JINSI YA KUVUTA WATEJA WENGI KWA BIASHARA YAKO MTANDAONI

kuvuta_wateja_mtandaoni


Je umejiuliza ni kwa namna rahisi watu wanaweza kuja kwa biashara yako kupitia mtandao ? Je website yako inakupatia kweli matokeo ya kukuletea wateja ? Je umebaki tuu kutegemea kupost post kwa mitandao ya kijamii kama Instagram na FB ili watu wakufahamu na kununua bidhaa zako ?
Nakukaribisha ujaribu kitu tunaita Search Engine Optimization (SEO).
mfano_wa_seo_katika_blog



SEO ni namna ya kufanya injini za utafutaji wa taarifa kama vile Googel, Bing, Yahoo ziweze kutaja website yako katika kurasa ya mwanzo ya majibu wanayopewa watu wakitafuta. Angalia mfano pichani mtu akisearch Jinsi ya kujifunza tenses, mara moja Google ina majibu ambapo blog yetu ya MBUKE TIMES [www.mbuke.blogspot.com ] inatajwa katika nafasi za mwanzo kabisa kwakua tumeitengeneza kwa kuzingatia SEO.
Wakati mwingine huwa anatafuta picha, pia SEO inahusika kuwapatia watu majibu ya picha kama uwezavyo kuona picha toka blog yetu ya Mbuke Times.
SEO_na_picha

Umuhimu wa SEO kwa mjasiriamali ni kuwa watu wakibofya hicho ambacho Google imeonyesha wanaweza kuingia kwa website au blog yako, na huko wakapata kukutafuta.
Wapo wateja wangu wengi tuu waliosema walikua wakitafuta vitu kwa Google wakaona namba yangu au wakaonyesha makala zangu na baada ya kuenda kusoma wakavutiwa hivyo wakanitafuta niwahudumie.
Na ikumbukwe hata kama unayo NGO bado utahitaji SEO ili kuvuta watu waje kwa website yako.
Kutengeneza website bila kutumia SEO na kukaa tuu kusubiria watu waitembelee hakutoweza kukuletea watembeleaji wengi wa website yako. Unahitaji SEO kwa mafanikio ya website yako na NGO.
Je wewe unangoja nini ili blog yako au Website yako ipate kuonekana na watu wengi wanao search Google ? Anza sasa kutumia SEO.
Tuwasiliane kwa ushauri na kuwezesha blog au website yako iwe kweli juu katika matokeo ya search .WhatsApp +57 301 297 1724
Share:

1 comment: