JINSI YA KUANZISHA BLOG: YOTE ULIYOTAKA KUYAJUA YAPO HAPA

Kila siku maelfu ya watu duniani wanafungua blog mpya. Pengine nawe ungependa kuanzisha blog yako. Changamoto katika blogging, ni jinsi ya kupata wasomaji wengi, na jinsi ya kuboresha blog yako siku hadi siku. Hivyo makala hii inakupa taarifa za awali za shughuli za blogging.

Takwimu
Teknolojia ya blogging, ambayo kwa mujibu wa Wikipedia, ilianza kutumika mwaka 1993, ilifikisha idadi ya blogs milioni 156 duniani kwa rekodi za mwaka 2011, Februari 26. Bila shaka idadi ya blogs kwa sasa ni zaidi ya milioni 300. Hakuna taarifa za hesabu ya idadi ya blogs za Tanzania, ingawaje kwa makadirio inaweza kufika zaidi ya elfu 50, hii ni kutokana na kuwa ni rahisi sana kuandikisha blogs kuliko kuziendesha. Tukifuatilia idadi ya blog hai, unaweza kukutana ni chache sana.

Kazi za blogs
Pamoja na kwamba wengi huanzisha blog kama jambo la kibiashara, kuna matumizi mengine mengi zaidi ya kuwa na blog kwa ajili ya kuingiza mapato. Blog inaweza kutumika kuandika habari binafsi, wengine huandika blog kama sehemu ya burudani/hobby kwakuwa wanapenda kuandika na wanapenda kutumia teknolojia, wengine huandika blog kwa ajili ya kufundisha mambo kadhaa, mfano mwalimu anaweza kuandaa blog kwa ajili ya darasa lake. Pia makampuni huwa na blog ili kutoa taarifa za bidhaa zao, pamoja ana maendeleo au mabadiliko fulani fulani katika uendeshaji wao. Wengine huanzisha blogs kama sehemu ya kutangaza bidhaa zao, mfano mzuri ni wabunifu wa mavazi wa Sinza Dar es salaam,  Rineez Arts.

Malengo: Malengo yako ya kuwa na blog, ndio yanakupa amri ya jinsi ya kuiendesha blogu husika. Mfano kama una malengo ya kuja kuuza matangazo, inabidi ujitahidi kweli blog yako ipate wasomaji wengi ambao wanajirudia rudia mara kwa mara kutembelea blogu yako. Hii ni kwasababu hakuna mtu au asasi ambayo ingependa kutangaza kwenye blog ambayo haina wasomaji- kwani matangazo yao hayatokuwa yakionekana na watu wengi. Malengo yako ndio yanaelekeza aina ya wasomaji unaotakiwa kuwalenga, na hivyo aina ya habari ya kuziweka kwa blogu yako.
Pengine kuwa na blogu ni njia tuu ya kufikia lengo fulani kubwa, mfano lengo lako linaweza kuwa ni kujenga network na watu wengi, hivyo kuwa na blog inayofahamika na watu wengi, na wewe kuwa na uwezo wa kufanya mawasiliano na wasomaji wako mmoja mmoja, ni sehemu pia ya mafanikio ya blog.

Kuandikisha blog: Kuna makampuni kadhaa yanayotoa huduma ya kurusha hewani bure blogs. Waweza kuwa na blog kupitia Blogger na kupitia Wordpress. Pia kuna Tumblr, Typepad, na Posterous. Unachotakiwa kufanya ni kujiandika kwa kampuni husika. Mfano kuwa na blogger blog, inabidi kwanza uwe na Gmail account, halafu unaenda kwenye address hii blogger home , na kufuata maelekezo ya jinsi ya kuandaa blog yako. Ambapo utaweza kuchagua jina la blog, anuani ya blog mfano mbuke.blogspot.com,na kisha utachagua muonekano wa blog yako – tunaita template. Baada ya kuchagua mambo hayo, tayari utakuwa umeweza kuwa mmiliki wa blog.

Kuendesha blog:  Kazi kubwa sio kuwa na blog, bali ni kuendesha blog, kwani kuna vipengele vingi sana vya kufuata ili kuwa na blog endelevu. Shughuli kuu za uendeshaji wa blog ni kuitangaza ili upate wasomaji wa hayo unayotaka kuandika. Kuna sababu nyingi kwanini watu waje  kutembelea blog yako,  ila kikubwa sana ni wewe kuweza kuwapatia habari au taarifa wanazozihitaji. Kuiendesha blog yako kuna maanisha kuandika makala  bora, kuwapatia taarifa watu kuwa blogu yako ipo hewani, na kuendelea kuwakumbusha kuwa ipo hewani.
Wewe mwenyewe kwa muda wako unaweza kujifunza mambo mengi ya msingi katika kuendesha blog toka jinsi ya kupata wasomajii wengi, kuandika makala nzuri, kuongeza urembo katika blog, kubadili template n.k. Baadhi ya sehemu unazoweza kupata kujifunza zaidi ni kama zifuatavyo:-
 http://www.problogger.net/
http://allbloggingtips.com/
http://www.spiceupyourblog.com/
http://www.bloggerplugins.org/
Wasiliana nami kwa WhatsApp +57 301 297 1724 upate mafunzo na maelekezo wewe kama wewe na kusaidiwa kuibuni na kuiboresha blog yako. Au niandikie email: john.myungire@gmail.com


Mikakati:  Ili uweze kuwa na blogu endelevu inabidi uwe na mikakati ya kimasoko kwa blogu yako, mikakati ya muundo wa habari zako, na mikakati ya usimamizi wa blogu yako ikiwa pamoja na jinsi unavyoweza kuboresha ubora wa muonekano wa blog na makala zako.
Mojawapo ya mikakati yako ya masoko inaweza kuwa ni kufungua ukurasa maalum wa Facebook. Hata hivyo kufungua ukurasa huko kuwa kwa mkakati maana kuna kazi kupata watu wa ku like ukurasa huo, na zaidi sana kuuendeleza ukurusa husika pamoja na blogu yako.

Mapato:  Mapato yanayotokana na blog yanaweza kuwa ni kutokana na matangazo, kuuza bidhaa kupitia blog yako, au hata kuamua kuja kuiuza blog yako maarufu kwa watu wengine, kama vile watu wanavyouza makampuni yao. Kwa upande wa matangazo, mapato yanaweza kuwa ya aina mbili – mapato ya moja kwa moja toka kwa asasi husika zinazotaka kutangaza kutoka blog yako, au matangazo kupitia Google – yanaitwa Google Adsense. Matangazo haya ya GoogleAdsense ni kuwa kama blog yako inakidhi viwango ambavyo Google wameweka, basi ukiwa umejiandikisha kwa ajili ya blog yako kupokea matangazo hayo,  utaweza kuona matangazo mbalimbali toka Google yakionekana kwa blog yako, na utalipwa kuendana na jinsi watu wanavyobofya na kununua bidhaa husika zinazotangazwa na Google.
Kuhusu mapato kutoka na kuuza bidhaa kupitia blogu yako ni kwamba wewe mwenyewe unaweza kuwa na bidhaa mfano unatoa huduma ya ushauri kwa wajasiriamali, basi ndio nafasi yako ya kuwapata wajasirimali kupitia blog yako. Au unaweza kujiandikisha na mfumo wa kuuza bidhaa wa watu wengine, na wewe ukalipwa posho (commission) kama watu watanunua bidhaa husika. Mfumo huo unaitwa Affiliate selling. Angalia orodha ya website zenye huduma ya Affiliate marketing/sales Hapa
Hivyo ingawa watu wengi hufikiria kuanzisha blogs ili wapate kuuza nafasi za matangazo, unatakiwa kujua kuna nafasi nyingi za kuingiza fedha zaidi ya matangazo.  Kinachotakiwa ni kujipanga, na kuwa na mkakati wa dhati wa ina gani ya mapato unayotaka kupata, na jinsi ya kuiendesha blog yako kwa kadri ya mapato unayolenga.
Kuna somo maalum kabisa tumeliandaa hapa Mbuke Times , waweza kulipata wakati wowote, kuhusu namna gani ya kuanzisha blog yenye faida kwa biashara. Angalia link hii: BLOG YA BIASHARA

Gharama: Kuna gharama nyingi za kuendesha blog, kama vile unaweza amua kuwa anuani tofauti na hizo za bure, hivyo mfano www.millardayo.com ni blog lakini ina anuani binafsi ambayo inalipiwa kila mwaka.
Wapo ambao watahitaji kuwa na muonekano bora wa blog zao, hivyo kuajiri mtu wa kuboresha muonekano au hata kuwa na muonekano mpya kabisa. Mfano Mbuke Times ni blog, ila hauwezi pata template kama hii kutoka templates zinazotolewa na blogger.
Na hata kama ukipata templates za bure, kama hii ya Mbuke Times, unatakiwa uwe na uwezo wa kubadilisha baadhi ya mambo kama vile background, au maandishi na kurasa nyingine zisizoendana na malengo ya blog yako. Kama hauwezi kufanya hivyo wewe mwenyewe itakubidi kuingia gharama ya mtu akufanyie. Ila usihofu gharama ya kuboresha blog yako. Wasiliana nami kwa email john.myungire@gmail.com au WhatsApp +57 301 297 1724 nitakuboreshea kwa gharama kidogo sana.
Gharama nyingine za uendeshaji wa blog ni manunuzi ya vifaa kama vile kamera, kompyuta, gharama za internet,  usafiri wa kuenda maeneo mbalimbali ili upate habari/taarifa. Pia zipo gharama za matangazo, zaidi sana muda mwingi utakaoutumia kutafuta taarifa,  kuandika makala, na kuitangaza blogu yako.
Share:

MAFUNZO MAALUM: JINSI YA KUFANYA WAZO LIWE BIDHAA INAYOLIPA

Je una wazo la biashara ila haujui unaanzaje kulifanya liwe kweli ni bidhaa ? Je umekua ukibuni bidhaa Fulani Fulani ila haupati “bahati” ya kufikia wateja wengi na kufaidika na bidhaa yako ? Basi jibu lipo katika uwezo sahihi wa kuunda bidhaa kwa kitaalamu tunaita Product Development.

Ni kweli kuwa fursa zipo nyingi sana na kinachotakiwa ni umakini wa kuziona. Ili uzione fursa wakati mwingine inakupasa uwe tayari una taarifa nyingi nyingi kuhusiana na uwezekano wa kufanya jambo fulani, kwani kwa hayo mambo ambayo unayajua ndio utaweza tambua kitu kinachowezekana kufanyika wakati watu wengine wanaona haiwezekani, wakati wengine wanaona ni matatizo , wewe unajiumia kichwa kujua suluhu yake itakuaje.

Kuna namna nyingi ambapo "ideas" huja, na sio kila idea inaweza kukuingizia fedha. Ukishapata idea itakupasa ujue namna ya kuichambua, namna ya kutengeneza thamani kweli kweli ili walengwa wainunue, na namna ya kupangilia vile utakavyoiwasilsha bidhaa au huduma yako uliyoweza itengeneza kupitia "idea" yako.
Mchakato woote huu kitaalamu tunauita PRODUCT DEVELOPMENT. Na ijumaa hii March 3, 2017 kupitia WhatsApp group na FB groups maalum, nitaelezea mbinu mbalimbali tunazotumia ktk kubuni na kuunda bidhaa toka kwenye idea mpaka kitu kinachoeleweka na kuuzika.
Haijalishi ni idea ya kuwa na app, idea ya kuuza bidhaa fulani, au kutengeneza bidhaa fulani, yote tuyajadili kwa umakini. Utajifunza namna ya kutafiti soko, namna ya kuunda VALUE kwa bidhaa yako, na mbinu za kujaribu haraka haraka bidhaa yako. Pia utapata ufafanuzi kuhusu namna ya kuwafikia wateja ili waweze nunua bidhaa zako.


Wasiliana nami kwa WhatsApp +57 301 297 1724 au +255 757 120 020 tukupe utaratibu wa kujiunga ktk somo hili la siku moja tuu. 
Share:

JIFUNZE ENGLISH: JINSI YA KUTOA MAELEKEZO AU AMRI KATIKA ENGLISH

Katika mawasiliano ya English ni muhimu kujua kuongea kwa namna sahihi hivyo basi ndio maana katika somo hili utaangalia namna ya kuandika na kuongea sentensi ambazo ni za kutoa maelekezo au tuseme kuamrisha. Sentensi hizi kwa English huitwa imperatives au command.

Jinsi ya kuunda sentensi ya kuamrisha/kutoa maelekezo katika English
Sentensi zote za kuamrisha katika English zinafuata kanuni kuu mbili :
Kwanza huwa na verbs zenye infinitive,
Yaani matendo yanayotajwa huandikwa au kusemwa bila kuyabadilisha vyovyote vile mfano tunajua kula ni EAT , basi utataja hivyo hivyo EAT bila kuanza kufikiria kwa namna gani ubadilishe nyakati ya hiyo verb husika.
Mfano mwingine tukio la kulala ni  SLEEP basi utatumia hilo hilo neno sleep bila kujiuliza ni kwa namna gani utabadili.
Pili daima kumbuka sentensi huwa zinaelekwa kwa nafsi ya pili
Yaani kwakua ni amri basi anayepokea  hiyo amri ni WEWE au NINYI kwa English tunasema YOU.
Hivyo basi ndio maana tunasema:
Sit down !  - Kaa chini  ( Yaani wewe au ninyi kaeni chini).
Go ! - Nenda ( Yaani wewe nenda au ninyi neneni)
Get out ! ( Yaani wewe toka au ninyi tokeni)

Kwanini uzingatie kuelewa jinsi kuamrisha na kutoa maelekezo kulivyo katika English
Ni kwa sababu wakati mwingine kama utatumia sentensi za namna hii bila kukusudia kutoa amri au maelekezo utajikuta ukieleweka vibaya. Hivyo kwa mfano kama unataka kuomba kitu au kupatiwa ufafanuzi fulani usiandike sentensi yako kiasi kwamba ikaonekana ni kama vile ni amri.
Na wajua wazi kama unataka kuomba kitu halafu ikaonekana kwa sababu ya ongea yako kuwa ni kama una amrisha, haitojenga picha nzuri na hivyo hutopewa unachotaka.

Namna ya kutoa amri au maelekezo ila usionekane unafanya kwa ukali
Ili usionekane mkali katika kitu unachotaka mtu afanye tumie neno please, can, could au would.
Mfano:
Please don’t come here badala ya  Don’t come here !
Would you sit down  ? Badala ya Sit down !
Can you come here ? Badala ya Come here !
Pia waweza tumia sentensi fupi kabla ya kutoa maelekezo. Sentensi zenyewe ni kama vile:
Would you mind….,  Would you please….,  I was wondering if  you can …..,
Mfano: Would you mind  to sit down ?  I was wondering if you can go .

Hitimisho:
Ni muhimu sana kujua kanuni na jinsi ya kuongea vizuri English. Tatizo la kutokufuata kanuni na miongozo ya English ni kuwa utajikuta unachoelezea kikaeleweka tofauti.
Kwa maelekezo zaidi ya English ingia kwa group letu la WhatsApp la JifunzeEnglish, kwa kutuma maombi yako kwa namba +57 301 2971724 au +255 757 120 020. Jitambulishe na useme unahitaji kusaidiwa nini.
Share:

JIFUNZE ENGLISH: MAMBO 5 YA KUFANYA ILI UJIAMINI KATIKA ENGLISH



Safari ya kujfunza English ni ndefu na kwa bahati mbaya watu wengi hupita katika safari hii kwa mateso makubwa kwakua hawajiamini katika kuongea na kuandika English. Makala hii ni sehemu ya jibu nilimpatia mwanafunzi wangu Abdi Mkizu, ambaye alitaka kwanini kwa zaidi ya miaka kumi sasa amekua akijifunza English hata hivyo bado anashindwa kuongea kwa kujiamini wakati baadhi ya marafiki zake wanaweza kuongea vizuri. Anauliza, je ni kwa sababu amekosa kujiamini katika English, na je afanyeje ili apate kujiamini.

Jichukulie wewe ni mwanafunzi wa daima
Kupoteza kujiamini kunawezekana kuwepo kwakua tayari haujichukulii kama mwanafunzi. Unadhani kuwa umeshajifunza vyote vya kujifunza hivyo sasa ni wakati wa kuongea English kwa ufasaha. Ila ukweli ni kuwa sote ni wanafunzi wa lugha wa maisha kwani hata Kiswahili chetu tuu hubadilika badilika mara kwa mara na pia hatukijui vizuri.
Ukijihesabia wewe kama mwanafunzi wa English wa milele, hautoogopa kukosea, maana kukosa kujiamini huja kwa sababu ya hofu ya kuogopa kukosea.
Kama kuna watu fulani wanakukera au kukukatisha tamaa katika kujaribu kwako English, hao watu waepuke kwa kuanzia. Fanya mazungumzo ya English na watu waelewa au na watu ambao kweli unaweza jifunza kutoka kwao, na wanaweza kukurekebisha. Weka mazingira katika kuwasiliana kwa English yanayoonyesha kuwa kweli upo katika kujifunza na upo tayari kukosolewa na kusaidiwa.

Shinda hali ya kujisikia iliyo ndani yako
Wakati mwingine mtu unaweza kushindwa English ni kwa sababu unajisikia kuwa wewe ni bora sana, au ni wa hadhi fulani, iwe kielimu, kimadaraka, kifedha au kiumri  uwa huwezi kuonekana unakosea mbele ya wengine. Unataka utengeneze picha kuwa wewe unajua English, kwakua unajiamini kuwa watu wanakutegemea wewe kuwa na kiwango fulani cha English.
Kumbuka lugha yeyote haina kazi zaidi ya kufanya watu wawasiliane.  Sasa kama wewe utaendelea kujisikia kuwa kwa umri wako, elimu yako au nyadhifa yako kuwa eti huwezi kuonekana unakosea, jiulize je kwako English itakua na kazi gani zaidi ? Chukulia kujua English ni kama kujua kupika. Kuna maana gani ujue kupika kama haupiki chakula chochote ? Hata kama hakitotoka chakula kizuri kama unavyodhani watu wanategemea, la msingi jua wewe upo katika safari ya kuweza kupika msosi mzuri zaidi siku moja. Usikubali kuishi kwa kuogopa maneno ya watu au kutaka kuwapendeza watu.

