomaanisha katika British English, hivyo hivyo maneno ya British English ambayo ni tofauti kabisa na yale ya American English. Angalia mfano hapa chini.
misamiati_american_vs_british_english

4.Matumizi ya Past Simple vs Present Perfect
Katika American English huwa badala ya kutumia present perfect mara nyingi hutumia simple past tense , mfano  Nimekula ugali - I ate ugali hii ni American English, ila  kwa British English huwa tunasema I have eaten ugali.
Mfano mwingine : Je umemuona mwalimu ? Kwa American English tumia Simple Past hivyo ingekua Did you see the teacher ? Ila kwa British English tunahitaji kutumia Present Perfect Tense : Have you seen the teacher ?

5.Matumizi ya neno Get
Kwenye American English huwa tunatumia  gotten , ila kwenye British English huwa tunatumia got. Mfano:  Nina matatizo mengi  - I have gotten many problems. Ila kwenye British English tutatumia I have got many problems.

6.Majina ya jumla - collective nouns:
Kwenye American English , majina yanayoonyesha makundi kama vile team, band  huandikwa kama ni majina ya umoja, ila kwenye British English huwa tunaandika kama vile ni wingi, mfano:
American English:  Real Madrid is a soccer team from Spain.
British English: Real Madrid are a football team from Spain.
Tafsiri: Real Madrid ni timu ya mpira wa miguu kutoka Hispania.

Hitimisho:
Hapa Mbuke Times tumekuandalia masomo mengi ya kukuwezesha kujua vema English. Bofya link hii kujifunza zaidi.
Pia tuna group la WhatsApp ambalo utapata nafasi ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara na kuongea na wengine English na pia kupata kusahihishwa pale unapokosea English.   Na kama hiyo haitoshi tuna darasa maalum la wewe na mwalimu tuu - personalize English class , ili ufundishwe kuendana na matatizo yako ya English, haijalishi kiwango chako cha Elimu ni kipi, tuna wanafunzi wa darasa la saba hadi wa Masters degree. Kila mmoja kwa nafasi yake atafundiswa tena kupitia mtandao, hivyo popote ulipo unaweza kujifunza. Tuna wanafunzi waliopo nje ya Tanzania, na karibu mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani. Njoo ujifunze na wewe. Kumbuka kutuandikia meseji WhatsApp +57 301 297 1724 au john.myungire@gmail.com
Share:

NAMNA 4 AMBAPO TENSES ZITAKUPA MSINGI WA KUONGEA ENGLISH KWA UFASAHA

Karibu kila unachotaka kukizungumza katika English utahitaji kutumia tenses kuelezea hicho unachotaka kukieleza.
Tunaposema tenses tunamaanisha namna ya kuelezea muda na hali ya tukio. Kwenye tenses tuna tenses kuu tatu yaani past , present na future.
Halafu kwa kila mojawapo ya hizo tenses tuna hali kuu nne za continuous(kuendelea), perfect(kukamilika), simple (kawaida) na perfect continuous(kukamilika kunakoendelea).

Hivyo kwa mfano tukitumia perfect tenses hutuongoza kujua  sio tuu  kwa mfano ukamilifu wa tukio bali ukamilifu huo uliotokea muda gani yaani je tukio lilikamilika wakati uliopita ? au limekamilika muda mfupi uliopita au litakamilika muda ujao.

Makala hii inakupa mwanga kuhusu namna gani kufahamu tenses kutakupa msingi imara wa kuongea English kwa ufasaha.

1. Wakati sahihi wa tukio kufanyika:
Tenses hutumika kusema kama tukio lilifanyika wakati uliopita, litafanyika wakati ujao wakati uliopo. Bila kujua vizuri kuwa kuna tenses kuu tatu yaani past, present na future, itakua ngumu kwako kutoa sentensi ukizingatia taarifa sahihi. Mfano: Yesterday , she is eating - mtu akiwa anamaanisha kuwa jana alikula. Hapa kuna tatizo kwani mtu huyu hajazingatia ukweli kuwa IS EATING.. Inamaanisha wakati uliopo, hivyo haiwezi kutumika kuelezea tukio la wakati uliopita.

2. Hali sahihi ya tendo:
Kama tulivyoona hapo juu kuna hali kuu nne. Usipozijua hizo hali vizuri unaweza kutoa taarifa isiyokamili. Mfano: Unataka kusema Nimekula ila wewe ukasema I eat. Hapa umechanganya hali za perfect na simple hivyo ukisema I eat ina maana ya Mimi hula. Yaani ukisema I eat  ina maana ya tendo hilo hufanyika  mara kwa mara au ni tendo la kawaida. Ila  kusema tendo limekamilika unahitaji kutumia present perfect tense, hivyo ungesema I have eaten.

