MAMBO 4 YA MSINGI ILI KUPATA SCHOLARSHIP YA ELIMU

Haraka haraka unapoliona tangazo la Schorlaship,unajisikiaje? Je, umekata tamaa ya kupata schorlaships? Pengine bado unayo nafasi ya kupata scholarship, endapo utazingatia mambo ya msingi. Makala inadokeza mambo hayo ya msingi.  

1. Kupata nafasi ya chuo : Ni wazi kuwa unataka schorlaship (uhisani) ili kusoma katika chuo fulani, basi ni muhimu kwanza uwe umepata chuo. Unahitaji kupata chuo kwa sababu kuu zifuatazo:
  • Kwanza mhisani unayetegemea akufadhili ni muhimu kwake awe na uhakika kuwa unakidhi viwango vya kusoma kozi fulani, na kuthibitisha hivyo, ndio maana umeweza kukubaliwa kujiunga na chuo husika.
  • Pili, unapokuwa umekubaliwa katika chuo fulani maana yake utapokea maelekezo ya gharama zote za masomo yako chuoni hapo, na pia itakuwa rahisi kwa mhisani kuwa na uhakika wa gharama unazomtajia.
  • Tatu , wahisani wengi hutoa ufadhili moja kwa moja kupitia vyuo, hivyo unapokuwa umepata kukubaliwa na chuo fulani, basi ni rahisi kuomba ufadhili toka kwa wahisani wanaofadhili kupitia chuo husika ulichokubaliwa. Mfano: MASTER SCHORLASHIP IN SWEDEN
2. Maandalizi kabla ya kuaply:
  • Hakikisha una matokeo mazuri ya darasani: Wahisani wanataka kuwa na uhakika kuwa utaweza kuhitimu masomo watakayokufadhili, hivyo basi matokeo yako mazuri ya darasani kabla ya ufadhili wako, ni dalili nzuri kuwa unao uwezo wa kuenda kusoma na kufanikiwa kumaliza hivyo, fedha za wahisani hazitopotea bure. Baadhi ya wahisani huenda mbali zaidi kwa kutaka kufahamu kuwa elimu watakayokupatia itakuwa kweli ya manufaa kwako na kwa jamii hivyo hupenda kupata maelezo toka kwako namna ambavyo utaitumia elimu utakayopata. Ndio maana maombi yako ya ufadhili mara nyingi huambatana na barua ya. kujitambulisha na kujieleza malengo yako kuhusiana na fani unayoenda kuisomea.
  • Hakikisha lugha hususani kiingereza kinapanda vema: Nimetaja hapo juu, kuwa kuna kujieleza kuhusu fani unayoenda kusoma inavyoendana na malengo yako na manufaa kwa jamii kwa ujumla. Utaweza kujieleza vema kupitia lugha mara nyingi ni kiingereza.
  • Boresha uwezo wako wa mawasiliano: Utahitaji kuandika barua na wakati mwingine hata kuhudhuria usaili wa ana kwa ana na wahisani, hivyo uwezo wako wa kufanya mawasiliano fasaha ni muhimu. Jizoeshe kufuata kanuni za mawasiliano fasaha. Rudia tena kusoma Communication Skills.
3. Wakati wa kuapply
  • Soma maelekezo vema:  Amini usiamini, kila elekezo lililowekwa katika tangazo la schorlaship lina kusudio lake maalum, hivyo basi hakikisha unasoma maelekezo yote, na tena kwa ufasaha. Hii inajumuisha,  kusoma mambo kama vile lini mwisho wa kuapply, mambo gani unatakiwa kueleza katika barua ya maombi, nyaraka unazotakiwa kuambatanisha wakati wa kutuma maombi, jinsi ya kutuma maombi n.k.
  • Fuata Maelekezo kwa usahihi: Kusoma tuu maelekezo haitoshi, bali unatakiwa uyafuate vema.
4. Nini cha kutarajia kuhusu Schorlaships
  • Gharama zitakazolipiwa: Tambua pia inawezekana kabisa wahisani wasifadhili kila aina ya gharama za masomo yako. Hivyo unaweza kuendelea kutafuta wahisani wengine zaidi ili kupata ufadhili wa kutosha kulipia gharama zako. Msisitizo hapa ni kuwa usiwaze tuu kupata mfadhili mmoja , angalia uwezekano wa ufadhili mwingine, na pia wewe mwenyewe namna unavyoweza kujilipia.
  • Schorlaship za kusoma ndani ya bongo zipo: Ni kukumbusha tuu kuwa kuna schorlaship nyingine nyingi tuu za kusoma kwa vyuo mbalimbali ndani ya Tanzania. Tembelea mara kwa mara websites za vyuo kama UDSM.
 

Share:

21 comments:

  1. Hii kitu (muongozo) imekaa vizuri sana. Ila scholarship za bongo ziko kimagumashi sana sasa hivi. Sio kama zile za zamani. Zina siasa nyingi sana.

    ReplyDelete
  2. Mwongozo upo vizuri nimeuelewaa bro

    ReplyDelete
  3. Shukran sana.. Pia nilihitaji kufahamu japokuwa taasisi moja au mtu binafsi anayeweza kunipa msaada huo wakielimu nilihitimu kidato cha sita 2017 na nina vigezo vya
    kuendelea na diploma kutokana na ufaulu wangu.

    ReplyDelete
  4. Nina washukuruni sani sana kwakupata haya maelezo 4.langu
    Nihili ikiwa MTU ajuwe kingereza ila anajua kiswili tu.atafanyaje?naye anahamu ya kusoma,anajiisi kusoma ni mziko kwake.A

    ReplyDelete
  5. Nashukuru kwa muongozo huo.Nilihitimu kidato cha nne 2017 nikafauru vyema,ila sikuweza kuendelea kidato cha tano.Napenda kusoma medicine ngazi ya diploma kwani vigezo ninavyo.Je naweza kupata mfadhili?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tembelea https://www.nia.ac.tz/fee-structure/

      Delete
  6. Nimejifunza kitu Asante sana

    ReplyDelete
  7. Je ili upate scholarship ya masters unatakiwa uwe na GPA ya kuanzia point ngapi

    ReplyDelete
  8. Asante kwa maelezo Bora zaidi Mimi nimemalza kidato cha sita na nimepata alama nzuri nanikaapply chuo nanikachaguliwa udom lakn kutokana nauwezo mdgo wa familia yetu inakuwa ningumu hata kulipa ada naomba msaada toka kwenu naamini mtanisaidia even through advicing me what may I do

    ReplyDelete
  9. Nimehitimu kidato cha NNE ndoto yangu ni kuwa fashion dressing designer tangu nikiwa mdogo nilitamani sana siku moja ndoto yangu itimie licha ya kuwa nakebiriana na changamoto za kifedha Ila bado nina nia sijakata tamaa hivyo kama kuna yeyote yule anaeweza kunisapport kwa kile ninachotamani kufikia hii ndo namba yangu 0653648264

    ReplyDelete
  10. Asante kwa maelezo mazuri,mimi nimemaliza certificate ya kozi ya community health na nilifaulu vizuri nahitaji sana kuendelea na diploma na degree ya community development katia chuo cha mipango Dodoma lakina kutokana na familia kukosa uwezo wakunisomesha na kuwa na mzazi mmoja tu nimekwama makini sijakata Tamaa atakaeguswa kunisaidia nitashukuru sana namba zangu ni hii 0623160456

    ReplyDelete
  11. Hello nimehitimu kidato Cha nne nahitaji nikasomee clinical medicine familia yangu Haina uwezo wa kunisomesha cjui mnanisaidiaje na hiyo ndo ndoto yangu toka utotoni sitaki kitu kingine

    ReplyDelete
  12. Thank you very much for your wonderfully guidance! In order to get masters scholarship in law what are the minimum G.P.A should I have????

    ReplyDelete
  13. ahsanteni sana kwa makala hii imeniongezea kitu kikubwa sana.

    ReplyDelete
  14. Hii ni nzuri sana. Itasaidia sana wanaotaka ufadhili, kufanya Application kwa ufasaha.

    ReplyDelete
  15. Asante sana ila nilikuwa naomba kuuliza kwa mtu ambae ameishia darasa la saba na anasoma Qt na kafaulu form 1 na tu ila ameshindwa kuendelea from 3 na 4 na anamuhitaji wa kusoma anaweza kupata mfadhili au wanawasaidia walio ingia chuo tu

    ReplyDelete
  16. Naitwa mwita Marwa chacha naomba ufadhili wa masomo nipo chuon mwaka wa kwanza kwa kozi ya uuguzi na ukunga ila mpaka sasa sjapata uhakika wa kulipia ada semisiter inayofata naomba kama ikimpendeza yeyote anisaidie namba yangu ni 0695386671 asant mungu Awabaliki

    ReplyDelete