JIFUNZE ENGLISH: TOFAUTI 6 KATI YA AMERICAN ENGLISH NA BRITISH ENGLISH

Ninaishi na mama wa kimarekani ambapo kwakua tumezoea kuongea English mbili tofauti yaani yeye American English na mie British English huwa tunajikuta tukibaki hatuelewani mara nyingi mpaka mmoja afafanue anamaanisha nini. Kwa kadri miaka inavyozidi kuenda kutokuelewana kati yangu na mama yangu huyu wa kufikia kunapungua kwani kila mmoja anajifunza utofauti wa lugha aliyezoea mwingine na hivyo kujiboresha katika kumuelewa.
Kabla wewe halijakukuta lililotukuta sisi, nataka nikusaidie kukuelezea utofauti ambao tumeuona kuhusu American English na British English ila kwanza tuanze kueleza huwa tunamaanisha nini tukisema American English , na je tunamaanisha nini tukisema British English.

American English ni nini ?
Ni aina ya kiingereza ambacho huzungumzwa nchini Marekani. Kumbuka hata ndani ya Marekani kwenyewe kuna namna tofauti tofauti ambapo English hutumika kutegemeana na jimbo au asili ya watu, mfano English ya watu wa kusini ya Marekani ni tofauti ukilinganisha na English ya watu wa maeneo mengine kama vile Kaskazini au Magharibi mwa Marekani.

British English ni nini ?
Ni aina ya kiingereza ambacho hutumika nchini Uingereza .Hata  nchini Uingereza pia watu wa maeneo tofauti tofauti ya Uingereza huwa na utofauti wa hapa na pale katika kuzungumza, mfano mtu wa Liverpool anaweza kuwa na aina tofauti ya matamshi ukilinganisha na mtu wa Manchester.

Kutegemeana na nchi imetaliwa au imekubali kwa kiasi kikubwa utamaduni wa Markeani au wa Uingereza , nchi au mahali husika hukumbwa na matumizi makubwa ya British au American English. Mfano kwakua tulitawaliwa sana na waingereza nchini Tanzania huwa tunatumia zaidi British English. Wakati hapa nchini Colombia wamepokea sana utamaduni wa kimarekani hivyo hata English inayofundishwa hapa mara nyingi ni American English.

Tofauti kati ya American English na British English ni kama ifuatavyo:

1.Matamshi:
Katika American English T hutamkwa kama L mfano little  itatamkwa lilo, beautiful - itatamkwa byuliful.
Pia kumbuka kuwa katika American English mara nyingi hutamka kila r katika neno wakati katika British English hutamka r endapo tuu ni herufi ya kwanza katika neno.

2.Uandikaji wa maneno.
Kuna maneno mengi katika American na British English ambayo huwa yana maana sawa hata hivyo huandikwa tofuati. Angalia mfano hapa chini.
utofauti_maneno_american_vs_british_english


3.Misamiati tofauti kati ya American na British English
Kuna maneno katika American English ni tofauti kabisa na jinsi maneno hayo yanavyomaanisha katika British English, hivyo hivyo maneno ya British English ambayo ni tofauti kabisa na yale ya American English. Angalia mfano hapa chini.
misamiati_american_vs_british_english

4.Matumizi ya Past Simple vs Present Perfect
Katika American English huwa badala ya kutumia present perfect mara nyingi hutumia simple past tense , mfano  Nimekula ugali - I ate ugali hii ni American English, ila  kwa British English huwa tunasema I have eaten ugali.
Mfano mwingine : Je umemuona mwalimu ? Kwa American English tumia Simple Past hivyo ingekua Did you see the teacher ? Ila kwa British English tunahitaji kutumia Present Perfect Tense : Have you seen the teacher ?

5.Matumizi ya neno Get
Kwenye American English huwa tunatumia  gotten , ila kwenye British English huwa tunatumia got. Mfano:  Nina matatizo mengi  - I have gotten many problems. Ila kwenye British English tutatumia I have got many problems.

6.Majina ya jumla - collective nouns:
Kwenye American English , majina yanayoonyesha makundi kama vile team, band  huandikwa kama ni majina ya umoja, ila kwenye British English huwa tunaandika kama vile ni wingi, mfano:
American English:  Real Madrid is a soccer team from Spain.
British English: Real Madrid are a football team from Spain.
Tafsiri: Real Madrid ni timu ya mpira wa miguu kutoka Hispania.

Hitimisho:
Hapa Mbuke Times tumekuandalia masomo mengi ya kukuwezesha kujua vema English. Bofya link hii kujifunza zaidi.
Pia tuna group la WhatsApp ambalo utapata nafasi ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara na kuongea na wengine English na pia kupata kusahihishwa pale unapokosea English.   Na kama hiyo haitoshi tuna darasa maalum la wewe na mwalimu tuu - personalize English class , ili ufundishwe kuendana na matatizo yako ya English, haijalishi kiwango chako cha Elimu ni kipi, tuna wanafunzi wa darasa la saba hadi wa Masters degree. Kila mmoja kwa nafasi yake atafundiswa tena kupitia mtandao, hivyo popote ulipo unaweza kujifunza. Tuna wanafunzi waliopo nje ya Tanzania, na karibu mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani. Njoo ujifunze na wewe. Kumbuka kutuandikia meseji WhatsApp +57 301 297 1724 au john.myungire@gmail.com
Share:

1 comment: