Badala ya kuita kichwa cha habari jinsi ya kujifunza English kama hujui tungeweza pia kusema jinsi ya kujifunza lugha yoyote ya kigeni kwa mara ya kwanza kwani utakayosoma hapa ni mambo ambayo hata mie niliyafuata nilipojifunza lugha nne za kigeni zikiwemo English na Spanish. Kanuni au mbinu utakazosoma hapa ndizo ambazo nimekua nikizifuata kwa miaka zaidi ya 10 nikifundisha English kwa watu wa viwango tofauti vya elimu ikiwemo wale walioishia elimu ya shule ya msingi, walioshia sekondari na wale wa vyuo vikuu.nitakupatia
1.Fahamu kila lugha ina muundo wake maalum
Elewa kuwa lugha unayoongea wewe Kiswahili ina muundo tofauti na namna tofauti za kuandika na kumaanisha mambo. Lugha yoyote ni sehemu ya tamaduni ya wazawa wa lugha hiyo hivyo kufahamu lugha inabidi uielewe lugha husika kwa mtazamo wa hiyo lugha sio kama wewe unavyoielewa lugha yako ya Kiswahili.
Hapa namaanisha kuwa fahamu aina za maneno na kanuni zinazohusika na maneno hayo. Mfano I am going to school . Kwanza fahamu katika sentensi hii kuna maneno MATANO yaani 1. I 2. AM 3. GOING 4. TO 5. SCHOOL. Haya maneno yanaangukia katika aina mbalimbali za maneno. Kwenye English tuna aina hizi za maneno nouns, pronouns, adjectives, adverbs, verbs, prepositions, conjunctions na interjections. Kufahamu hatua kwa hatua jinsi kila aina ya maneno hapo juu inavyomaanisha na inatumikaje ni muhimu sana ili uweze kujua utatumiaje maneno.
Tumesema English ina muundo tofauti kwani kuna namna tofauti za kuunda sentensi kwahiyo usipojua vema utajikuta ukitaka kutafsiri neno kwa neno toka English kwenda Kiswahili na usiweze kuleta maana sahihi. Au utataka kutafsiri Kiswahili kwenda English neno kwa neno na usipate maana iliyo sahihi.
Kwahiyo mwanzoni kabisa mwa kusoma lugha yeyote, kama English ni kufahamu na kukubali kuwa kuna utofauti mkubwa hivyo basi ukubali kuielewa lugha nyingine kama ilivyo na sio kutaka kuifananisha lugha nyingine na lugha yako.
Nasema hivi kwa sababu kwa mfano katika sentensi I am going to school - tafsiri yake sahihi kwa Kiswahili ni kuwa NINAENDA SHULE. Hapa tunaona kabisa kwenye Kiswahili tuna maneno mawili tuu, wakati kwenye English sentensi hiyo hiyo imeandikwa kwa maneno matano.
2. Dhamiria kuweza English kwa ufasaha
Dhamira yako ndio itakayoamua namna gani utajifunza na kuweka bidii katika English. Kama unajifunza English ila kichwani unajiambia kuwa hauwezi na hauihitaji kuijua kwa undani basi hivyo ndivyo utakavyoishia kwani kusoma ni kugumu na kama hauna dhamira ya kutosha, hautoweza kujituma na kuvumilia ugumu utakaokumbana nao.
Epuka marafiki ambao wanabeza ujuaji wa English kikweli kweli. Epuka maneno ya waliokata tamaa ya kujifunza English kwa ufasaha. Hujui kwanini wanasema wanayosema. Pengine wao hawakufahamu mbinu rahisi za kujifunza English, pengine toka mwanzo hawakuwa na mikakati ya kutosha, muda wa kutosha na wengine ni uvivu wa kujituma zaidi pale mambo yanapokua magumu katika kujifunza. Hivyo wao sio wewe. Kama unataka kujua English jitume wewe kama wewe, jiambie hiyo ni changamoto na wewe unaweza kabisa kuishinda.
3.Jizoeshe kusikia na kusoma English iliyo sahihi
Kama tulivyoona hapo awali kuwa lugha tofauti zina miundo tofauti ya jinsi ya matumizi ya maneno hivyo basi ukijizoesha kusikia na kusoma English iliyo sahihi utaweza kuzoea kusikia muundo wa sentensi na muelekeo wake.
Mfano utagundua kuwa kumbe katika English kama unataka kumuuliza mtu ameamkaje utasema tuu “How did you sleep ?” na sio kama ambavyo ungeweza sema kwa tafsiri ya moja kwa moja ya Kiswahili kwenda English: “ How have you woken up ?”
Mfano mwingine badala ya kumuita mpishi COOK wewe ukamuita COOKER, kwa sababu tuu umejiambia kama anayefundisha (teach) ni TEACHER basi anayepika (cook) ni COOKER. Au kwa mfano ukataka kusema “mambo madogo madogo” ukasema kwa English “small small things” kitu ambacho hakipo badala yake sema tuu “minor things”.
4. Tafuta msaada wa maelekezo
Kukosea kuandika na kuzungumza kunaweza kuwa tatizo kubwa sana ila utakapokua na mwalimu au mtu wa kukusaidia kukuweka sawa ni hatua njema ya mafanikio yako katika English.
Mwalimu mzuri atakusaidia sio tuu kujua kanuni za English bali pia kukuboresha katika kuzoea uandishi wa English kama English na sio kutafsiri toka Kiswahili kwenda English.
Kumbuka hapa Mbuke Times tunaendesha mafunzo ya English tena kupitia mtandao kiasi kwamba wewe na mwalimu wako mtaweza kuwasiliana na atakueleza kanuni zote za English na muundo wa English . Huna haja ya kutoka nyumbani kwako au ofisini, popote ulipo utaweza kusoma kwani masomo yanaendeshwa kupitia WhatsApp, Skype , Facebook na Imo.
Wasiliana nasi kwa namba WhatsApp na Imo +57 301 297 1724 tukuelekeze namna ya kuanza masomo haya. Au tucheki kwa email: john.myungire@gmail.com
5. Soma maelezo toka vyanzo mbalimbali
Pamoja na kwamba sisi hapa Mbuke Times tumeandika kitabu chetu kabisa cha English kiitwacho: English: Mbinu na Kanuni za Kuijua, ambacho kina maelekezo ya kanuni zote za msingi na mbinu za kuijua English, bado tunasisitiza wanafunzi wetu watafute kusoma vitabu tofauti na kufanya mazoezi tofauti.
La msingi ni kuwa kusoma vitabu au kutembelea websites tofauti tofauti huchangia kuelewa kwa urahisi English kwani utakua unajizoesha kuona English ikitumika katika maeneo tofauti tofauti.
Hata hivyo, kama ndio kwanza unaanza kujifunza English , jikite kwenye kitabu kimoja ili upate mtazamo wa jumla wa English , kisha kadri unavyoendelea kujifunza ndio uongeze idadi ya vitabu au websites unazotembelea kujifunza English.
6. Fanya mazoezi ya English mara nyingi sana
Kujifunza English kunaweza kuwa kugumu sana ukizingatia na ukweli kuwa kwanza ni lugha nyingine na tamaduni tofauti. Kuna kanuni nyingi na maneno mapya ya kuyafahamu. Yote haya kuyafahamu yanataka muda na marudio ya mara kwa mara ili yakae kichwani. Usipokua na nafasi ya kufanya marudio marudio utasahau na hivyo utaona kuwa kusoma English ni shida.
Jitume usome mara kwa mara kwa bidii zote utaweza. Katika hili utaona umuhimu wa mwalimu binafsi maana atakusaidia kukupatia mazoezi ya mara kwa mara na kukusahihisha. Kuwa na mwalimu kutakufanya uwe na nidhamu ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara, ila ukijiachia wewe mwenyewe utapitisha tuu muda wa kusoma.
Kumbuka Mbuke Times itakupatia mwalimu binafsi wa kukuelekeza , kukupatia mazoezi na kukusahihisha. Tucheki kwa WhatsApp +57 301 297 1724 au kwa email john.myungire@gmail.com
0 comments:
Post a Comment