JINSI YA KUSHINDA USHINDANI MKUBWA WA KIBIASHARA ULIOPO SASA

mabadiliko_ushindani_kibiashara
Hivi karibuni mwekezaji mkubwa duniani Warren Buffet ameuza hisa zake nyingi za kampuni ya Walmart kwakua anasema Walmart haielekei pazuri kibiashara kwani biashara kubwa ya rejareja inaelekea kufanyika kupitia mtandao na sio supermarkets kubwa kubwa  kama za Wallmart.  Wallmart imepoteza mauzo kwa kiwango kikubwa wakati wauzaji wa rejareja wa mtandaoni waitwao Amazon ndio wameshika kasi sasa. Tulisikia pia jinsi NOKIA ilivyopoteza biashara ya simu za mkononi .
Tuangalie katika makala hii namna gani unaweza kujidhatiti ili biashara yako isipitwe na kupotezwa na ushindani.

Mabadiliko ya ushindani yanavyoathiri biashara yako
Kampuni au wajasiriamali wengi hupoteza biashara wakati mwingine sio kwasababu kuna kitu fulani wanakosea, ila ni kwa sababu hawakuendana na kasi ya mabadiliko katika soko. Mabadiliko hayo yanaweza kuwa ya kiutendaji, kiubunifu au kiteknolojia.

Katika kufanya ujasiriamali haitoshi tuu kuwa mzuri katika hicho unachofanya, yaani kuwa na bidhaa nzuri na bei poa. Haitoshi tuu kuwa na soko kubwa leo na watu wanaokuzunguka na kukubali leo. Kwakua biashara yako sio tuu kwa ajili ya leo, unahitaji kuwa na mkakati wa namna gani utapita katika nyakati tofauti tofauti za kijamii, na kimaendeleo. Unahitaji kuwa mwepesi wa kubadilika.

Mabadiliko gani mfanyabiashara anahitaji ili asipotezwe na ushindani
Mfanya  biashara  hautoweza kubadilika kama haujiwekei mpango wa kujifunza ili uweze kweli kujua unabadilika kivipi na wakati gani haswa ni muafaka kubadilika.

Inakupasa ujijengee utamaduni wa kutaka kujua zaidi nini kinaendelea katika ulimwengu wa biashara, je mbinu gani zinafaa kwa sasa za kimatangazo , uendeshaji wa biashara n.k

Kwa mfano, biashara kibao sasa zimeingia kutumia kwelikweli blogs ana mitandao ya kijamii kama sehemu za kujitangaza  na kuuza bidhaa zao. Hata hivyo hata mitandao hiyo nayo inahitaji ubunifu na mikakati ya kutosha ili kweli ikuletee faida na usipitwe na wakati.

Tatizo la mabadiliko ni kuwa hukuathiri kidogo kidogo , na usipokua makini unaweza kudhani kila kitu kipo sawa, hadi uje ushtuke kuwa mabadiliko hayo yamekuathiri , tayari athari zake zimeshakua kubwa na pengine hutoweza tena kujiboresha ili uweze kushinda katika ushindani.

Ufanye nini sasa ili kutokupitwa na mabadiliko ya ushindani ?

  • Weka mkakati wa kujiendeleza  ili ujue mabadiliko yanaendelea katika ulimwengu wa biashara yako.
  • Tilia maanani sio tuu namna gani unavyojiboresha na biashara yako bali pia mabadiliko yanayofanywa na wengine wanaofanya biashara kama  yako au biashara zinazofanana na biashara yako.
  • Fikiria biashara yako kwa mapana zaidi kwani mambo yanayotokea katika ulimwengu mkubwa zaidi ya hapo ulipo sasa yanaweza pia kuathiri biashara yako, hivyo wewe ukiiangalia biashara yako kwa mapana, unaweza jiandaa kukabiliana na magumu hayo.
  • Wekeza katika mbinu za kisasa za marketing na mauzo , kwa mfano je unatumia inbound marketing ?
Pata msaada usipitwe na mabadiliko
Wasiliana nami kwa WhatsApp +57 301 297 1724 [Namba ya nchini Colombia ] ili nikupatie ushauri binafsi utakaoendana na aina ya ujasiriamali unaofanya au unaotaka kufanya. Njoo tubuni mikakati ya marketing na jinsi utakavyopanua soko lako. Au nicheki kwa email john.myungire@gmail.com

Share:

0 comments:

Post a Comment