JINSI YA KUANZISHA BLOG: YOTE ULIYOTAKA KUYAJUA YAPO HAPA

Kila siku maelfu ya watu duniani wanafungua blog mpya. Pengine nawe ungependa kuanzisha blog yako. Changamoto katika blogging, ni jinsi ya kupata wasomaji wengi, na jinsi ya kuboresha blog yako siku hadi siku. Hivyo makala hii inakupa taarifa za awali za shughuli za blogging.

Takwimu
Teknolojia ya blogging, ambayo kwa mujibu wa Wikipedia, ilianza kutumika mwaka 1993, ilifikisha idadi ya blogs milioni 156 duniani kwa rekodi za mwaka 2011, Februari 26. Bila shaka idadi ya blogs kwa sasa ni zaidi ya milioni 300. Hakuna taarifa za hesabu ya idadi ya blogs za Tanzania, ingawaje kwa makadirio inaweza kufika zaidi ya elfu 50, hii ni kutokana na kuwa ni rahisi sana kuandikisha blogs kuliko kuziendesha. Tukifuatilia idadi ya blog hai, unaweza kukutana ni chache sana.

Kazi za blogs
Pamoja na kwamba wengi huanzisha blog kama jambo la kibiashara, kuna matumizi mengine mengi zaidi ya kuwa na blog kwa ajili ya kuingiza mapato. Blog inaweza kutumika kuandika habari binafsi, wengine huandika blog kama sehemu ya burudani/hobby kwakuwa wanapenda kuandika na wanapenda kutumia teknolojia, wengine huandika blog kwa ajili ya kufundisha mambo kadhaa, mfano mwalimu anaweza kuandaa blog kwa ajili ya darasa lake. Pia makampuni huwa na blog ili kutoa taarifa za bidhaa zao, pamoja ana maendeleo au mabadiliko fulani fulani katika uendeshaji wao. Wengine huanzisha blogs kama sehemu ya kutangaza bidhaa zao, mfano mzuri ni wabunifu wa mavazi wa Sinza Dar es salaam,  Rineez Arts.

Malengo: Malengo yako ya kuwa na blog, ndio yanakupa amri ya jinsi ya kuiendesha blogu husika. Mfano kama una malengo ya kuja kuuza matangazo, inabidi ujitahidi kweli blog yako ipate wasomaji wengi ambao wanajirudia rudia mara kwa mara kutembelea blogu yako. Hii ni kwasababu hakuna mtu au asasi ambayo ingependa kutangaza kwenye blog ambayo haina wasomaji- kwani matangazo yao hayatokuwa yakionekana na watu wengi. Malengo yako ndio yanaelekeza aina ya wasomaji unaotakiwa kuwalenga, na hivyo aina ya habari ya kuziweka kwa blogu yako.
Pengine kuwa na blogu ni njia tuu ya kufikia lengo fulani kubwa, mfano lengo lako linaweza kuwa ni kujenga network na watu wengi, hivyo kuwa na blog inayofahamika na watu wengi, na wewe kuwa na uwezo wa kufanya mawasiliano na wasomaji wako mmoja mmoja, ni sehemu pia ya mafanikio ya blog.

Kuandikisha blog: Kuna makampuni kadhaa yanayotoa huduma ya kurusha hewani bure blogs. Waweza kuwa na blog kupitia Blogger na kupitia Wordpress. Pia kuna Tumblr, Typepad, na Posterous. Unachotakiwa kufanya ni kujiandika kwa kampuni husika. Mfano kuwa na blogger blog, inabidi kwanza uwe na Gmail account, halafu unaenda kwenye address hii blogger home , na kufuata maelekezo ya jinsi ya kuandaa blog yako. Ambapo utaweza kuchagua jina la blog, anuani ya blog mfano mbuke.blogspot.com,na kisha utachagua muonekano wa blog yako – tunaita template. Baada ya kuchagua mambo hayo, tayari utakuwa umeweza kuwa mmiliki wa blog.

Kuendesha blog:  Kazi kubwa sio kuwa na blog, bali ni kuendesha blog, kwani kuna vipengele vingi sana vya kufuata ili kuwa na blog endelevu. Shughuli kuu za uendeshaji wa blog ni kuitangaza ili upate wasomaji wa hayo unayotaka kuandika. Kuna sababu nyingi kwanini watu waje  kutembelea blog yako,  ila kikubwa sana ni wewe kuweza kuwapatia habari au taarifa wanazozihitaji. Kuiendesha blog yako kuna maanisha kuandika makala  bora, kuwapatia taarifa watu kuwa blogu yako ipo hewani, na kuendelea kuwakumbusha kuwa ipo hewani.
Wewe mwenyewe kwa muda wako unaweza kujifunza mambo mengi ya msingi katika kuendesha blog toka jinsi ya kupata wasomajii wengi, kuandika makala nzuri, kuongeza urembo katika blog, kubadili template n.k. Baadhi ya sehemu unazoweza kupata kujifunza zaidi ni kama zifuatavyo:-
 http://www.problogger.net/
http://allbloggingtips.com/
http://www.spiceupyourblog.com/
http://www.bloggerplugins.org/
Wasiliana nami kwa WhatsApp +57 301 297 1724 upate mafunzo na maelekezo wewe kama wewe na kusaidiwa kuibuni na kuiboresha blog yako. Au niandikie email: john.myungire@gmail.com


