FIKRA 6 AMBAZO SI ZA KWELI KUHUSU BRAND

Brand ikieleweka vizuri na kujengwa kwa usahihi inaweza kuleta faida kubwa sana sio tuu kwamba utafahamika au biashara yako kufahamika, ila kuna faida nyingi ikiwa pamoja na kupata mapato makubwa, kufanikiwa kupata wafanyakazi bora na kupata ushirikiano na washirika mbalimbali.
Hata hivyo watu wengi wamekua hawaelewi kwa usahihi kuhusu brand , hivyo makala hii itakupa ufahamu kuhusu brand na kuondoa zile fikra potofu ambazo pengine ulikua nazo.

1. Kutengeneza brand ni swala linalohusu makampuni tuu au wafanyabiashara:
UKWELI: Hata mtu binafsi anahitaji brand. Ukiachilia mbali watu binafsi hata asasi za kiraia, asasi za kiserikali na nchi kwa ujumbla wake zinahitaji kuzingatia swala la brand. Ndio maana kwa mfano Afrika Kusini wana asasi maalum iliyoundwa mwaka 2002 kwa ajili ya kusimamia South Africa kama brand. Asasi inaitwa Brand South Africa.
2. Brand ni ubunifu tuu mzuri wa logo na rangi ambazo biashara itatumia:
UKWELI: Ingawaje ni kweli kuwa rangi maalum na logo ni sehemu ya brand, hivyo viwili pekee haviwezi kutengeneza brand.
3. Brand ni bidhaa:
Kwa mfano kama mie nauza soda, basi soda yangu ndio brand yangu.
Ukweli: Brand na bidhaa ni vitu viwili tofauti. Brand itakusaidia kuuza bidhaa zako endapo utakua na brand nzuri.
4. Matangazo yatakuboreshea brand:
Ingawaje ni kweli kuwa kujitangaza kupitia njia mbalimbali kama vile magazetini, redioni, kwenye tv na mitandao ya kijamii kutakuwafanya watu waijue brand yako, lakini ili kujenga brand imara na yenye kukuletea faida kweli unahitaji zaidi ya matangazo. Hata namna matangazo yako inabidi iwe ya ubunifu na mkakati mkubwa ili kweli ujenge brand unayokusudia.
5. Brand ni swala la marketing tuu:
Marketing huchukua nafasi kubwa katika kutengeneza brand , hata hivyo brand ni swala linalohitaji mambo zaidi ya marketing. Kama ni biashara au asasi unahitaji kupanga mikakati mingine mingi ya usimamizi wa wafanyakazi, uzalishaji wa bidhaa , mambo ya usimamizi wa fedha , yote hayo huathiri brand yako.
6. Kutoa ujumbe tofauti tofauti kwa wateja:
Kama unataka kujenga brand inakupasa ujipange vema ili uhakikishe unataka ufahamike kwa watu. Swala sio tuu kutoa ujumbe na kuwafikia watu wengi, bali katika brand la msingi ni aina gani ya ujumbe unaousambaza na msisitizo gani unauweka. Hivyo kama unaonyesha taswira tofauti tofauti katika namna unavyofanya mambo au matangazo yako basi itakua shida kwa walengwa wako maana watashindwa kujua namna gani wakutazame wewe, na hivyo utashindwa kujenga ule ukaribu unaotarajia kuujenga.
Angalia hata rangi unazotumia mara kwa mara kwenye logo, website au matangazo yako inabidi ziwe za aina moja katika sehemu zote sio kwenye website kuna rangi nyingine, kwenye page ya Facebook rangi nyingine. Au logo ya Instagram nyingine , logo ya Facebook nyingine na iliyopo kwa website yako ni nyingine.

MBUKE TIMES tumedhamiria kukusaidia kufanikisha kutengeneza brand yako iwe wewe kama mtu binafsi, au asasi isiyo ya kiserikali (NGO) au ni kwa ajili ya shughuli zako za #ujasiriamali tutalifanikisha hilo.


Tutafute kwa Facebook au kwa WhatsApp +57 301 297 1724
Share:

0 comments:

Post a Comment