FAIDA 6 ZA KUWA NA WEBSITE KWA AJILI YA BIASHARA AU NGO

faida za kuwa na website
Je umekua ukisikia tuu swala la kuwa na website lakini hujaelewa kwanini haswa uwe na website kwa ajili ya biashara au asasi yako isiyo ya kiserikali (NGO)? Au unayo website lakini haujaona bado faida za kuwa na website ? Basi makala hii itakupasha  faida haswa ya kuwa na website kwa namna ambayo pengine hujawahi kufikiria.
Hakuna wakati ambao website ni ya muhimu kama wakati ambapo tupo katika zama za utandawazi. Yawezekana ukajiona kuwa unachofanya ni kidogo hivyo hauhitaji website , hata hivyo kuna mengi utakua unakosa kwa kutokujikita katika kuwa na website kwa biashara au asasi yako.

Kukipa thamani ufanyacho
Imekua kawaida watu wengi kuamini kuwa biashara au asasi yenye website basi itakua makini . Hata hivyo sio tuu website ili mradi website. Unatakiwa uwe na website ambayo kweli inaonyesha umakini na ubora wa asasi au biashara yako hii inajumuisha website yenye muonekano mzuri, yenye maelezo yaliyokamilika, yenye taarifa ambazo kweli.

Kuleta ushawishi
Unahitaji website ili kuweza kujenga uaminifu na kuonekana kweli upo serious. Website yako itakupa nafasi ya kuwaeleza watu kwa umakini na kwa ushawishi kile unachofanya  na kwanini wakutafute wewe. Tena website itakusaidia kufanya ushawishi huu kwa watu wengi sana kuliko kuwa tuu na vipeperushi ambavyo utasambaza kwa watu wachache.

Kuelezea Ufanyacho
Website hukufanya uwe na nafasi ya kueleza mambo uyafanyacho kwa watu wengi zaidi. Ni kweli unaweza kuwa na akaunti nyingi za mitandao ya kijamii . Lakini watu wengi hawatopata kukufahamu vizuri kama sio kupitia kwa website yako ambapo utakua na kurasa zilizopangiliwa vema kabisa.

Kupatikana wakati masaa 24 siku 7 za wiki
Ofisi yako hufungwa , duka lako hufungwa, lakini website yaweza kupatikana masaa 24 siku 7 za wiki. Hivyo kuwa na website ni fursa kwako kuwafaikia walengwa wako masaa yote kila siku.

Kuwasiliana na kuwaelimisha wateja
Kwa kutumia blog itakayoambatana na website yako utaweza kuwapatia wateja wako na wale wateja watarajiwa Makala ambazo zitawaelimisha na kuwavuta karibu na wewe. Pia ni nafasi yako ya kuwapa updates kuhusu bidhaa mpya unazotaka kutoa au mabadiliko mengine ya kiutendaji , kimarketing na sera za biashara au asasi yako.

Kuwa na email address binafsi
Website itakufanya uweze kuwa na email address inayotaja jina la biashara yako. Haipendezi na haionekani kuwa “professional” pale unapohitajika kutaja email address yako halafu ukatumia email yenye domain ya makampuni makubwa kama gmail, yahoo au Hotmail. Kama kampuni yako ni ABC Limited, basi ni vema ukasema jinalako@abc.com au  jinalako@abc.co.tz

Kwa wewe unayetaka kuwa na website inayokunufaisha tuwasiliane kwa WhatsApp +57 301 297 1724 tukusaidie. Au comment  kwa hii post.
Share:

12 comments:

  1. nataka niwe na website itakayo husika na kutoa taarifa kwa jamii nifanyeje

    ReplyDelete
  2. Habari:naomba unasaidie jins ya kutengeneze website ambayo utausika na ujasiriamali,kilimo,na ufugaji ambayo itakuwa inamilikiwa na kikundi cha vijana cha singida youth network(syn).

    ReplyDelete
  3. Naitaji website ambayo itahusika na upandaji Wa miti na utunzaji wa mazingira kwa ujumla mfano
    Plantabillionoftree.com
    Jonasjovin3@gmail.com
    +255762276275
    +255626063600

    ReplyDelete
  4. Hi
    It is my hope that you are getting on well!
    I have set my new year plan of having a website by 2020.
    I am planing to have my own online platform which I have thought to call it as "Tanzania Legal Services Unit" (TALESU), the platform by which people will have to create an account in order to access legal materials, it will be a free use website where people will need not to pay for it in order to subscribe. The only requirement will be for them create an account and sign in whenever they they want to access some reading from the website!
    The website should display various legal subjects and topics that readers will need to pass through!
    However, I am prepared to make full payment by the end of March 2020 or not later than that.
    What I want from you is write prepare the bill I am likely to incur!
    Be fair, and priceful! I will abide by your terms and condition of payment!

    Yours
    Masanja

    ReplyDelete
  5. Habar mm ni mjasiriamali nauza nguo za dukani nina page Facebook sina website na hii inaniwiavigumu kufikia wateja wengi naitaji msaada jinsi ya kufungua website

    ReplyDelete
  6. Nahitaji mtu wa kunifundisha kutengeneza website na blog tuwasiliane 0768763701 nipo Daresalamu

    ReplyDelete
  7. Asante sana kwa somo zuri. Nahitaji kuwa na website nitawezaje???

    ReplyDelete
    Replies
    1. https://chat.whatsapp.com/JyKf52AhAleCSpSXgpmwum
      Jiunge kwenye Group hili la mafunzo ya kutengeneza website

      Delete
  8. Naomba mafunzo kutoka kwenu nijue namna ya kufungua web site step by step

    ReplyDelete
  9. Kwa wanaohitaji mafunzo au msaada wowote juu ya masuala ya website tuwasiliane kupitia no. 0693783527

    ReplyDelete
  10. Je ni njia gani nifanye ili nipate website ya biashara

    ReplyDelete