Kama unatamani kuwa na blog kuna mambo mawili nataka nikushirikishe leo:
1. Ni kweli unaweza kuendesha blog kupitia simu yako au tablet yako , na tena kwa kutumia Play Store unaweza kuinstall app maalum ya blogger au wordpress kutegemea na teknolojia gani unaitumia.
Kupitia apps hizo unaweza fanya mambo ya msingi kama kuandika post, na kuedit post. Hata hivyo apps hizo si nzuri kama hauna kabisa blog. Mfano kwa blogger inabidi kwanza uwe umetengeneza bog kwa kutumia browser kama vile Google Chrome, au Firefox, kisha uitumie ap kuandika, na kuedit makala.
2. Utajiuliza kwanini nimetaja blogger na WordPress. Hizi ni teknolojia zinazoongoza katika kutengeneza blogs. Zipo nyingine nyingi ila hizi mbili ndizo zinazotumiwa na watu wengi zaidi. Mfano blog maalum ya Tanzania ya MillarAyo imetengenezwa kwa kutumia WORDPRESS wakati blog ya Issa Michuzi imetumia BLOGGER.
Kuna sababu za msingi na za kitaalamu kwanini mfano uamue WordPress badala ya blogger.
Blogger na WordPress zote ni bure, ila WordPress ambayo ni bure ina vikwazo kadhaa mfano kuna kikomo cha kiasi cha uhifadhi unaoweza pata wa picha na taarifa zako ukitumia wordpress.com , na hata kuziedit templates zake kuna kikomo. Hata hivyo worpress unaweza kuwa nayo na kuihost mahali popote unapotaka wewe, tofauti na ilivyo blogger, ambayo ni kweli ni bure kabisa, na haina ukomo wa kiwango cha uhifadhi -storage capacity, ila huwezi ihamisha blog yako uipeleke kwa mtu mwingine.
WordPress hutupatia uhuru wa kutengeneza blogs na websites nzuri sana, kwakutumia vitu vingine kama plugins na themes zilizo nzuri sana, hata hivyo ifikapo kwenye swala la usalama , blogger ni kimbilio zaidi kwani blogs za blogger zinasimamiwa na Google, hivyo usalama wake ni mkubwa kuliko wewe binafsi kutafuta kampuni yoyote tuu ya kuhost blog yako ya WordPress.
Usisahau MBUKE TIMES tunaweza kukusaidia kutimiza ndoto yako ya kuwa na blog ya ukweli. Sio tuu kwamba tutaifanya blog yako ipendeze, ila pia tutakuelimisha ujue vyanzo mbalimbali vya mapato ya blog ukiacha matangazo, na namna ya wewe kunufaika binafsi ukiacha kifedha.
Tuwasiliane kwa WhatsApp +57 301 297 1724 au email : john.myungire@gmail.com
nimeelewa mkuu
ReplyDeleteUmeeleweka kiongoz
ReplyDeleteNa0mba unisaidie blog yangu hii kuset
ReplyDelete