Picha na foter.com |
Ni ukweli
usio na ubishi kuwa kwa sasa programs,
software au wengi tunazifahamu kwa jina la applications (Apps) ndio sehemu ya
teknolojia inayoongoza karibu kila kitu katika maisha. Iwe maisha yako binafsi, elimu, mahusiano,
biashara, uzalishaji , afya , ulinzi na hata usafiri na burudani vyote vinahitaji
programs.
Maana ya programming
Kwa kifupi programming ni shughuli ya kuandika programs, ambazo pia huitwa software au apps.
Yaani ni namna ya kuifundisha kompyuta ambayo ni mashine tuu, jinsi ya kutimiza hizo kazi unazotaka kufanikisha kupitia hiyo kompyuta. Utaifundisha kompyuta kupitia maandishi maalum utakayoandika ambayo kompyuta zimetengenezwa kuyaelewa na hivyo kufanya hayo unayotaka ifanye.
Maandishi hayo maalum unayoandika ili kompyuta iweze kufanya kazi unazotaka ifanye , huitwa codes.
Codes huandikwa kwa kutumia lugha maalum ambazo zinatafsiriwa na kueleweka kwa kompyuta. Lugha hizo huitwa programming languages. Zipo programming languages nyingi sana kutegemeana na aina ya program unayotaka kutengeneza , mahitaji ya spidi, na wapi unataka program ifanye kazi. Majina ya baadhi ya program ni kama vile C, C++, Java, PHP, Python, JavaScript, Ruby na Scala.
Mfano mzuri
wa program ni kama Facebook, ambapo wewe unaweza kuingia na kuandika ujumbe
wako na kupost ili watu wauone. Kuna mtu
au watu walioandika hiyo program iitwayo Facebook inayokupa wewe nafasi ya
kufanya unayotaka.
Faida za kujua programming
Hivyo basi
kufahamu programming na kwanini watu wengi wanahitajika kujifunza programming
tunatakiwa tufahamu kuwa programming
ni namna ya kutengeneza zana (tools)
ambazo watu wanaweza kutumia kufanikisha mambo kadhaa.
Mfano ilivyo Facebook ni
kwa ajili ya mawasiliano.
Kwa hiyo
programming inaanzia kwenye kujenga wazo la matumizi ya kitu fulani
utakachokiita program, mfano yaweza kuwa unataka kuwa na program ambayo
itakufanya utunze kumbukumbu za matokeo ya watoto wako, picha za matukio ya
familia, nk. Hayo ni mambo unayotaka kuyafanya kupitia program au app fulani.
Mfano rahisi wa kuandika program
Mfano ili kama lengo lako ni program
itakayowakaribisha wageni nyumbani kwako kwa kuwauliza majina yao kisha kusema
karibu na kutaja jina la mgeni husika.
Hivi ndio muonekano wa program yako unavyoweza kuwa:
Mgeni anapewa nafasi ya kutaja jina lake kisha anabofya OK |
Halafu mgeni anakaribishwa kwa kutumia neno Karibu kisha kutaja jina lake |
Program hiyo imeweza kuandikwa kwa kutumia code ifuatayo :
Programming language iliyotumika kuandika program hii inaitwa JavaScript |
Programming itakufikisha wapi ?
Hivyo basi
ukijifunza kuandika codes utaweza kuandika programs za kufanya mambo mengi
unayotaka kuyaona yakitokea. Mfano programs nyingi zimeanzishwa kwa sababu
programmers walitaka kutimiza mahitaji fulani kupitia programs ambazo
hazikuwepo. Mfano Mark Zuckerberg wa Facebook anasema hivi kuhusu
Facebook:
When I made Facebook my goal was to help people understand what was going on in their world a little better. I wanted to create an environment where people could share whatever information they wanted, but also have control over whom they shared that information with.
Yaani kwa kifupi alitaka
awe na program anayoita mazingira ya mtandaoni ambapo watu wanaweza kushare
taarifa mbalimbali . Na hivyo ndivyo ilivyo Facebook mpaka leo.
Ili kutengeneza hicho alichotaka kukitengeneza ilimbidi aandike Codes, kama
tulivyoona maana ya codes hapo juu. Na ilimbidi atumie programming languages.
Na kwa kiwango kikubwa Facebook imeandikwa na inaendeshwa kwa kutumia
programming language iitwayo PHP. Programming languages nyingine zinazotumika
katika kukuletea Facebook unayoitumia pengine kila siku ni pamoja na Java, Python, C++, Hack, Erlang, D, Haskell, na Xhp.
Hivi karibuni rafiki yangu wa Morogoro, Tanzania aitwaye Elias Tyrphone,
akishirikiana na wenzake walitengeneza App kwa ajili ya watu kuitumia kutoa
taarifa za watu waliopotea. App hiyo inaitwa NitafuteApp. Huu ni mfano wa jinsi
programming inavyoweza kusaidia kutatua matatizo ambayo wewe unayaona katika
jamii na yanahitaji program.
Hitimisho
Je umeelewa maana ya programming ? Ni matumaini yangu kuwa utahamasika
nawe kuanza kujifunza kuandika codes ili uweze kuandika programs zitakazotatua
hayo unayoyawaza iwe ni kwa ajili ya familia yako, masomoni, marafiki zako,
biashara yako au hata kutengeneza programs/apps ambazo jamii kwa ujumla
itazitumia.
Usikose sehemu ya pili ya makala hii ambapo tutaangalia namna ya kuanza
kujifunza kuandika codes.
Ila waweza anza kujifunza codes kupitia websites hizi, au cheki vitabu
vya lugha mbalimbali vya bure kwa kubofya hapa.
Noted,Kupitia makala hii najua Wengi watatamani na wataweza maana makala ime pangiliwa kwa lugha rahisi sana inayoeleweka hata kwa asiyejua sana computer ana elewa.
ReplyDeleteAhsante sana Pacoster
ReplyDeleteAHSANTE
ReplyDeleteasante,je ni wapi naweza kujifunza javascript
ReplyDeleteAsante Sana kwa kutufundisha
ReplyDeleteNashukuru kwa msaada lakin nataka kujua zaidi programming c
ReplyDeleteSafi
ReplyDeleteNimekuelewa lakn hzo code kila program inacode jinc ya kuziandika ama vp
ReplyDelete