Google AdSense ni matangazo yanayowekwa katika website. Matangazo hayo ni kwamba watu wanaotaka kutangaza bidhaa zao hufanya kushindania kupata nafasi ya kutangaziwa matangazo yao.
Watu wanapozungumzia kutaka kutengeneza hela kupitia mtandao hutaja Google AdSense.
Ngoja nikudokeze kidogo kuhusu AdSense. Ni kweli hulipa. Hata hivyo kuna mambo machache ya kufahamu:
Mchakato wa kujiunga na Google AdSense
Kuna mchakato unaohitaji umakini kweli kweli ili uweze kusajiliwa kwa hiyo huduma ya AdSense. Sio kila website , blog au YouTube account inaweza tuu kusajiliwa. Moja ya mambo ya kuzingatia ni kuwa uwe na contents za kutosha, na wakati mwingine husisitiza lugha sahihi itumike kwa blog au website yako ili kweli Google waweze kuipitisha blog yako.
Jinsi hela zinavyoingia kupitia Google AdSense
Unahitaji views nyingi kwa blog au website yako ili uweze kuingiza fedha kupitia Google AdSense. Hata hivyo kuwa tuu na Views nyingi kwa website au blog yako haimaanishi basi eti mapato yatakua makubwa.
Hii ni kwa sababu matangazo yanaoyoonyeshwa hutegemea ni kiasi gani watu wameahidi kulipia kwa kila click ya tangazo husika.
Hivyo kuna mambo mawili makubwa yanayosababisha mapato yawe makubwa au madogo. Kwanza bei ambayo watangazaji wamesema wapo tayari kulipia kwa kila CLICK ya tangazo husika, na pili idadi ya clicks kwa kila tangazo.
Kwenye idadi ya clicks hapo ndipo panapoleta ile hali kuwa unaweza kuwa na hata VIEWS ELFU 10 kwa siku lakini ukapata mapato kidogo kuliko mwenye VIEWS EFLU 5 kwa siku.
Inawezekana mwenzako mwenye views chache ana matangazo yenye dau kubwa halafu watembeleaji wake kweli wanakua interested na hayo matangazo yanayoonyeshwa katika website au blog husika.
Maandalizi ya msingi ili uanze kuingiza fedha kupitia Google AdSense:
Katika yote yote, unahitaji design nzuri ya blog, unahitaji kutambua vema walengwa husika ambao kweli kupitia hao matangazo yatakua yenye kulipa, na pia unahitaji uwe na makala zitakazoweza kweli kuvuta watu wengi zaidi waje kwa blog au site yako. Kwani kadri watu wanavyotembelea ndivyo unaongeza nafasi ya wewe kupata watu watakao click matangazo husika na hapo ndipo utakapoingiza fedha.
Mapato mengine zaidi ya Google AdSense
Kama unaona AdSense ni ngumu, kuna njia nyingine nyingi tuu za kuingiza hela kupitia blog au website yako.
-- Njoo tuzungumzie upate maujanja zaidi na maelekezo yanayokuhusu wewe kama wewe maana kila blog au site ni tofauti na nyingine hivyo mikakati ya kuingiza fedha inaweza kuwa tofauti.
Nicheki kwa WhatsApp +57 301 297 1724.
Usikose siku ya Alhamis Feb 16 saa mbili usiku nitakua nikifundisha kupitia WhatsApp na FB groups maalum jinsi ya kuwa na blog kwa ajili ya kampuni, NGO na biashara mbalimbali. Wasiliana nami ujiandikishe uje ujifunze namna ya kuingiza mapato na kuongeza MAUZO kupitia blogs.
Enter your comment... Makin xana bro
ReplyDeleteVizuri sana
ReplyDeleteNashukru kwa somo zuri, Mimi nimetengeneza blog ambayo ni hii www.tenachew.com.
ReplyDeleteNaweza kujiunga na Google AdSense?
Google AdSense
DeleteIla nmeisajili blog yangu Na Adsense Na wananiambia unsupported language.Unalzungumziaje hili suala.
ReplyDeleteWanataka utumie lugha ya kingereza.
DeleteBlog yangu ina mafunzo mengi.
ReplyDeletehttps://upendokitundu.blogspot.com
Thanks.
Delete