Mikakati:  Ili uweze kuwa na blogu endelevu inabidi uwe na mikakati ya kimasoko kwa blogu yako, mikakati ya muundo wa habari zako, na mikakati ya usimamizi wa blogu yako ikiwa pamoja na jinsi unavyoweza kuboresha ubora wa muonekano wa blog na makala zako.
Mojawapo ya mikakati yako ya masoko inaweza kuwa ni kufungua ukurasa maalum wa Facebook. Hata hivyo kufungua ukurasa huko kuwa kwa mkakati maana kuna kazi kupata watu wa ku like ukurasa huo, na zaidi sana kuuendeleza ukurusa husika pamoja na blogu yako.

Mapato:  Mapato yanayotokana na blog yanaweza kuwa ni kutokana na matangazo, kuuza bidhaa kupitia blog yako, au hata kuamua kuja kuiuza blog yako maarufu kwa watu wengine, kama vile watu wanavyouza makampuni yao. Kwa upande wa matangazo, mapato yanaweza kuwa ya aina mbili – mapato ya moja kwa moja toka kwa asasi husika zinazotaka kutangaza kutoka blog yako, au matangazo kupitia Google – yanaitwa Google Adsense. Matangazo haya ya GoogleAdsense ni kuwa kama blog yako inakidhi viwango ambavyo Google wameweka, basi ukiwa umejiandikisha kwa ajili ya blog yako kupokea matangazo hayo,  utaweza kuona matangazo mbalimbali toka Google yakionekana kwa blog yako, na utalipwa kuendana na jinsi watu wanavyobofya na kununua bidhaa husika zinazotangazwa na Google.
Kuhusu mapato kutoka na kuuza bidhaa kupitia blogu yako ni kwamba wewe mwenyewe unaweza kuwa na bidhaa mfano unatoa huduma ya ushauri kwa wajasiriamali, basi ndio nafasi yako ya kuwapata wajasirimali kupitia blog yako. Au unaweza kujiandikisha na mfumo wa kuuza bidhaa wa watu wengine, na wewe ukalipwa posho (commission) kama watu watanunua bidhaa husika. Mfumo huo unaitwa Affiliate selling. Angalia orodha ya website zenye huduma ya Affiliate marketing/sales Hapa
Hivyo ingawa watu wengi hufikiria kuanzisha blogs ili wapate kuuza nafasi za matangazo, unatakiwa kujua kuna nafasi nyingi za kuingiza fedha zaidi ya matangazo.  Kinachotakiwa ni kujipanga, na kuwa na mkakati wa dhati wa ina gani ya mapato unayotaka kupata, na jinsi ya kuiendesha blog yako kwa kadri ya mapato unayolenga.
Kuna somo maalum kabisa tumeliandaa hapa Mbuke Times , waweza kulipata wakati wowote, kuhusu namna gani ya kuanzisha blog yenye faida kwa biashara. Angalia link hii: BLOG YA BIASHARA

Gharama: Kuna gharama nyingi za kuendesha blog, kama vile unaweza amua kuwa anuani tofauti na hizo za bure, hivyo mfano www.millardayo.com ni blog lakini ina anuani binafsi ambayo inalipiwa kila mwaka.
Wapo ambao watahitaji kuwa na muonekano bora wa blog zao, hivyo kuajiri mtu wa kuboresha muonekano au hata kuwa na muonekano mpya kabisa. Mfano Mbuke Times ni blog, ila hauwezi pata template kama hii kutoka templates zinazotolewa na blogger.
Na hata kama ukipata templates za bure, kama hii ya Mbuke Times, unatakiwa uwe na uwezo wa kubadilisha baadhi ya mambo kama vile background, au maandishi na kurasa nyingine zisizoendana na malengo ya blog yako. Kama hauwezi kufanya hivyo wewe mwenyewe itakubidi kuingia gharama ya mtu akufanyie. Ila usihofu gharama ya kuboresha blog yako. Wasiliana nami kwa email john.myungire@gmail.com au WhatsApp +57 301 297 1724 nitakuboreshea kwa gharama kidogo sana.
Gharama nyingine za uendeshaji wa blog ni manunuzi ya vifaa kama vile kamera, kompyuta, gharama za internet,  usafiri wa kuenda maeneo mbalimbali ili upate habari/taarifa. Pia zipo gharama za matangazo, zaidi sana muda mwingi utakaoutumia kutafuta taarifa,  kuandika makala, na kuitangaza blogu yako.
Share:

5 comments:

  1. kwani ni lazima watu waku follow kupitia email? maana nataka wasomji wa blog yangu wanifollow kupitia social network ninazotimia mimi

    ReplyDelete

  2. Thanks for sharing, nice post! Post really provice useful information!

    FadoExpress là một trong những top công ty vận chuyển hàng hóa quốc tế hàng đầu chuyên vận chuyển, chuyển phát nhanh siêu tốc đi khắp thế giới, nổi bật là dịch vụ gửi hàng đi đài loan uy tín, giá rẻ

    ReplyDelete