UFAHAMU UNDANI WA SAKATA LINALOENDELEA LA APPLE VS FBI

Picha na Trustedreviews.com
Vyombo kibao vya habari ulimwenguni vinazungumzia sakata la mvutano unaoendelea kati ya kampuni ya Apple na shirika la upelelezi la Marekani (FBI). Lengo la makala hii  ni kukujuza kwa undani nini haswa chanzo chake , nini kimefanyika mpaka sasa na nini kinaweza kuendelea.

Nini kimepelekea kuwepo kwa mvutano huu
Mvutano huu unakuja kwakuwa FBI wapo katika muendelezo wa uchunguzi kuhusu shambulizi la kigaidi lililotokea tarehe 2 Desemba, 2015 huko San Bernadino, California. Katika shambulizi hilo mke na mume wote wa asili ya Kipalestina majina yao ni Syed Rizwan Farook na Tashfeen Malik walishambulia wafanyakazi wa idara ya afya ya San Bernadino waliokuwa kwenye sherehe na mafunzo maalum.

Katika shambulizi hilo watu 14 waliuawa na 22 kujeruhiwa vijana. Mke na mume waliofanya

 shambulizi hilo walifanikiwa kutoroka katika eneo la tukio hata hivyo wakiwa njiani kutoroka

 mbali zaidi polisi waliwashambulia kwa risasi na kuwaua wote wawili.


Hii ni picha gari lililotumika kutoroka eneo la tukio na washambuliaji wanandoa Syed na mkewe. Hapa kama unavyoliona likiwa limeshambuliwa vibaya kwa risasi. Picha na wikipedia.


Hivyo katika uchunguzi wao FBI wanataka kujua mambo yaliyopo katika simu ya huyo mume aliyefanya shambulizi bwana Syed.

Wanachotaka FBI toka kwa Apple
Kabla ya huu mvutano uliopo sasa FBI tayari walikwisha pokea taarifa zilizohifadhiwa kama akiba kwenye iCloud Service na mmiliki wa simu hiyo bwana Syed. Hata hivyo taarifa hizi haziwatoshi FBI kwakuwa bwana Syed aliacha kupost taarifa zaidi mwezi Oktoba 19,2015.

Kupitia agizo maalum toka mahakama ya wilaya huko Los Angeles , tarehe 16 Feb 2016 Apple walipewa siku 5 za kuwapatia FBI ushirikiano wa kiufundi ili FBI ifanikiwe kupata taarifa zote za simu hiyo ya marehemu Syed.
Hii inafuatia ukweli kuwa bila kuwa na password , wanachoweza kufanya FBI ni kujaribu jaribu password mbalimbali mpaka ipatikane ya kufungua simu hiyo, hata hivyo simu za Apple zimetengenezwa kiasi kwamba ukikosea password mara 10 basi taarifa zote zilizopo katika simu zinafutika.
Hivyo basi msaada wa kiufundi unaohitajika na FBI ni kwa Apple kutengeneza software ya kuwezesha kuondoa hizo settings za kukataza kujaribu jaribu password. 
Kwa lugha ya kitaalamu ni kuwa FBI wanataka watengenezewe mlango wa nyuma ili waweze "kucheza" wanavyotaka katika kuhack hiyo simu ya ndugu Syed.

Msimamo wa Apple katika mvutano huu na FBI
Mkurugenzi mtendaji wa Apple bwana Tim Cook ameeleza wazi kuwa kampuni yake haipo tayari kufanya hayo wanayotaka FBI kwani kufanya hivyo ni kuwaweka wazi wateja wake, kwa kuruhusu mashirika ya kipepelezi kama FBI kudokoa taarifa za wateja wao.

Msimamo wa viongozi wa makampuni ya teknolojia duniani
Viongozi wa makampuni makampuni makubwa kama Facebook, WhatsApp, Google na Microsoft ni kuwa Apple isikubali kufanya hayo  yanayotakiwa na FBI.
Naye mtaalamu wa mambo ya usalama wa mifumo ya kompyuta, mwanzilishi na mwandikaji wa software maalum ya kupambana na virusi vinavyoharibu mifumo ya mitandao, ndugu John McAffe wa kampuni ya McAffe, anasema kuwa Apple isikubali kufanya hivyo kwani kitakachotokea ni kuwa FBI ingawa inasema kuwa inahitaji kusaidiwa kufungua simu moja tuu , itakachotokea ni kuwa itatumia ujuzi huo kufungua simu nyingine.
Mkongwe wa mambo ya usalama wa mifumo ya mawasiliano alipohojiwa na RT kuhusu sakata la Apple vs FBI

Yeye bwana McAffe amesema yupo tayari kukaa chini  yeye na kundi la hackers toka kampuni yake kwa muda wa wiki zisizozidi tatu na kuwapatia taarifa zote wanazotaka FBI toka kwa simu hiyo kwani kampuni yake ina wataalamu wa kuhack walio bora kabisa. 

Nini kitaendelea kama Apple isipotoa ushirikiano:
Kwa mujibu wa RT kama Apple haitofanya inavyotakiwa ndani ya siku tano iliyopewa , basi swala litapelekwa mahakama ya juu zaidi. Na kama mahakama zaidi zitashindikana, basi itapelekwa mahakama kuu ya Marekani( US Supreme Court).

Vyanzo:
 1. Wikipedia :
https://en.wikipedia.org/wiki/2015_San_Bernardino_attack

2. RT :
https://www.rt.com/usa/333403-bill-gates-san-bernardino-iphone/
3: USATODAY: 
http://www.usatoday.com/story/tech/news/2016/02/23/latest-us-vs-apple-over-san-bernardino-iphone/80786384/
Share:

0 comments:

Post a Comment