NAMNA 4 AMBAPO TENSES ZITAKUPA MSINGI WA KUONGEA ENGLISH KWA UFASAHA

Karibu kila unachotaka kukizungumza katika English utahitaji kutumia tenses kuelezea hicho unachotaka kukieleza.
Tunaposema tenses tunamaanisha namna ya kuelezea muda na hali ya tukio. Kwenye tenses tuna tenses kuu tatu yaani past , present na future.
Halafu kwa kila mojawapo ya hizo tenses tuna hali kuu nne za continuous(kuendelea), perfect(kukamilika), simple (kawaida) na perfect continuous(kukamilika kunakoendelea).

Hivyo kwa mfano tukitumia perfect tenses hutuongoza kujua  sio tuu  kwa mfano ukamilifu wa tukio bali ukamilifu huo uliotokea muda gani yaani je tukio lilikamilika wakati uliopita ? au limekamilika muda mfupi uliopita au litakamilika muda ujao.

Makala hii inakupa mwanga kuhusu namna gani kufahamu tenses kutakupa msingi imara wa kuongea English kwa ufasaha.

1. Wakati sahihi wa tukio kufanyika:
Tenses hutumika kusema kama tukio lilifanyika wakati uliopita, litafanyika wakati ujao wakati uliopo. Bila kujua vizuri kuwa kuna tenses kuu tatu yaani past, present na future, itakua ngumu kwako kutoa sentensi ukizingatia taarifa sahihi. Mfano: Yesterday , she is eating - mtu akiwa anamaanisha kuwa jana alikula. Hapa kuna tatizo kwani mtu huyu hajazingatia ukweli kuwa IS EATING.. Inamaanisha wakati uliopo, hivyo haiwezi kutumika kuelezea tukio la wakati uliopita.

2. Hali sahihi ya tendo:
Kama tulivyoona hapo juu kuna hali kuu nne. Usipozijua hizo hali vizuri unaweza kutoa taarifa isiyokamili. Mfano: Unataka kusema Nimekula ila wewe ukasema I eat. Hapa umechanganya hali za perfect na simple hivyo ukisema I eat ina maana ya Mimi hula. Yaani ukisema I eat  ina maana ya tendo hilo hufanyika  mara kwa mara au ni tendo la kawaida. Ila  kusema tendo limekamilika unahitaji kutumia present perfect tense, hivyo ungesema I have eaten.

3. Je ni kauli ya kutendewa au kutenda:
Tenses zitakuwezesha  kutambulisha kama  unatumia kauli ya kutenda au kutendewa hivyo uweze kukamilisha sentensi kwa ufasaha.
Mfano: Unataka kusema :”Nilikula” ila unaandika hivi: I was eaten , hata hivyo kusema I was eaten hii ni kauli ya kutendewa yaani passive voice hivyo sentensi  I was eaten ina maanisha “ Nililiwa”. Ili uweze kusoma vema passive voice  unatakiwa ujue tenses kwanza.

4. Je kuna sharti katika sentensi husika
Tenses zitakusaidia kujifunza vema namna ya kuandika na kuongea sentensi zenye kuonyesha masharti au vitu vinavyotegemeana. Sentensi hizo kwa  English huwa tunaziita conditional sentences. Nasema tenses zitakusaidia kujua conditional sentences kwakua conditional sentences zote zinaandikwa kwa kuunganisha tenses fulani fulani. Mfano: Conditional sentences type 1 huandikwa kwa/ kuweka IF kisha Simple Present Tense…. Halafu malizia sentensi kwa kutumia Simple Future Tense. Mfano: Kama akija nitamuona. If he comes , I will see him. Hapa tunaona kuwa he comes  hii ni simple present tense, na  I will see him ni Simple Future Tense

Hitimisho
Kuunda sentensi katika English kunahitaji umakini mkubwa sana haswa kwenye matumizi ya tenses , na tumeona hapo juu kwanini unahitaji kujua tenses kwani jinsi utakavyounda sentensi unahitaji kuzingatia hayo mambo niliyotaja hapo juu ambayo yenyewe ili uyafanye vema unahitaji kujua kutumia tenses.
Kwahiyo kila uandikapo au kutaka kutamka sentensi ya English jiulize yafuatayo :
Kwanza :Je sentensi ipo katika tense gani ? - past, present, au future ?
Pili: Je sentensi inaonyesha hali ipi -perfect, continous, simple au perfect continous ?
Tatu: Je sentensi ni passive voice au sio passive voice ?
Nne: Je ni conditional sentence ? Kama ndio je ni  type zero, type 1, type 2 au type 3 ?
Katika kujiuliza maswali yote hayo utaona namna gani tenses zinavyohitajika.

Unatimizaje ndoto yako ya kujua tenses na English kwa ujumla ?
Tazama ukurasa wetu wa Jifunze English utaona makala kibao . BOFYA HAPA KUJIFUNZA ENGLISH BURE
Tuwasiliane kwa WhatsApp +57 301 297 1724 au john.myungire@gmail.com  ujipatie kitabu cha English chenye maelezo mazuri kuhusu tenses zote.
Kumbuka pia tunaendesha masomo binafsi kwa mtu mmoja mmoja anayetaka kujua English kwa ufasaha. Tuwasiliane uanze sasa kutimiza ndoto yako ya kujua English.
Share:

0 comments:

Post a Comment