FAHAMU MTEJA MLENGWA UONGEZE MAUZO YA BIASHARA YAKO

Wakati mwingine unaweza lalamika kuwa biashara ngumu , wateja hawanunui bidhaa yako au kuna ushindani mkubwa wa soko lakini kumbe tatizo lipo kwako wewe mwenyewe kwakua hujamtambua kweli kweli ni NANI HASWA NDIO MTEJA wako. 

Mtazamo usio sahihi kuhusu mteja
Waweza sikia kwa mfano mtu akisema eti haelewi kwanini ana marafiki wengi lakini eti bidhaa zake hazipati wateja. Wingi wa watu pekee haufanyi uwepo wa wateja. Mfano sio kwa sababu unaouza nguo za akina mama basi wanawake wote ni wateja wako.
Sio kwa sababu kwa mfano kwakua kuna shule nyingi mtaani kwenu basi ukleta viatu vya shule utapata tuu kuuza kwakua wanafunzi au wazazi wa wanafunzi hao ndio wateja wako na wapo wengi.
Ukiulizwa biashara yako inalenga wakina nani, unasema kila mtu, na ndio maana kwako haiingii akili kuwa kwanini ushindwe kuuza wakati unamlenga kila mtu. Hata hivyo kama unataka biashara endelevu ni lazima uwe na walengwa maalum.

Maana ya mteja mlengwa:
Tunaposema walengwa maalum tunamaanisha kundi fulani la watu ambao wana sifa za jumla ambazo kwa kutumia sifa hizo utafahamu vema namna gani ya kuwahudumia na kuwapatia kweli kitu wanachohitaji.

Kwahiyo mteja mlengwa ni yule ambaye kweli anaguswa na bidhaa husika unayotaka kuifikisha kwa wateja.
Mteja mlengwa unamfafanua kwa kuangalia aina gani ya bidhaa unaitoa, nani haswa atafaidika nayo, nani.

Faida za kufahamu kwa umakini mteja mlengwa
Kuwa na walengwa maalum kunakuongezea uwezo wa kuwa mbunifu zaidi maana upo kwa aina fulani tuu , hivyo unatumia muda mwingi "ukiwa" na hao walengwa wako, utawafahamu vema mwelekeo wao, tabia zao, shida zao , na wanayopendelea hivyo kujiset ziendano na hao.
--Kuwa na wateja maalum kutakufanya ufahamu namna bora zaidi za kuwasiliana nao kimasoko, vile unavyoweza tengeneza matangazo yako , promotions na mbinu zingine za kimasoko kama vile contents zako ziweje.
--Kuwa na wateja maalum kutakufanya hata ujiset vema katika kupanga bei za bidhaa zako, mfano mzuri iphone mpya mara nyingi bei zao ni juu kuliko aina nyingi za simu kwakua iphone ina aina maalum ya wateja waliokusudiwa.
--Kuwa na wateja maalum na kuwatafiti vizuri kunakupa amani kwa maana utapunguza stress za kujiona unashindana na kila mtu. Ukishakua na wateja maalum, utajikita nao , utajituma nao, utafocus zaidi kwenye mfumo wa biashara yako na bidhaa yako, na sio kwenye kuangalia washindani wako wanafanya nini.
--Kujua wateja vizuri kutakufanya kweli kweli utengeneze upekee wako mbele ya soko.
Usipitwe na ufahamu mambo haya ya ujasiriamali haswa katika zama hizi za kidigitali. Nicheki kwa ushauri binafsi na muongozo wa mambo ya masoko na jinsi unavyoweza itumia teknolojia kuwafikia watu wengi zaidi. +57 301 297 1724
Share:

0 comments:

Post a Comment