Kumbuka haushindani na mtu yeyote:
Wakati mwingine kule kutokuajimini kunakuja kwasababu unadhani kiwango chako cha English inabidi kiwe kama cha fulani, au kwanini fulani anajua zaidi English kuliko wewe. Binadamu tupo tofauti, hivyo tuna uwezo tofauti katika kujifunza lugha. Jiambie tuu kuwa la msingi katika kujifunza lugha ni kuweza kuwasiliana. Kama unaweza kuelewa na wewe kueleza vitu vikaeleweka basi upo katika nafasi nzuri katika English. Na kwamba taratibu hatua kwa hatua ukiendelea kuitumia English utakuja kuweza vizuri.
Usijilanganishe na jinsi mwingine anavyotamka kwa ubora zaidi kuliko wewe, au mwingine anavyoandika status bomba kuliko wewe. English unayotaka kuijua ni kwa matumizi yako wewe na sio kama anavyohitaji mtu mwingine. Pia hujui mazingira aliyojifunza huyo mwingine, inawezekana alijifunza kwa urahisi zaidi yako au amepata fursa nyingi zaidi za kuitumia English kuliko wewe. Ni wakati wako sasa na wewe kuitumia kila fursa uipatayo kuzungumza au kuandika kwa English.

Haitoshi kujiona unajua endelea kujifunza English:
Kutokujiamini huja kama tayari umeshajihakikishia kisaikolojia kuwa kwa muda uliotumia kujifunza English, kwa “materials” uliyo nayo, ni lazima tuu uwe unajua au umefikia kiwango fulani cha English. Hivyo basi inapotokea ukashindwa kutamka sentensi fulani, au kuelewa mazungumzo fulani, wewe mwenyewe utajiangalia kwa mtazamo mbovu, kuwa kumbe wewe ni bure kabisa, au kujiambia maneno kama vile basi kumbe hautoweza English.
Hata hivyo nakusihi uamini kuwa lugha haina mwisho katika kujifunza. Inawezekana kabisa ni kweli ulijifunza kwa umakini hivyo ambavyo ulijifunza, hata hivyo kuna vitu vingine muhimu na mbinu kadhaa bado haukujifunza.  Hivyo unapokosea au kushindwa kutunga sentensi au kuelewa sentensi fulani, badala ya kupoteza imani, unatakiwa hapo ndipo upate hamasa ya wapi haswa unaweza kurekebisha.

Tambua madhaifu yako katika English yapo wapi:

Jiulize katika kutojiamini kwako kuandika na kuongea English ni mambo gani haswa unadhani huyafahamu vizuri au utayakosea endapo utaongea au kuandika. Kuwa mkweli kwako wewe mwenyewe kwani inawezekana huko kujiona haujiamini ni kiashirio kuwa kuna mambo kadhaa inabidi ujifunze, ila wewe badala ya kutilia mkazo hayo mambo unayotakiwa kujifunza ili ujiboreshe, wewe unakataa bila kujua kwakua kukiri kuwa kuna mambo ambayo kweli bado inabidi ujifunze ni kujirudisha nyuma katika fikra zako za kwamba wewe tayari unajua English. Bila kujijua unapenda “idea” kuwa wewe upo fiti katika English, wakati ukweli ni kuwa bado kuna mambo mengi inabidi ujifunze.


Hitimisho

Mara baada ya kujifunza hayo yote niliyoeleza hapo juu ya namna ya kujiamini katika kuongea na kuandika English , unatakiwa mara moja uanze kuyafanyia kazi. Tafuta nafasi ambapo unaweza kweli ukatumia hiyo lugha. Ndio maana nilitengeneza group  la WhatsApp la JifunzeEnglish ili kwamba wewe na wengine wote wenye kutaka kufanya mazoezi ya kuongea na kuandika English muweze kupata hiyo nafasi ya kutumia English , pia kujifunza kutokana na makosa ya wengine.  Ni matumaini yangu kuwa katika group hili utajisikia huru kuongea na kukosea, lakini zaidi sana utajifunza kuwa haupo peke yako katika kukosea kwani mimi kama mwalimu, nipo kurekebisha wote wanaokosea.

Kama haujajiunga na group letu la WhatsApp la kujifunza English, nitumie maombi yako ya kujiunga kwa namba +57 301 297 1724. Na kama unataka darasa lako binafsi la English pia wasiliana nami, uanze kuweza kweli kujifunza English.

Share:

NAMNA YA KISASA NA BORA YA KUTAFUTA WATEJA WA BIASHARA YAKO

namna_ya_kupata_wateja_wengi
Katika ushindani wa kibiashara uliopo na mabadiliko ya kiuchumi na kiteknolojia, kupata wateja kumekuwa kugumu sana. Hivyo ili ufanikiwe kweli katika biashara inabidi sio tuu uwe na bidhaa nzuri lakini pia ujue namna bora ya kutafuta wateja.
Hata kama una duka la nguo tuu dogo au saluni waweza kuwa umeathirika na namna ambavyo ushindani wa biashara ulivyo. Hivyo katika makala hii utajifunza mbinu ya kisasa kabisa ya kupata wateja wa biashara yako.

Kabla ya kujifunza  mbinu ya jinsi ya kupata wateja unahitaji kujua kwanza kwanini ni ngumu kupata wateja.

Hali ngumu ya kiuchumi : Kuna namna mbili ambapo hali ya kiuchumi inaweza athiri kupatikana kwa wateja. Kwanza kuwafanya wasiwe na uwezo wa kulipia bidhaa yako , na pili kuwafanya wajifikirie sana kuhusu kununua bidhaa zako. Katika yote haya hali ngumu ya kiuchumi inajenga ukinzani wa wewe kujenga ushawishi kwa wateja wako kununua bidhaazako.

Mabadiliko ya teknolojia: Teknolojia inafanya watu wengi zaidi waweze kuwafikia wateja wako ambapo hapo kabla haikua rahisi. Enzi hizo ilikua utengeneze vipeperushi au uwe na hela za kutosha kutangaza redio, kwa tv na kwenye mabango. Ila sasa watu kupitia Facebook, WhatsApp, na Instagram wanaweza kuwafikia watu wengi kwa urahisi. Hata yule mtengeneza keki mtaani kwenu nae yupo Instagram akitangaza keki na mikate yake. Bwana Mangi nae yupo kwa Facebook akitafuta wateja wa kibanda chake cha kuuza vocha za simu na MPESA.

Njia ya kisasa ya kisasa ya kuwapata wateja:
Tumefika wakati ambapo wateja wengi wana taarifa nyingi kuhusu wapi na kwa bei gani bidhaa zinapatikana. Hivyo wewe kuwa tuu na bidhaa fulani au kwa bei fulani hakutoshi kuwa njia ya kuwafikia.
Pia kwakua kuna watangazaji wengi wa bidhaa inakupasa wewe kuwa na namna ya kipekee ya kuwafikia wateja wako bila kuwa kero kwa wateja kama walivyo watu wengine wengi ambao ni wazi kabisa kwa “makelele” yao ya matangazo wanaonekana wazi wanachotaka wao ni kuuza tuu hizo bidhaa waishie zao. Ni ukweli wa kitaalamu katika marketing kuwa watu wengi  hawapendi kujisikia kuwa fulani anawauzia bidhaa. Hata hivyo hivyo haimaanishi kuwa watu hawapendi kununua. Watu hupenda kununua ila hawapendi ile hali ya kuwekwa “kati” na mtu anayejaribu kuwauzia kitu.