3. Je ni kauli ya kutendewa au kutenda:
Tenses zitakuwezesha  kutambulisha kama  unatumia kauli ya kutenda au kutendewa hivyo uweze kukamilisha sentensi kwa ufasaha.
Mfano: Unataka kusema :”Nilikula” ila unaandika hivi: I was eaten , hata hivyo kusema I was eaten hii ni kauli ya kutendewa yaani passive voice hivyo sentensi  I was eaten ina maanisha “ Nililiwa”. Ili uweze kusoma vema passive voice  unatakiwa ujue tenses kwanza.

4. Je kuna sharti katika sentensi husika
Tenses zitakusaidia kujifunza vema namna ya kuandika na kuongea sentensi zenye kuonyesha masharti au vitu vinavyotegemeana. Sentensi hizo kwa  English huwa tunaziita conditional sentences. Nasema tenses zitakusaidia kujua conditional sentences kwakua conditional sentences zote zinaandikwa kwa kuunganisha tenses fulani fulani. Mfano: Conditional sentences type 1 huandikwa kwa/ kuweka IF kisha Simple Present Tense…. Halafu malizia sentensi kwa kutumia Simple Future Tense. Mfano: Kama akija nitamuona. If he comes , I will see him. Hapa tunaona kuwa he comes  hii ni simple present tense, na  I will see him ni Simple Future Tense

Hitimisho
Kuunda sentensi katika English kunahitaji umakini mkubwa sana haswa kwenye matumizi ya tenses , na tumeona hapo juu kwanini unahitaji kujua tenses kwani jinsi utakavyounda sentensi unahitaji kuzingatia hayo mambo niliyotaja hapo juu ambayo yenyewe ili uyafanye vema unahitaji kujua kutumia tenses.
Kwahiyo kila uandikapo au kutaka kutamka sentensi ya English jiulize yafuatayo :
Kwanza :Je sentensi ipo katika tense gani ? - past, present, au future ?
Pili: Je sentensi inaonyesha hali ipi -perfect, continous, simple au perfect continous ?
Tatu: Je sentensi ni passive voice au sio passive voice ?
Nne: Je ni conditional sentence ? Kama ndio je ni  type zero, type 1, type 2 au type 3 ?
Katika kujiuliza maswali yote hayo utaona namna gani tenses zinavyohitajika.

Unatimizaje ndoto yako ya kujua tenses na English kwa ujumla ?
Tazama ukurasa wetu wa Jifunze English utaona makala kibao . BOFYA HAPA KUJIFUNZA ENGLISH BURE
Tuwasiliane kwa WhatsApp +57 301 297 1724 au john.myungire@gmail.com  ujipatie kitabu cha English chenye maelezo mazuri kuhusu tenses zote.
Kumbuka pia tunaendesha masomo binafsi kwa mtu mmoja mmoja anayetaka kujua English kwa ufasaha. Tuwasiliane uanze sasa kutimiza ndoto yako ya kujua English.
Share:

JIFUNZE ENGLISH: JINSI YA KUTOA MAELEKEZO AU AMRI KATIKA ENGLISH

Katika mawasiliano ya English ni muhimu kujua kuongea kwa namna sahihi hivyo basi ndio maana katika somo hili utaangalia namna ya kuandika na kuongea sentensi ambazo ni za kutoa maelekezo au tuseme kuamrisha. Sentensi hizi kwa English huitwa imperatives au command.

Jinsi ya kuunda sentensi ya kuamrisha/kutoa maelekezo katika English
Sentensi zote za kuamrisha katika English zinafuata kanuni kuu mbili :
Kwanza huwa na verbs zenye infinitive,
Yaani matendo yanayotajwa huandikwa au kusemwa bila kuyabadilisha vyovyote vile mfano tunajua kula ni EAT , basi utataja hivyo hivyo EAT bila kuanza kufikiria kwa namna gani ubadilishe nyakati ya hiyo verb husika.
Mfano mwingine tukio la kulala ni  SLEEP basi utatumia hilo hilo neno sleep bila kujiuliza ni kwa namna gani utabadili.
Pili daima kumbuka sentensi huwa zinaelekwa kwa nafsi ya pili
Yaani kwakua ni amri basi anayepokea  hiyo amri ni WEWE au NINYI kwa English tunasema YOU.
Hivyo basi ndio maana tunasema:
Sit down !  - Kaa chini  ( Yaani wewe au ninyi kaeni chini).
Go ! - Nenda ( Yaani wewe nenda au ninyi neneni)
Get out ! ( Yaani wewe toka au ninyi tokeni)

Kwanini uzingatie kuelewa jinsi kuamrisha na kutoa maelekezo kulivyo katika English
Ni kwa sababu wakati mwingine kama utatumia sentensi za namna hii bila kukusudia kutoa amri au maelekezo utajikuta ukieleweka vibaya. Hivyo kwa mfano kama unataka kuomba kitu au kupatiwa ufafanuzi fulani usiandike sentensi yako kiasi kwamba ikaonekana ni kama vile ni amri.
Na wajua wazi kama unataka kuomba kitu halafu ikaonekana kwa sababu ya ongea yako kuwa ni kama una amrisha, haitojenga picha nzuri na hivyo hutopewa unachotaka.

Namna ya kutoa amri au maelekezo ila usionekane unafanya kwa ukali
Ili usionekane mkali katika kitu unachotaka mtu afanye tumie neno please, can, could au would.
Mfano:
Please don’t come here badala ya  Don’t come here !
Would you sit down  ? Badala ya Sit down !
Can you come here ? Badala ya Come here !
Pia waweza tumia sentensi fupi kabla ya kutoa maelekezo. Sentensi zenyewe ni kama vile:
Would you mind….,  Would you please….,  I was wondering if  you can …..,
Mfano: Would you mind  to sit down ?  I was wondering if you can go .

Hitimisho:
Ni muhimu sana kujua kanuni na jinsi ya kuongea vizuri English. Tatizo la kutokufuata kanuni na miongozo ya English ni kuwa utajikuta unachoelezea kikaeleweka tofauti.
Kwa maelekezo zaidi ya English ingia kwa group letu la WhatsApp la JifunzeEnglish, kwa kutuma maombi yako kwa namba +57 301 2971724 au +255 757 120 020. Jitambulishe na useme unahitaji kusaidiwa nini.
Share:

JIFUNZE ENGLISH: MAMBO 5 YA KUFANYA ILI UJIAMINI KATIKA ENGLISH



Safari ya kujfunza English ni ndefu na kwa bahati mbaya watu wengi hupita katika safari hii kwa mateso makubwa kwakua hawajiamini katika kuongea na kuandika English. Makala hii ni sehemu ya jibu nilimpatia mwanafunzi wangu Abdi Mkizu, ambaye alitaka kwanini kwa zaidi ya miaka kumi sasa amekua akijifunza English hata hivyo bado anashindwa kuongea kwa kujiamini wakati baadhi ya marafiki zake wanaweza kuongea vizuri. Anauliza, je ni kwa sababu amekosa kujiamini katika English, na je afanyeje ili apate kujiamini.

Jichukulie wewe ni mwanafunzi wa daima
Kupoteza kujiamini kunawezekana kuwepo kwakua tayari haujichukulii kama mwanafunzi. Unadhani kuwa umeshajifunza vyote vya kujifunza hivyo sasa ni wakati wa kuongea English kwa ufasaha. Ila ukweli ni kuwa sote ni wanafunzi wa lugha wa maisha kwani hata Kiswahili chetu tuu hubadilika badilika mara kwa mara na pia hatukijui vizuri.
Ukijihesabia wewe kama mwanafunzi wa English wa milele, hautoogopa kukosea, maana kukosa kujiamini huja kwa sababu ya hofu ya kuogopa kukosea.
Kama kuna watu fulani wanakukera au kukukatisha tamaa katika kujaribu kwako English, hao watu waepuke kwa kuanzia. Fanya mazungumzo ya English na watu waelewa au na watu ambao kweli unaweza jifunza kutoka kwao, na wanaweza kukurekebisha. Weka mazingira katika kuwasiliana kwa English yanayoonyesha kuwa kweli upo katika kujifunza na upo tayari kukosolewa na kusaidiwa.

Shinda hali ya kujisikia iliyo ndani yako
Wakati mwingine mtu unaweza kushindwa English ni kwa sababu unajisikia kuwa wewe ni bora sana, au ni wa hadhi fulani, iwe kielimu, kimadaraka, kifedha au kiumri  uwa huwezi kuonekana unakosea mbele ya wengine. Unataka utengeneze picha kuwa wewe unajua English, kwakua unajiamini kuwa watu wanakutegemea wewe kuwa na kiwango fulani cha English.
Kumbuka lugha yeyote haina kazi zaidi ya kufanya watu wawasiliane.  Sasa kama wewe utaendelea kujisikia kuwa kwa umri wako, elimu yako au nyadhifa yako kuwa eti huwezi kuonekana unakosea, jiulize je kwako English itakua na kazi gani zaidi ? Chukulia kujua English ni kama kujua kupika. Kuna maana gani ujue kupika kama haupiki chakula chochote ? Hata kama hakitotoka chakula kizuri kama unavyodhani watu wanategemea, la msingi jua wewe upo katika safari ya kuweza kupika msosi mzuri zaidi siku moja. Usikubali kuishi kwa kuogopa maneno ya watu au kutaka kuwapendeza watu.

Kumbuka haushindani na mtu yeyote:
Wakati mwingine kule kutokuajimini kunakuja kwasababu unadhani kiwango chako cha English inabidi kiwe kama cha fulani, au kwanini fulani anajua zaidi English kuliko wewe. Binadamu tupo tofauti, hivyo tuna uwezo tofauti katika kujifunza lugha. Jiambie tuu kuwa la msingi katika kujifunza lugha ni kuweza kuwasiliana. Kama unaweza kuelewa na wewe kueleza vitu vikaeleweka basi upo katika nafasi nzuri katika English. Na kwamba taratibu hatua kwa hatua ukiendelea kuitumia English utakuja kuweza vizuri.
Usijilanganishe na jinsi mwingine anavyotamka kwa ubora zaidi kuliko wewe, au mwingine anavyoandika status bomba kuliko wewe. English unayotaka kuijua ni kwa matumizi yako wewe na sio kama anavyohitaji mtu mwingine. Pia hujui mazingira aliyojifunza huyo mwingine, inawezekana alijifunza kwa urahisi zaidi yako au amepata fursa nyingi zaidi za kuitumia English kuliko wewe. Ni wakati wako sasa na wewe kuitumia kila fursa uipatayo kuzungumza au kuandika kwa English.

Haitoshi kujiona unajua endelea kujifunza English:
Kutokujiamini huja kama tayari umeshajihakikishia kisaikolojia kuwa kwa muda uliotumia kujifunza English, kwa “materials” uliyo nayo, ni lazima tuu uwe unajua au umefikia kiwango fulani cha English. Hivyo basi inapotokea ukashindwa kutamka sentensi fulani, au kuelewa mazungumzo fulani, wewe mwenyewe utajiangalia kwa mtazamo mbovu, kuwa kumbe wewe ni bure kabisa, au kujiambia maneno kama vile basi kumbe hautoweza English.
Hata hivyo nakusihi uamini kuwa lugha haina mwisho katika kujifunza. Inawezekana kabisa ni kweli ulijifunza kwa umakini hivyo ambavyo ulijifunza, hata hivyo kuna vitu vingine muhimu na mbinu kadhaa bado haukujifunza.  Hivyo unapokosea au kushindwa kutunga sentensi au kuelewa sentensi fulani, badala ya kupoteza imani, unatakiwa hapo ndipo upate hamasa ya wapi haswa unaweza kurekebisha.

Tambua madhaifu yako katika English yapo wapi:

Jiulize katika kutojiamini kwako kuandika na kuongea English ni mambo gani haswa unadhani huyafahamu vizuri au utayakosea endapo utaongea au kuandika. Kuwa mkweli kwako wewe mwenyewe kwani inawezekana huko kujiona haujiamini ni kiashirio kuwa kuna mambo kadhaa inabidi ujifunze, ila wewe badala ya kutilia mkazo hayo mambo unayotakiwa kujifunza ili ujiboreshe, wewe unakataa bila kujua kwakua kukiri kuwa kuna mambo ambayo kweli bado inabidi ujifunze ni kujirudisha nyuma katika fikra zako za kwamba wewe tayari unajua English. Bila kujijua unapenda “idea” kuwa wewe upo fiti katika English, wakati ukweli ni kuwa bado kuna mambo mengi inabidi ujifunze.


Hitimisho

Mara baada ya kujifunza hayo yote niliyoeleza hapo juu ya namna ya kujiamini katika kuongea na kuandika English , unatakiwa mara moja uanze kuyafanyia kazi. Tafuta nafasi ambapo unaweza kweli ukatumia hiyo lugha. Ndio maana nilitengeneza group  la WhatsApp la JifunzeEnglish ili kwamba wewe na wengine wote wenye kutaka kufanya mazoezi ya kuongea na kuandika English muweze kupata hiyo nafasi ya kutumia English , pia kujifunza kutokana na makosa ya wengine.  Ni matumaini yangu kuwa katika group hili utajisikia huru kuongea na kukosea, lakini zaidi sana utajifunza kuwa haupo peke yako katika kukosea kwani mimi kama mwalimu, nipo kurekebisha wote wanaokosea.

Kama haujajiunga na group letu la WhatsApp la kujifunza English, nitumie maombi yako ya kujiunga kwa namba +57 301 297 1724. Na kama unataka darasa lako binafsi la English pia wasiliana nami, uanze kuweza kweli kujifunza English.

Share: