PICHA:KAA MBALI NA BLOG ZA NAMNA HII NI AIBU KUBWA KWA TAIFA

Kumekuwepo na wimbi la vijana wengi wanaoingia katika uwanja wa blogging bila kuwa na ujuzi na uelewa wa nini haswa cha kufanya cha msingi. 
Wengi wa vijana hao wanachojali ni kuandika kupata tuu clicks nyingi kwa blogs zao hivyo hata habari za uongo na zisizo na maana wataziweka. 

Ni wazi kuwa vijana wanaofanya hivi tayari wamekwishapoteza matumaini ya kufanya mambo ya maana kwa jamii , na hakuna namna ya kuwarekebisha. Kwani kuandika vitu vya namna hii ati ili mradi tuu upate watu wa kutembelea blog yako, sio tuu kwamba ni wizi wa muda wa watu wengine na kuwapotezea MB zao, bali pia kunawarudisha nyuma hao waandishi wenyewe kwani wanajijaza ujinga wa kuwa hii ndio njia sahihi ya kujitafutia riziki.

Badala ya kujenga blogs za kuheshimika kiasi kwamba hata watu wenye biashara zao au asasi nyingine za heshima ziweze hata kuvutiwa kutangaza huko kwa blog zao, wao wamekazana na ujinga huu ambapo hakuna asasi ya kuheshimika itakayopenda kuhusanishwa na blog ya namna hii hivyo hawataweza kutangaza huko.

Lengo la vijana hawa ni kupata matangazo kupitia Ad Sense hata hivyo Google wana taratibu na sheria kali kuhusu huduma hiyo na sio kila blog yenye kutembelewa sana itapata kukubaliwa kuweka matangazo ya Ad Sense. 

Hivyo wito kwa vijana wengine wanaotamani kuingia katika blog na kuendeleza mtindo huu wa blog zisizo na maana, ni kuwa sio rahisi kihivyo kutengeneza fedha kupitia Google kwa kuweka tuu habari za uongo na kurubuni watu watembelee blog yako.

Badala ya kupoteza muda wako na muda wa watu wengine , ni bora ujikite kufanya mambo ya msingi ya kukuingizia fedha. 

Zifuatazo ni baadhi ya posts za blog za aina hiyo.


Share:

0 comments:

Post a Comment