MAANA YA SEO NA MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUFANYA SEO

 

Maana ya SEO

SEO ni kifupi cha maneno ya kiingereza yafuatayo – Search Engine Optimization. Hata hivyo hiyo sio maana ya SEO. Tunaposema SEO tunamaanisha ni jumla ya maarifa yanayofanywa ili kufanya machapisho yapewe kipaumbele kwenye search engines kama vile Google, Yahoo, Bing n.k pale mtu anapokua anatafuta kitu kupitia search engines hizo. Katika makala hii, Mbuke Times, tutakuwezesha uelewe vema maana ya SEO na mambo gani uyazingatie unapofanya  SEO.

Jinsi SEO inavyofanya kazi

Kazi kubwa ya SEO ni kuhakikisha kuwa watu wanaposearch mtandaoni kitu fulani basi website/blog yako nayo ionekane kwenye ukurasa wa kwanza wa majibu ya search husika kwamba na wewe pia una kitu ambacho wao wanakitafuta.

Tuchukulie mfano kwa search engine ya Google. Unapoandika climb Kilimanjaro, utaletewa majibu mengi kutoka websites/blogs mbalimbali. Lengo la SEO ni kuhakikisha website/blog yako inakuwepo kwenye hayo majibu katika ukurasa wa kwanza.

Mambo ya kuzingatia ili kuifikia maana ya SEO

Ili ufahamu SEO inavyofanya kazi inakupasa kwanza ujue jinsi search engines kama vile Google , Bing n.k zinavyofanya kazi.

Kwanza kabisa, fahamu kuwa Search engines zina lengo kuu la kuwapatia watumiaji wa mtandao majibu bora ya kile wanachokitafuta mtandaoni.

Hivyo basi, ili search engines ziyape kipaumbele machapisho yako ni lazima kwanza yawe yenye ubora , yaani yenye kujibu haswa kile ambacho watu wanatafuta mtandaoni.

Pili elewa kuwa search engines huanza kwanza kukusanya machapisho kutoka katika websites na blogs na kuzihifadhi taarifa hizo ili pale mtu anapohitaji taarifa basi zenyewe huchunguza katika hifadhi zake kuona machapisho yapi yanaweza mfaa haswa mtu anayetafuta kitu husika.

Hii ina maana kuwa machapisho yako yanapaswa kuandaliwa kwa namna ambayo search engines zinaweza kuyakusanya kwa urahisi na kwa ubora zaidi. Mfano unapaswa kubainisha keyword phrase, kuwepo na picha, picha ziwe na ALT text , kuwe na subheadings n.k.  Tutayazungumzia hayo yote hapo baadae.

Tatu, search engines kama tulivyoona kuwa zinamlenga mtafutaji wa taarifa apate majibu bora. Njia nyingine wanayotumia kujua kuwa machapisho ni bora ni kwa namna machapisho “yanavyopigiwa debe” ya kuwa ni bora. Machapisho hupigiwa debe kwamba ni bora kwa namna ambavyo watu wengi wameshare. Search engines hutumia links toka websites na blogs mbalimbali kupima ubora wa machapisho yako. Hivyo ni vema kufanya juhudi ili websites na blogs mbalimbali ziweze kuchapisha au kulink website/blog yako.

Nne,  watu wengi siku hizi hutumia simu na tablets kuingia mtandaoni. Hivyo ili search engine ione kuwa machapisho yako yanawafaa wale wanaotafuta taarifa mtandaoni, inakupasa ujitahidi website yako iwe inamuonekano mzuri kwenye simu na tablets.  Kitaalamu tunasema website au blog yako iwe mobile friendly.

Hitimisho:

Usikose makala nyingine ambapo tutachambua zaidi kuhusu faida za kufanya SEO.

Kama unawaza kuanza kufikiria kufanya SEO, tuwasiliane sasa kwa namba +255 623 029 683 ili tukusaidie.

Share:

0 comments:

Post a Comment