TABIA 9 KATIKA KUTUMIA ENGLISH AMBAZO SI NZURI HATA KIDOGO

Kama unajifunza English au undataka kutumia vizuri English jitahidi sana utumie kanuni na taratibu sahihi za uandishi na uongeaji wa kiingereza. Katika makala hii fupi nitakukumbusha mambo 9 ambayo hutakiwi kuyafanya ili usionekane unatumia vibaya English.

Katika English kuna tabia sugu ambazo ni mbaya kweli kweli ngoja nizitaje hapa chini.
1. Kutokutumia alama za maandishi kwa usahihi. Mfano pa kuweka kiulizo usiweke kiulizo. Au kutumia alama ya kushangaa wakati huhitajiki kuitumia au kuzitumia nyingi bila sababu. Ushawahi ona mtu karibu kila aandikacho humalizia na !!!!!!!
2. Kutumia vifupi vya maneno isivyopaswa mfano Its Friday badala ya It's Friday
3. Kutokutumia herufi kubwa ipasavyo mfano tunasoma kuwa proper nouns zote ni lazima ziandikwe kwa herufi kubwa ila utakuta mtu kaandika jina lake au la mkoa kwa herufi ndogo
4. Kutokutumia maneno ya kuonyesha ustaarabu kama vile please, would, may, can. Usipotumia haya utajikuta ukionekana kama vile unatoa amri au sio mstaarabu.
5. Kuandika I kwa herufi ndogo mfano: John and i are friends.
6. Kutokutumia salamu kwa ufasaha kulingana na aina ya mtu unayewasiliana nae. Mfano hufai kumsalimia boss wako au mwalimu wako HEY!
7. Katika kuongea kuna ile tabia ya mtu kujilazimisha kuiga lafudhi kama vile ni mtu wa nchi fulani matokeo yake anasikika kama kero kwa huyo anayeongea nae. Jitahidi uongee taratibu na utamke maneno kwa ufasaha lakini sio utake kuonekana wewe kuwa ni mmarekani au mwingereza kwa mfano.
8. Kutokufanya punctuation ipasavyo mfano penye kutakiwa comma usiweke comma. Mfano mzuri katika picha hapa ya post hii DON'T TEACH JOHN ina maanisha usimfundishe mtu aitwaye John, waka Don't teach, John ina maana kuwa mtu aitwaye John ndio anaambiwe asifundishe.
9. Kutokufanya juhudi kuandika maneno ya English kama yanavyotakiwa kuandikwa badala yake kufanya mazoea ya kuandika English kama Kiswahili au kuiga maneno ya watu mfano Thanks kuandika TX.

Share:

1 comment: