Ni kawaida kuona watu wengi wakitumia vifupi katika English bila kuzingatia kanuni za lugha ya English. Matokeo ya kutotumia vifupi hivyo kwa usahihi ni kupoteza maana iliyokusudiwa.
Katika makala hii tuangalie namna sahihi ya kuandika vifupi kwa usahihi kama vile you’re, it’s , we’re, they’re, that’s n.k.
I am kifupi chake sahihi ni I’m na sio AM kama wengi ambavyo huandika. Elewa kuwa AM ni auxiliary verb au verb to be kutegemeana na wapi imetumika , na hutumika mwanzoni peke yake endapo tuu unataka kuandika swali. Mfano: Am Iate ? Hapa ni swali je nimechelewa ?
Kinachotokea unapochanganya vifupi katika English
Ni kwamba wengi wanapochanganya hivyo vifupi ni kwamba huandika maneno mengine ambayo hubeba maana tofauti. Hii hutokea kwakua maneno ambayo wengi huchanganya hutamkika kwa ufanano mkubwa . Angalia mifano hapa chini:
They are kifupi chake sahihi ni They’re ila wengi huchanganya na kuandika Their. Hata hivyo their ina maana ya YAO au CHAO, VYAO, wakati They’re sahihi ina maana ya Wao ni.
It is kifupi chake sahihi ni It’s ila wengi huchanganya na kuandika Its. Hata hivyo Its maana yake YAKE, WAKE n.k, wakati It’s sahihi ina maana ya Yeye ni .
You are kifupi chake sahihi ni You’re hata hivyo wengi huandika Your. Hata hivyo Your ina maana ya Yako, wako au Chako, wakati You’re iliyo sahihi ina maana ya Wewe ni .
That is kifupi chake sahihi ni That’s hata hivyo wengi hukosea kwa kuandika Thats. Hakuna neno thats, hivyo kuacha mtu aonekane
Will not kifupi chake sahihi ni Won’t , hata hivyo kwa makosa wengi huandika wont bila kuwa apostrophe , hata hivyo hilo neno wont lisilo na apostrophe humaanisha kitu tofauti kabisa yaani tabia fulani ambayo mtu kaizoea.
Shall not kifupi chake sahihi ni Shan’t , hata hivyo wengi huandika kimakosa bila kuweka apostrophe hivyo kuwa shant ambayo inaweza kumaanisha kukosea, au kujisaidia kwenye nguo au mtu aliyejisaidia kwa nguo yake.
Vifupi vyenye kubeba maana tofauti tofauti hata vikiandikwa kwa usahihi katika English
Inabidi kuwa makini na maneno yenye apostrophe na S kwa sababu huweza kuwa na maana tofauti. Jinsi ya kujua maana sahihi ni wewe kusoma kwa umakini sentensi nzima na mazingira ya sentensi kujua maana halisi iliyokusudiwa. Angalia mifano hapa chini:
She’s .. inaweza kuwa She is, She has au She was
Mifano:
She’s gone to school - hapa She’s inasimama badala ya She has .
She’s eating .. hapa she’s inasimama badala ya She is.
She’s on the phone when I came in. Hapa She’s inasimama badala ya She was.
Zingatia hilo tulilolisoma hapo juu kwa maneno He’s , It’s .
Mifano zaidi ya vifupi
Picha ifuatayo inaonyesha mifano zaidi ya vifupi zaidi katika English. Soma kwa umakini vifupi kama vile vifupi vya Should have, would have, could not, would not n.k
Kama umeinjoi somo hili tafadhali share na wengine wajifunze zaidi huko Facebook au kwa WhatsApp. Na kama unataka kujifunza zaidi tuwasiliane kwa WhatsApp +57 301 297 1724 au kwa email john.myungire@gmail.com tuna group maalum la WhatsApp utakaloweza kufanya mazoezi ya unachokijua na wengine na kupata kurekebishwa.
Pia tuna mwalimu ambaye ataweza kukufundisha wewe mwenyewe binafsi kwa kukubaliana muda na namna ya kusoma. Hauna haja ya kutoka kwako au ofisini kumfuata mwalimu. Utaweza soma yote kupitia simu yako ya mkoni. Tuwasiliane ujue zaidi utaratibu huu wa mwalimu wa English upoje.
Hii namba yako niya nchi gani mkuu
ReplyDelete