Wengi wanapozungumzia ujasiriamali huusisha na kufanya biashara. Ingawa ni kweli kuwa kuanzisha na kufanya biashara ni kazi kubwa ya ujasiriamali, maana halisi ya ujasiriamali ni pana , labda tuu tuseme ujasiriamali huanza kabla ya kuanza biashara na ni zaidi ya kufanya biashara.
Katika makala hii utajifunza maana halisi ya ujasiriamali ili uweze kujipima kama kweli unataka kuwa mjasiriamali kwa maana ya kwamba upo na sifa au unataka kujituma ili uwe na sifa ya kuwa mjasiriamali wa kweli, kwani wengi wanaweza kujifunza ujasiriamali hata kama hawakuzaliwa kuwa wajasiriamali.
Maana ya ujasiriamali
Ujasiriamali ni namna unavyoweza kufikia suluhu ya matatizo fulani na kupitia utoaji wako wa suluhu wa tatizo husika ukalipwa. Tunaposema suluhu maana ya kuwa kuja na kitu fulani ambacho kitaboresha hali iliyopo ambayo inawatatiza watu wengi. Sio lazima UTENGENEZE KITU KIPYA KABISA, lakini hata ukabuni namna bora zaidi ya kufanya kinachofanyika sasa ni ujasiriamali. Sio kila anayefanya biashara ni mjasirmali, wengi ni wafanyabiashara tuu.
Ndio maana tunasema kwenye ujasiriamali kuna RISK kwakua unakuja na kitu fulani au namna fulani ya kufanya jambo ambayo sio kila mtu anayo au aliitarajia. Inabidi kufikiria vema namna gani utakachofanya kitaleta kweli manufaa kwa jamii na wewe utalipwa. Hivyo kwa kifupi
UJASIRIAMALI ni NAMNA YA KUBUNI NA KUFANIKISHA ULETAJI WA HUDUMA AU BIDHAA FULANI YENYE MANUFAA KWA WALENGWA NA WALENGWA HAO WAKAKULIPA.
Mchanganyiko uliopo kati ya ufanyabiashara na ujasiriamali
Ni rahisi kufikiria tuu kuwa mjasiriamali ni MFANYABIASHARA. Lakini ukiangalia kwa mapana yake, si kila mfanyabiashara ni mjasiriamali.
Kwa mfano kama wewe umemuona jirani yako kaanza kupika chapati , na wewe kesho unaanza kupika chapati uuze kama yeye afanyavyo , hapo hakuna ujasiriamali.
Ila kwa mfano kama ukaona kuwa kumbe watu wengi wanaokuja kununua chapati hutaka wafungiwe wakazile maofisini mwao, wewe ukaja na mtindo wa kupika chapati, ukaziweka katika mfuko maalum ambao utahakikisha chapati hizo zinabaki za moto hadi hapo walaji watakapozihitaji basi huo ni ujasiriamali. Kwa sababu umeenda mbali zaidi na kujua namna gani ufanye ili kutatua hali fulani , na umekuja na kitu bora zaidi.
Ila kwa mfano kama ukaona kuwa kumbe watu wengi wanaokuja kununua chapati hutaka wafungiwe wakazile maofisini mwao, wewe ukaja na mtindo wa kupika chapati, ukaziweka katika mfuko maalum ambao utahakikisha chapati hizo zinabaki za moto hadi hapo walaji watakapozihitaji basi huo ni ujasiriamali. Kwa sababu umeenda mbali zaidi na kujua namna gani ufanye ili kutatua hali fulani , na umekuja na kitu bora zaidi.
Ujasiriamali ni zaidi ya biashara
Ujasiriamali sio tuu mpaka uwe kwenye kufanya biashara. Kama tulivyoona hapo awali ni kuwa ujasiriamali ni namna ya kubuni na kufanikisha uwepo wa kitu chenye thamani kwa walengwa. Hivyo mtu anaweza kuwa mjasiriamali hata sehemu ya kazi yaani mahali alipoajiriwa. Mfano badala badala ya kukubali tuu kufanya mambo kwa mazoea na hata yanayolalamikiwa kuwa ni shida, wewe unaweza kuja na njia bora zaidi ya kufanya kazi husika, na wengine wakakuiga.
Ujasiriamali si wa kila mtu
Ujasiriamali unakutaka uone yanayowezakana mahali ambapo wengine wanaona haiwezekani. Ubunifu na uthubutu na ufahamu wa nini unachofanya. |
Ujasiriamali unahitaji kuwa kweli unayependa kuboresha mambo. Uwe mtu usiyekubali tuu hali kama ilivyo. Je unajiona wewe ni mdadisi wa mambo ? Je unatamani kuwa tofauti na mwingine au kufanya mambo fulani ambayo ni ya kipekee au ya zaidi ya watu wengine ?
Je unawaza kujiajiri zaidi ? Je unajiamini wewe mwenyewe na unajiona unao uwezo wa kufanya mambo makubwa au ni mtu wa kukata tamaa ?
Ujasiriamali unataka kukubali kufanya mambo katika mazingira ya kwamba inawezekana kabisa jambo hilo lisifanikiwe, ila kutokufanikiwa kwa jambo hilo hakukuumizi kichwa, unachoangalia wewe ni kuwa kama jambo hilo likifanikiwa basi litaleta manufaa kwa hao unaowalenga.
Ingawaje ni kweli kuwa ujasiriamali unaweza kufikia hatua ya kukuleta faida ya kifedha, lakini wajasiriamali wa kweli huongozwa na vitu vya ziada katika kufanya shughuli zao wanazozifanya. Wao huona mbali zaidi ya faida ya leo. Wajasiriamali huona kweli uwezekano wa kuingiza fedha kama shughuli wanayoifanya itafanikiwa, lakini fedha sio jambo la kwanza linalowapeleka kufanya hicho wanachokifanya.
Hitimisho:
Je upo tayari kufanya ujasiriamali wenye mafanikio ? Zipi ni changamoto zinazokukumbuka ? Je una biashara ambayo ungepena uifanye kwa mafanikio kama mjasiriamali ? Au labda unahitaji mafunzo au ushauri binafsi wa hatua kwa hatua ili uwe mjasiriamali mzuri. Tuwasiliane kwa WhatsApp +57 301 297 1724 au email john.myungire@gmail.com
SoMo zuri sana nimeelewa zaidi maana ya ujasiriamali kuliko hapo kabla
ReplyDeleteShukran kwa somo zur
ReplyDeleteMaelezo mazuri sana
ReplyDelete