Ukichanganya na ukweli huo kuwa watu hawapendi kujisikia wakiuziwa bidhaa, halafu hali ngumu ya uchumi na mabadiliko ya teknolojia yanafanya kuwepo na “makelele” ya wafanyabiashara wengi,  basi wewe unahitaji mbinu ya ziada.
Hivyo basi mbinu ya kisasa ninayozungumzia hapa ni kutengeneza ushirika na wateja kama jamii ambayo itakuamini na kukuona una kitu zaidi ya kutaka tuu kuwauzia bidhaa zako. Kwa mbinu hii unajenga uhusiano na kufikia hisia za wateja wako, unatambua matatizo yao , unakua kweli mshirika wao katika yale ambayo unaona wao wanaweza kunufaika kupitia bidhaa zako hapo baadae.
Kwa mfano kama wewe ni muuza nguo, badala ya kila wakati kuwatangazia tuu mzigo mpya ulio nao, tambua kwanini hawa watu wanunue nguo mpya. Zungumza nao kuhusu hayo mambo. Mfano iwe ni swala la kujisitiri, au unadhani wananunua sana kwa ajili ya kujionyesha kuwa wanaenda na wakati na ni watu wa mitindo, basi waonyeshe unalielewa hilo kwa kutumia mitandao ya kijamii ukipost vitu vinavyoendana na hayo mambo ya mitindo na kuenda na wakati.

Jiweke katika nafasi zao, na uwahudumie vema kihisia kwanza , ukishawaonyesha kuwa wewe unaweza na unajua nini wanataka , hapo ni rahisi kuwaambia kuhusu bidhaa zako ambazo zitawafikisha katika malengo hayo wanayodhamiria.
Kwa mbinu hii unaondoa upinzani wa wateja kutaka kukusikiliza , na unafanya rahisi kwa wao kufanya maamuzi ya kununua bidhaa zako kwakua hawaoni kama unawauzia bidhaa, bali wanaona ni muendelezo wa ukaribu wako na utayari wako wa kuwaona wakijisikia vizuri na kufikia malengo yao.
Katika kutengeneza huo ukaribu wako na wao kupitia machapisho, videos, na picha mbalimbali wenyewe wateja wajisikia utayari wa kukutafuta.
Tunahitaji kiitalamu hii njia ya kupata wateja wengi
Hii njia niliyoieleza ni muhtasari tuu wa aina ya marketing inayoitwa kwa kitaalamu inbound marketing.
Inbound marketing ni pana, ina mambo mengi na inaanza hata kwenye website ya biashara yako.


Kama unataka kuanza kufanyia kazi mbinu hii na unahitaji muongozo zaidi usisite kunifuta kwa namba WhatsApp +57 301 297 1724. Au kwa email john.myungire@gmail.com

Share:

JIFUNZE ENGLISH: JINSI YA KUSOMA SAA NA TAREHE KWA ENGLISH

kusoma_saa_English
Kusoma saa na kusoma tarehe kwa English ni muhimu sana kama sehemu ya wewe kujua English kwa ufasaha. Katika Makala hii tutajifunza vema namna tofauti za kusoma saa na kusoma tarehe kwa kiingereza.

Kusoma tarehe katika English:
Kwenye English tarehe huandikwa kwa kuanza na SIKU halafu MWEZI halafu mwaka. Mfano  16th  Feb. 2017, na utaisoma hivi : SIXTEENTH of February  Two Thousand and Seventeen.                        

Kumbuka: Kuna mbili za kusoma mwaka yaani

Kusoma namba nzima nzima  mfano: 2017 waweza sema namba kamili yaani elfu mbili na kumi na saba hivyo ukasema Two thousand and seventeen.
Njia ya pili ya kusoma mwaka ni kwa kusoma kwa mafungu ya namba mbili mbili yaani 20 halafu 17 hivyo ikawa TWENTY SEVENTEEN.

Kumbuka kwenye kutaja siku huwa tunasoma kwa viashiria hivi kutegemeana na namba ya mwisho ya tarehe:
1 – th yaani first mfano 1st Jan.2017 first of January twenty seventeen. Au 21st Jan 2016 ikasomwa Twenty first of January  twenty sixteen.

11 – th mfano 11th Feb . 2015 Eleventh of February twenty fifteen.
2 – nd mfano 2nd March 2016 Second of March twenty sixteen.
12- th mfano 12th April 2015 Twelfth of April twenty fifteen
3-rd mfano 3rd May 1998  Third of May nineteen nighty eight.
23 – 23rd  mfano 23rd June 2010 Twenty third of June twenty ten
Pia tambua kuwa kuandika tarehe inategemea na aina ya English, kama ni British English hiyo ambayo mnaitumia huko Tanzania ni kuwa unaanza na siku halafu mwezi halafu mwaka yaani 16th Feb. 2017 ila kama ni American English tarehe huandikwa kwa kuanza na mwezi kisha siku halafu mwaka yaani kwa mfano Feb . 16,2017 
                      
Jinsi ya kusoma saa kwa English                                                                       
Kuna namna mbili za kusoma saa katika English

Aina ya kwanza ya kusoma saa kwa English
Katika aina hii huwa tunaanza kutaja dakika kisha saa.  Na kumbuka katika English saa hutajwa kama mshale unavyoonyesha. Hivyo kwa mfano saa mbili asubuhi mshale utakua kwenye namba NANE, nawe utasema EIGHT usiseme kama kwa Kiswahili tunavyosema MBILI halafu ukasema TWO.
Mfano mweingine 7:25AM kwa Kiswahili ni saa moja kumi asubuhi ila kwa English kumbuka tunasoma saa kama zilivyoandikwa hivyo badala ya MOJA tutasema SEVEN. 
Kusoma dakika pia katika English kunategemea na je dakika zipo kabla ya 30 au baada ya 30 kama unavyoweza kuona katika picha hapa chini.
dakika_minutes_in_English

Hivyo kwa saa 7:25AM jiulize je dakika zipo kati ya dk 1 hadi 30 ? Kama ndio basi tumia PAST ukitaja dakika. Yaani mfano Twenty Five Minutes Past SEVEN.                                               

Tukumbuke AM maana yake ni kuanzia saa sita kamili usiku hadi saa tano na dk 59 asubuhi. Baada ya hapo ni PM    
                   
Aina ya Pili ya kusoma saa kwa English
Namna nyingine ya kusoma saa kwa English ni kwa kutaja namba kwa makundi mawili. Yaani kwanza kundi la saa kisha kundi la dakika. Mfano: 11:20 AM utasema Eleven Twenty in the morning                       Mfano mweinine 1:20PM utasema One twenty in the afternoon.                        


Hauna haja ya kusema ni afternoon au evening au night kama unaongea na mtu moja kwa  moja kwakua huyo mtu atakua akijua unataja saa gani kama unachotaka kusema wakati huo ni saa ngapi.
Angalia mfano hapa chini wa kusoma saa mbalimbali

Jifunze Zaidi:
Jiunge na group letu la WhatsApp kwa kutuma maombi ya kujiunga kwa namba hii +57 301 297 1724. Na pia karibu ujipatie kitabu chenye kanuni za msingi za kujua English. Kitabu kinaitwa English: Mbinu na Kanuni za Kuijua. Kitabu kinapatikana popote ulipo pale maana utatumiwa kwa email au kwa WhatsApp au kwa Facebook. Kitabu ni Tshs. Elfu Kumi na Tano.
kitabu_cha_English


Share:

MAFUNZO MAALUM YA VILE BLOG INAVYOWEZA KUKUWEKA VEMA KATIKA USHINDANI WA KIBIASHARA

blog_ya_biashara

Kati ya vitu ambavyo utajutia hukufanya kwa ajili ya biashara yako katika ulimwengu huu wa kidigitali ni kuwekeza katika INBOUND MARKETING. Inbound Marketing ni namna ambavyo unakua na contents za kutosha na kuvutia mtandaoni kiasi kwamba walengwa wa biashara yako wanatambua wewe ni nani na kwa namna gani unafaa kuwahudumia.

Na njia bora ya kutengeneza na kusambaza contents zako ni kutumia blog ya biashara yako.
Blogs hizi za biashara ni tofauti na blogs za habari kama vile za kina Michuzi, blogs za biashara hujikita katika kuelezea mambo matatizo unayojaribu kutatua kupitia bidhaa zako na pia kuonyesha ukaribu wako na jamii kwa kuwapa contents ambazo kweli wanazihitaji.
Biashara nyingi zenye websites huwa na ukurusa wa BLOG hata hivyo biashara nyingi bado hazijaanza kutumia vema blog kama chombo cha marketing na kuongeza mauzo.


-- Wasiliana nasi tukupe mafunzo haya peke yako ili uweze kweli kuwa na blog yenye kulipa. Utapata mafunzo  maalum ya hatua kwa hatua ya namna ya kuwa na blog kwa ajili ya biashara yako. Utajifunza kuhusu teknolojia ya blog, namna ya kuandika makala zenye mashiko na zenye kukuletea wateja, na hatua kwa hatua ya jinsi ya kusambaza makala zako na kupata wasomaji wengi.
Wasiliana nami hapa FB au kwa WhatsApp +57 301 297 1724.


Photo credit: socialmarketingfella.com
Share:

JINSI YA KUSHINDA USHINDANI MKUBWA WA KIBIASHARA ULIOPO SASA

mabadiliko_ushindani_kibiashara
Hivi karibuni mwekezaji mkubwa duniani Warren Buffet ameuza hisa zake nyingi za kampuni ya Walmart kwakua anasema Walmart haielekei pazuri kibiashara kwani biashara kubwa ya rejareja inaelekea kufanyika kupitia mtandao na sio supermarkets kubwa kubwa  kama za Wallmart.  Wallmart imepoteza mauzo kwa kiwango kikubwa wakati wauzaji wa rejareja wa mtandaoni waitwao Amazon ndio wameshika kasi sasa. Tulisikia pia jinsi NOKIA ilivyopoteza biashara ya simu za mkononi .
Tuangalie katika makala hii namna gani unaweza kujidhatiti ili biashara yako isipitwe na kupotezwa na ushindani.

Mabadiliko ya ushindani yanavyoathiri biashara yako
Kampuni au wajasiriamali wengi hupoteza biashara wakati mwingine sio kwasababu kuna kitu fulani wanakosea, ila ni kwa sababu hawakuendana na kasi ya mabadiliko katika soko. Mabadiliko hayo yanaweza kuwa ya kiutendaji, kiubunifu au kiteknolojia.

Katika kufanya ujasiriamali haitoshi tuu kuwa mzuri katika hicho unachofanya, yaani kuwa na bidhaa nzuri na bei poa. Haitoshi tuu kuwa na soko kubwa leo na watu wanaokuzunguka na kukubali leo. Kwakua biashara yako sio tuu kwa ajili ya leo, unahitaji kuwa na mkakati wa namna gani utapita katika nyakati tofauti tofauti za kijamii, na kimaendeleo. Unahitaji kuwa mwepesi wa kubadilika.

Mabadiliko gani mfanyabiashara anahitaji ili asipotezwe na ushindani
Mfanya  biashara  hautoweza kubadilika kama haujiwekei mpango wa kujifunza ili uweze kweli kujua unabadilika kivipi na wakati gani haswa ni muafaka kubadilika.

Inakupasa ujijengee utamaduni wa kutaka kujua zaidi nini kinaendelea katika ulimwengu wa biashara, je mbinu gani zinafaa kwa sasa za kimatangazo , uendeshaji wa biashara n.k

Kwa mfano, biashara kibao sasa zimeingia kutumia kwelikweli blogs ana mitandao ya kijamii kama sehemu za kujitangaza  na kuuza bidhaa zao. Hata hivyo hata mitandao hiyo nayo inahitaji ubunifu na mikakati ya kutosha ili kweli ikuletee faida na usipitwe na wakati.

Tatizo la mabadiliko ni kuwa hukuathiri kidogo kidogo , na usipokua makini unaweza kudhani kila kitu kipo sawa, hadi uje ushtuke kuwa mabadiliko hayo yamekuathiri , tayari athari zake zimeshakua kubwa na pengine hutoweza tena kujiboresha ili uweze kushinda katika ushindani.

Ufanye nini sasa ili kutokupitwa na mabadiliko ya ushindani ?

  • Weka mkakati wa kujiendeleza  ili ujue mabadiliko yanaendelea katika ulimwengu wa biashara yako.
  • Tilia maanani sio tuu namna gani unavyojiboresha na biashara yako bali pia mabadiliko yanayofanywa na wengine wanaofanya biashara kama  yako au biashara zinazofanana na biashara yako.
  • Fikiria biashara yako kwa mapana zaidi kwani mambo yanayotokea katika ulimwengu mkubwa zaidi ya hapo ulipo sasa yanaweza pia kuathiri biashara yako, hivyo wewe ukiiangalia biashara yako kwa mapana, unaweza jiandaa kukabiliana na magumu hayo.
  • Wekeza katika mbinu za kisasa za marketing na mauzo , kwa mfano je unatumia inbound marketing ?
Pata msaada usipitwe na mabadiliko
Wasiliana nami kwa WhatsApp +57 301 297 1724 [Namba ya nchini Colombia ] ili nikupatie ushauri binafsi utakaoendana na aina ya ujasiriamali unaofanya au unaotaka kufanya. Njoo tubuni mikakati ya marketing na jinsi utakavyopanua soko lako. Au nicheki kwa email john.myungire@gmail.com

Share:

FURSA: JINSI YA KUINGIZA FEDHA KUPITIA GOOGLE ADSENSE

Google AdSense ni matangazo yanayowekwa katika website. Matangazo hayo ni kwamba watu wanaotaka kutangaza bidhaa zao hufanya kushindania kupata nafasi ya kutangaziwa matangazo yao. Watu wanapozungumzia kutaka kutengeneza hela kupitia mtandao hutaja Google AdSense. Ngoja nikudokeze kidogo kuhusu AdSense. Ni kweli hulipa. Hata hivyo kuna mambo machache ya kufahamu: Mchakato wa kujiunga na Google AdSense Kuna mchakato unaohitaji umakini kweli kweli ili uweze kusajiliwa kwa hiyo huduma ya AdSense. Sio kila website , blog au YouTube account inaweza tuu kusajiliwa. Moja ya mambo ya kuzingatia ni kuwa uwe na contents za kutosha, na wakati mwingine husisitiza lugha sahihi itumike kwa blog au website yako ili kweli Google waweze kuipitisha blog yako. Jinsi hela zinavyoingia kupitia Google AdSense Unahitaji views nyingi kwa blog au website yako ili uweze kuingiza fedha kupitia Google AdSense. Hata hivyo kuwa tuu na Views nyingi kwa website au blog yako haimaanishi basi eti mapato yatakua makubwa. Hii ni kwa sababu matangazo yanaoyoonyeshwa hutegemea ni kiasi gani watu wameahidi kulipia kwa kila click ya tangazo husika. Hivyo kuna mambo mawili makubwa yanayosababisha mapato yawe makubwa au madogo. Kwanza bei ambayo watangazaji wamesema wapo tayari kulipia kwa kila CLICK ya tangazo husika, na pili idadi ya clicks kwa kila tangazo. Kwenye idadi ya clicks hapo ndipo panapoleta ile hali kuwa unaweza kuwa na hata VIEWS ELFU 10 kwa siku lakini ukapata mapato kidogo kuliko mwenye VIEWS EFLU 5 kwa siku. Inawezekana mwenzako mwenye views chache ana matangazo yenye dau kubwa halafu watembeleaji wake kweli wanakua interested na hayo matangazo yanayoonyeshwa katika website au blog husika. Maandalizi ya msingi ili uanze kuingiza fedha kupitia Google AdSense: Katika yote yote, unahitaji design nzuri ya blog, unahitaji kutambua vema walengwa husika ambao kweli kupitia hao matangazo yatakua yenye kulipa, na pia unahitaji uwe na makala zitakazoweza kweli kuvuta watu wengi zaidi waje kwa blog au site yako. Kwani kadri watu wanavyotembelea ndivyo unaongeza nafasi ya wewe kupata watu watakao click matangazo husika na hapo ndipo utakapoingiza fedha. Mapato mengine zaidi ya Google AdSense Kama unaona AdSense ni ngumu, kuna njia nyingine nyingi tuu za kuingiza hela kupitia blog au website yako. -- Njoo tuzungumzie upate maujanja zaidi na maelekezo yanayokuhusu wewe kama wewe maana kila blog au site ni tofauti na nyingine hivyo mikakati ya kuingiza fedha inaweza kuwa tofauti. Nicheki kwa WhatsApp +57 301 297 1724. Usikose siku ya Alhamis Feb 16 saa mbili usiku nitakua nikifundisha kupitia WhatsApp na FB groups maalum jinsi ya kuwa na blog kwa ajili ya kampuni, NGO na biashara mbalimbali. Wasiliana nami ujiandikishe uje ujifunze namna ya kuingiza mapato na kuongeza MAUZO kupitia blogs.
Share:

FAHAMU MTEJA MLENGWA UONGEZE MAUZO YA BIASHARA YAKO

Wakati mwingine unaweza lalamika kuwa biashara ngumu , wateja hawanunui bidhaa yako au kuna ushindani mkubwa wa soko lakini kumbe tatizo lipo kwako wewe mwenyewe kwakua hujamtambua kweli kweli ni NANI HASWA NDIO MTEJA wako. 

Mtazamo usio sahihi kuhusu mteja
Waweza sikia kwa mfano mtu akisema eti haelewi kwanini ana marafiki wengi lakini eti bidhaa zake hazipati wateja. Wingi wa watu pekee haufanyi uwepo wa wateja. Mfano sio kwa sababu unaouza nguo za akina mama basi wanawake wote ni wateja wako.
Sio kwa sababu kwa mfano kwakua kuna shule nyingi mtaani kwenu basi ukleta viatu vya shule utapata tuu kuuza kwakua wanafunzi au wazazi wa wanafunzi hao ndio wateja wako na wapo wengi.
Ukiulizwa biashara yako inalenga wakina nani, unasema kila mtu, na ndio maana kwako haiingii akili kuwa kwanini ushindwe kuuza wakati unamlenga kila mtu. Hata hivyo kama unataka biashara endelevu ni lazima uwe na walengwa maalum.

Maana ya mteja mlengwa:
Tunaposema walengwa maalum tunamaanisha kundi fulani la watu ambao wana sifa za jumla ambazo kwa kutumia sifa hizo utafahamu vema namna gani ya kuwahudumia na kuwapatia kweli kitu wanachohitaji.

Kwahiyo mteja mlengwa ni yule ambaye kweli anaguswa na bidhaa husika unayotaka kuifikisha kwa wateja.
Mteja mlengwa unamfafanua kwa kuangalia aina gani ya bidhaa unaitoa, nani haswa atafaidika nayo, nani.

Faida za kufahamu kwa umakini mteja mlengwa
Kuwa na walengwa maalum kunakuongezea uwezo wa kuwa mbunifu zaidi maana upo kwa aina fulani tuu , hivyo unatumia muda mwingi "ukiwa" na hao walengwa wako, utawafahamu vema mwelekeo wao, tabia zao, shida zao , na wanayopendelea hivyo kujiset ziendano na hao.
--Kuwa na wateja maalum kutakufanya ufahamu namna bora zaidi za kuwasiliana nao kimasoko, vile unavyoweza tengeneza matangazo yako , promotions na mbinu zingine za kimasoko kama vile contents zako ziweje.
--Kuwa na wateja maalum kutakufanya hata ujiset vema katika kupanga bei za bidhaa zako, mfano mzuri iphone mpya mara nyingi bei zao ni juu kuliko aina nyingi za simu kwakua iphone ina aina maalum ya wateja waliokusudiwa.
--Kuwa na wateja maalum na kuwatafiti vizuri kunakupa amani kwa maana utapunguza stress za kujiona unashindana na kila mtu. Ukishakua na wateja maalum, utajikita nao , utajituma nao, utafocus zaidi kwenye mfumo wa biashara yako na bidhaa yako, na sio kwenye kuangalia washindani wako wanafanya nini.
--Kujua wateja vizuri kutakufanya kweli kweli utengeneze upekee wako mbele ya soko.
Usipitwe na ufahamu mambo haya ya ujasiriamali haswa katika zama hizi za kidigitali. Nicheki kwa ushauri binafsi na muongozo wa mambo ya masoko na jinsi unavyoweza itumia teknolojia kuwafikia watu wengi zaidi. +57 301 297 1724
Share:

FURSA ZA BIASHARA: JINSI YA KUZITAMBUA NA KUZITUMIA


Je unatafuta fursa ? Je unafikiri kuwa maisha yako yangeboreka kama ungekuwa na fursa zaidi ? Kama ndio nina habari njema kwako.
Maana ya Fursa za Kibiashara
Kwanza kabisa acha KUTAFUTA FURSA, kwasababu kufanya hivyo ni kurefusha mchakato wa kufaidika na fursa. Fursa hazitafutwi, fursa hazitengenezwi, kwakua fursa daima zipo.
Nasema fursa zipo daima kwakua maana ya fursa ni tatizo ambalo linahitaji suluhu na kupitia suluhu hiyo huyo mtoa suluhu atafaidika kwa kuingiza kipato au kupiga hatua kwa namna nyingine yoyote.
Ninaposema tatizo namaanisha ugumu wowote ule ambao wewe upo katika jamii. Ugumu huo unaweza kuuona wewe kama wewe hivyo suluhu yako ikasambaa kwa watu wengi zaidi ambao wana tatizo kama lako, au ugumu (tatizo) likawa linawagusa watu fulani wewe ukalitatua kwa ajili yao, na ukaingiza kipato.

Mifano ya jinsi ya kutambua fursa za kibiashara
Ngoja nikupe mifano ya mambo makubwa duniani ambayo yamefanyika kwa kuangalia fursa kwa namna hiyo niliyoitaja hapo juu.
Huduma maarufu ya kuhifadhi taarifa mtandaoni iitwayo DROPBOX ilianzishwa kwakua mwanzilishi wake alikua msahaulifu sana wa FLASH DRIVE. Hivyo akatafuta njia ya kuhakikisha files/taarifa zake zinaweza kupatikana popote pale , hata akisahau flashdrive.
Au chukulia mfano wa YouTube iliyoanzishwa kwa sababu waanzishaji walipata shida ya kutafuta video ya Janet Jackson ambaye aliachia matiti wazi wakati wa show ya Super Bowl, hivyo waanzishaji wa YouTube wakajiuliza laiti ingekuwepo huduma ambapo watu popote pale wanaweza kushare kwa urahisi wao wenyewe videos za watu au matukio mbalimbali pengine isingekua shida kwao kuipata hiyo video ya YouTube.
Mfano wa FURSA iliyoonekana baada ya kutazama tatizo la watu wengine ni huduma ya barua pepe ya GMAIL. Huduma hii ilikuja kwakua ilionekana wakati huo huduma za barua pepe hazikua na namna ya kuwasaidia watu kutafuta emails zilizopita , na pia nafasi ndogo ya kuhifadhi emails ililazimu watu kufuta emails zao nyingi tuu.
Ninachojaribu kusema ni kuwa badala ya kuhangaika KUTAFUTA FURSA, au KUWAAMBIA WATU WAKUONYESHE fursa, anza wewe mwenyewe KUZIANGALIA FURSA. Fursa zipo kila wakati , kila mahali. Unachotakiwa tuu ni umakini wako wa KUTAZAMA na KUUNGANISHA UNGANISHA mambo ili uweze kulitambua tatizo haswa ni lipi na uweze kubuni suluhisho sahihi.

Nini ufanye ukishatambua fursa
Kulitambua tatizo na hata kubuni tuu suluhisho peke yake hakuwezi kukunufaisha kama haujajua vema namna ya kuwasilisha suluhu yako kwa walengwa, namna ya kuchambua soko na kupanga uzalishaji na uuzaji wa hicho utakachozalisha au kusambaza.
Sio lazima utengeneze bidhaa mpya, inawezekana hata kuboresha bidhaa zilizopo tuu ni fursa, au kutoa bidhaa toka eneo moja kwenda eneo lingine.
Mfano wa bidhaa iliyozalishwa kwa kuona fursa ya kuboresha bidhaa iliyopo ni kifaa cha kusikiliza muziki cha Apple kiitwa ipod.

Anza sasa kutumia fursa za kibiashara
--Je umeanza kutambua fursa na unataka muongozo wa jinsi gani ya kuhakikisha kweli inakuingizia kipato ? Njoo tuzungumze. Upate ushauri wa kitaalamu kuhusu utengenezaji wa bidhaa (Product Development) na pia namna ya kuwafikia wateja unaowalenga walipie bidhaa husika. Nicheki hapa FB au kwa WhatsApp +57 301 297 1724
Share: