Je una wazo la biashara ila haujui unaanzaje kulifanya liwe
kweli ni bidhaa ? Je umekua ukibuni bidhaa Fulani Fulani ila haupati “bahati”
ya kufikia wateja wengi na kufaidika na bidhaa yako ? Basi jibu lipo katika
uwezo sahihi wa kuunda bidhaa kwa kitaalamu tunaita Product Development.
Ni kweli kuwa fursa zipo nyingi sana na kinachotakiwa ni
umakini wa kuziona. Ili uzione fursa wakati mwingine inakupasa uwe tayari una
taarifa nyingi nyingi kuhusiana na uwezekano wa kufanya jambo fulani, kwani kwa
hayo mambo ambayo unayajua ndio utaweza tambua kitu kinachowezekana kufanyika
wakati watu wengine wanaona haiwezekani, wakati wengine wanaona ni matatizo ,
wewe unajiumia kichwa kujua suluhu yake itakuaje.
Kuna namna nyingi ambapo "ideas" huja, na sio kila
idea inaweza kukuingizia fedha. Ukishapata idea itakupasa ujue namna ya
kuichambua, namna ya kutengeneza thamani kweli kweli ili walengwa wainunue, na
namna ya kupangilia vile utakavyoiwasilsha bidhaa au huduma yako uliyoweza
itengeneza kupitia "idea" yako.
Mchakato woote huu kitaalamu tunauita PRODUCT DEVELOPMENT.
Na ijumaa hii March 3, 2017 kupitia WhatsApp group na FB groups maalum,
nitaelezea mbinu mbalimbali tunazotumia ktk kubuni na kuunda bidhaa toka kwenye
idea mpaka kitu kinachoeleweka na kuuzika.
Haijalishi ni idea ya kuwa na app, idea ya kuuza bidhaa
fulani, au kutengeneza bidhaa fulani, yote tuyajadili kwa umakini. Utajifunza
namna ya kutafiti soko, namna ya kuunda VALUE kwa bidhaa yako, na mbinu za
kujaribu haraka haraka bidhaa yako. Pia utapata ufafanuzi kuhusu namna ya
kuwafikia wateja ili waweze nunua bidhaa zako.
Wasiliana nami kwa WhatsApp +57 301 297 1724 au +255 757 120
020 tukupe utaratibu wa kujiunga ktk somo hili la siku moja tuu.
0 comments:
Post a Comment