Kusoma saa na kusoma tarehe kwa English ni muhimu sana kama
sehemu ya wewe kujua English kwa ufasaha. Katika Makala hii tutajifunza vema
namna tofauti za kusoma saa na kusoma tarehe kwa kiingereza.
Kusoma tarehe katika
English:
Kwenye English tarehe huandikwa kwa kuanza na SIKU halafu MWEZI halafu mwaka.
Mfano 16th Feb. 2017, na utaisoma hivi : SIXTEENTH of
February Two Thousand and Seventeen.
Kumbuka: Kuna mbili za kusoma mwaka yaani
Kusoma namba nzima nzima mfano: 2017
waweza sema namba kamili yaani elfu mbili na kumi na saba hivyo ukasema Two
thousand and seventeen.
Njia ya pili ya kusoma mwaka ni kwa kusoma kwa mafungu ya namba mbili mbili
yaani 20 halafu 17 hivyo ikawa TWENTY SEVENTEEN.
Kumbuka kwenye kutaja siku huwa tunasoma kwa viashiria hivi
kutegemeana na namba ya mwisho ya tarehe:
1 – th yaani first mfano 1st Jan.2017 first of January twenty
seventeen. Au 21st Jan 2016 ikasomwa Twenty first of January twenty sixteen.
11 – th mfano 11th Feb . 2015 Eleventh of
February twenty fifteen.
2 – nd mfano 2nd March 2016 Second of March
twenty sixteen.
12- th mfano 12th April 2015 Twelfth of April
twenty fifteen
3-rd mfano 3rd May 1998 Third of May nineteen nighty eight.
23 – 23rd mfano 23rd June 2010 Twenty third
of June twenty ten
Pia tambua kuwa kuandika tarehe inategemea na aina ya
English, kama ni British English hiyo ambayo mnaitumia huko Tanzania ni kuwa
unaanza na siku halafu mwezi halafu mwaka yaani 16th Feb. 2017 ila kama ni
American English tarehe huandikwa kwa kuanza na mwezi kisha siku halafu mwaka
yaani kwa mfano Feb . 16,2017
Jinsi ya kusoma saa
kwa English
Kuna namna mbili za kusoma saa katika English
Aina ya kwanza ya
kusoma saa kwa English
Katika aina hii huwa tunaanza kutaja dakika kisha saa. Na kumbuka katika English saa hutajwa kama
mshale unavyoonyesha. Hivyo kwa mfano saa mbili asubuhi mshale utakua kwenye
namba NANE, nawe utasema EIGHT usiseme kama kwa Kiswahili tunavyosema MBILI
halafu ukasema TWO.
Mfano mweingine 7:25AM kwa Kiswahili ni saa moja kumi asubuhi ila kwa English
kumbuka tunasoma saa kama zilivyoandikwa hivyo badala ya MOJA tutasema SEVEN.
Kusoma dakika pia katika English kunategemea na je dakika zipo kabla ya 30 au
baada ya 30 kama unavyoweza kuona katika picha hapa chini.
Hivyo kwa saa 7:25AM jiulize je dakika zipo kati ya dk 1 hadi 30 ? Kama ndio
basi tumia PAST ukitaja dakika. Yaani mfano Twenty Five Minutes Past SEVEN.
Tukumbuke AM maana yake ni kuanzia saa sita kamili usiku
hadi saa tano na dk 59 asubuhi. Baada ya hapo ni PM
Aina ya Pili ya
kusoma saa kwa English
Namna nyingine ya kusoma saa kwa English ni kwa kutaja namba kwa makundi
mawili. Yaani kwanza kundi la saa kisha kundi la dakika. Mfano: 11:20 AM
utasema Eleven Twenty in the morning Mfano mweinine 1:20PM utasema
One twenty in the afternoon.
Hauna haja ya kusema ni afternoon au evening au night kama
unaongea na mtu moja kwa moja kwakua
huyo mtu atakua akijua unataja saa gani kama unachotaka kusema wakati huo ni
saa ngapi.
Angalia mfano hapa chini wa kusoma saa mbalimbali
Jifunze Zaidi:
Jiunge na group letu la WhatsApp kwa kutuma maombi ya kujiunga kwa namba hii +57 301 297 1724. Na pia karibu ujipatie kitabu chenye kanuni za msingi za kujua English. Kitabu kinaitwa English: Mbinu na Kanuni za Kuijua. Kitabu kinapatikana popote ulipo pale maana utatumiwa kwa email au kwa WhatsApp au kwa Facebook. Kitabu ni Tshs. Elfu Kumi na Tano.
NIKUPONGEZE KWA MAELEZO MAZURI NA YAKUELEWEKA. ILA NINASWALI JE? NI KITU GANI HASA CHAKUZINGATIA KUSUDI KUWEZA KUONGEA MAANA IYO NDO CHANGAMMOTO KUBWA ASANTE.
ReplyDelete