Picha na foter.com |
Kama unataka kuanzisha biashara, au umekwisha anzisha, basi hii mada
inakuhusu. Na hata unataka kuajiriwa au unatafuta kazi bora zaidi uliyonayo, ni
jambo la msingi kujua namna ya kuwa na Brand inayouzika.
Maana ya Brand
Branding
ni namna ya kutengeneza HISIA chanya mbele za hadhira. Ni namna unavyotaka wafikirie na waitambue
bidhaa husika au asasi.
Mfano
ukisikia MBUKE TIMES unapata picha ya sehemu penye tafakari za kipekee, mambo
ya kujenga na habari zenye uhakika. Ni kusudio langu ku BRAND Mbuke Teims kwa
mtindo huo.
Kuna mengi ya kufanya ili kujenga hisia hizo- jinsi unavyowasiliana
na hadhira , huduma kwa wateja, aina ya bidhaa zako, uwajibikaji wako
kiutendaji n.k
Hii sio
maana ya Brand
Brand sio rangi , sio logo, sio jina la bidhaa. , bali ni nini vitu kama hivyo
vina leta hisia na vinasadia kufanikisha lengo la uwepo wa bidhaa/asasi au mtu
husika.
Kwanini unahitaji kuwa
na Brand
Kama tulivyoona katika maana ya Brand, lengo kuu la Brand ni kufanikisha
kukubaliwa mbele ya wale unaowalenga, hivyo basi unahitaji Brand ili
kujiwezesha kupata kazi bora unayoihitaji kwani kwa picha nzuri utakayoijenga
kwa jamii , unaweza kupata watu watakaotaka kufanya nawe kazi.
Pia Brand inakusaidia pale unapotaka kuanzisha biashara , au kama tayari
unayo biashara basi inakurahisishia kuuza bidhaa zako nyingine mpya.
Brand inakufanya ujenge mtandao na watu wa muhimu katika fani yako,
ajira na biashara.
Je unatengeneza Brand yako ?
Kwanza
kabisa inabidi ujijue unapenda kufanya nini na nini utakachotoa kwa jamii kama
bidhaa. Mfano kama lengo lako ni kutoa huduma za michezo mfano mpira wa miguu,
basi utajikita katika kujifunza kwa undani kuhusu mambo ya mpira wa miguu,
kushiriki katika michezo na kushare habari za kina kuhusu mpira wa miguu.
Hata hivyo haitoshi tuu kuonekana upo fiti katika hicho bidhaa yako ,
bali pia uwafanye watu wengine wapende kuwa karibu nawe. Hapa ndipo kazi ya
ziada inahitaji katika namna yako ya kufanya mawasiliano.
Kumbuka mawasiliano ni zaidi ya unachozungumza, hata namna ya mavazi
yako, lugha yako, umakini wako, tafakari zako, jinsi ulivyo wa msaada, mtandao
wako n.k vyote vitakusaidia kujitengeneza kama BRAND.
Jitokeze ufahamike
Kujifunza na kuwa na kitu cha maana cha kutoa kwa jamii hakutoshi kama
haujafahamika na kuanza kujenga Brand. Tafuta nafasi ya kuzungumza na makundi ya watu unaowalenga.
Tumia mitandao ya kijamii kwa faida ili kuifanya jamii ikutambue kwa namna
unavyolenga kuja kutoa bidhaa yako.
Hitimisho
Fikiria
na amua leo, je wewe unataka kutambulika kama mtu wa namna gani? Anza kujijenga kama BRAND !
Kumbuka
tunatengeneza BRANDS ili kunufaika hususani kifedha na kimaendeleo. Haijalishi muda gani
utachukua kabla ya kuweka BRAND imara, ila kumbuka INALIPA kufanya hivyo.
Waweja
jibrand kama MTU MAKINI, MWAMINIFU, MCHAPAKAZI halafu uone matokeo yake. Ila inahitaji kazi na mikakati kufikia huko.
0 comments:
Post a Comment