MAMBO 6 YA KUFANYA ILI KUTIMIZA NDOTO YA KUFANYA BIASHARA UIPENDAYO


mambo ya kufanya ili kufanya biashara uipendayo
Makala hii ni katika kukusaidia wewe ambaye unatamani kufanya biashara ila haujui uanze wapi. Wapo wengi kama wewe wamebaki kusita sita wasijue wapi pa kuanza au biashara ipi ya kufanya. Usikubali ubaki na kigugumizi. Fahamu haya uanze mara moja biashara yako.
Makala inaanza na swali toka kwa mmoja wa wasomaji wa Mbuke Times.
Unashauriwa usome pia (Bofya link ifuatayo):

Swali kuhusu nini cha kufanya ili kuweza kuanzisha biashara yenye mafanikio:
Me na ndoto ya kua mfanyabiashara mkubwa hapa Tanzania na pia duniani kwa ujumla .
Dhumun la mm kukutafuta nlikua naomba msaada wako wa mawazo nifanyeje maana ndo naelekea kufanya mtihan wa taifa form 6 on may 2 na nlikua na ndoto ya kuzalisha sabun za maji I mean production of liquid soap nlkua na naomba nitumie mbinu gan il niweze kua mjasilia Mali bora hapa Tanzania ili niweze kufikia malengo yangu  I am interested in this please help me.Thanks.

Jibu kuhusu mambo ya kufanya ili uwe na biashara endelevu na yenye mafanikio:
Ni jambo bora kutaka kuwa mjasiriamali. Nitakueleza hapa mambo ambayo inakupasa kuzingatia halafu unitafute kwa WhatsApp ili tuongee zaidi +57 301 297 1724.
Mambo ya kuzingatia ni:
1.  Kuwa makini toka mwanzo kujua nani haswa watakua wateja wa biashara yako.
2. Chunguza kweli kweli nini haswa watu wanataka katika soko kuhusiana na sabuni. Usikubali tuu kutengeneza bidhaa kwa sababu wewe unapenda kufanya hiyo product. Ingawaje uzuri na ubora wa kitu ni muhimu katika kuuza bidhaa, lakini kama si kitu ambacho mtu anakihitaji hatonunua.
3. Jiwezeshe kweli kweli katika ufahamu wa utengenezaji wa hiyo bidhaa yako. Kwani watu hawataki tuu bidhaa ili mradi , na kama unataka kutoka haswa basi inabidi uwe na kitu special cha kuwapa watu.
4. Jifunze kuhusu masoko na kujitangaza. Uwe makini na social media, fikiria namna gani unataka kujitambulisha katika jamii ili kweli watu wakukubali.
5. Anza sasa kujionyesha kupitia mtandao, na hata nje ya mtandao kuwa mtu unayejiheshimu na unayeweza kuaminika kwani ili uweze kuwauzia watu inabidi kwanza wakuamini na kutazamia mazuri toka kwako.

6. Usisubiri mpaka mambo yakae vema kama unavyofikiria kichwani mwako eti  uanze kujaribu hiyo biashara. Wapo wengi huwa na mawazo mazuri lakini hawaanzishi biashara kwakua  wanajiwekea vikwazo vingi wao wenyewe, vikwazo ambavyo  havina msingi kwakua biashara inahitaji sana kujaribu. Ukishajua bidhaa gani unataka kutengeneza, umeshatambua nani haswa unawalenga kuwauzia , anza mara moja kidogo kidogo, usiwaze kutaka kuanza biashara katika kiwango kikuubwa. Mara kwa mara biashara hukua baada ya kujifunza mambo madogo madogo , na kuwa na imani kuwa mambo yataenda sawa. La msingi ni kujifunza, uwe na subira na ujue kuwa katika biashara swala sio kupata mapato swala la msingi ni kutimiza mahitaji ya watu na kujifunza kujiboresha siku hadi siku. Ukiingia katika biashara kwa lengo la kutaka “kupiga hela” uishie zako,  unaweza jikuta upo katika wakati mgumu sana.

Share:

3 comments:

  1. habari ndg ahsante sana kwa makala yako ni nzuri mno samahani naomba ushauri nawezaje kuanzisha car wash services???

    ReplyDelete