Ni jambo la kawaida kujiuliza kama unampenda Fulani
au kama Fulani anakupenda. Katika tafakari hii, wengi hujikuta wakipata
tafakari tofauti. Uzoefu wangu unanifanya niamini kuna maana tofauti kuu 3
zinazojitokeza miongoni mwetu wakati wa kutafakari swala la upendo katika
mapenzi.
Jiunge nami katika tafakari hii kwa kusoma
jinsi watu wanavyotafsiri tofauti neno Upendo katika mahusiano:’-
1.Kujali: Kuna
wanaoamini kuwa kujali tuu inatosha kuonyesha kuwa unampenda fulani, au fulani
kuonyesha anakujali basi hiyo ndio maana halisi ya upendo. Wengi hujikuta wakitumia
muda mwingi kutafuta zawadi na surprises za ‘nguvu’ kama sehemu kuu ya
kuonyesha upendo wao. Aina hii ya upendo inahusika sana hasa kwa watu waliopo
mashuleni na vyuoni. Wengi wanaoamini maana hii ya upendo, husisitiza sana
kuogopwa/kunyenyekewa kama sehemu ya kuonyeshwa kuwa nao wanapendwa.
2. Kujitoa kafara: Katika maana hii, upendo ni swala la jinsi gani unavyojitoa kwa
mwingine ili kuona anakuwa na furaha na ajihisi kuwa salama kutokana na uwepo
wako. La msingi katika aina hii ya upendo ni kupenda kumfahamu vema mwenzi
wako, kujua shida zake, na ndoto zake, na kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha
anaona uwepesi katika shida zake, na kuwa anakuwa na matumaini ya kuwa ndoto zake
zitatimia. Upendo wa namna hii huwa na subira, na huonekana zaidi kwa
waliokomaa kifikra, na wenye kujiheshimu wao wenyewe.
3.Kuvutia: Kwa
wengine upendo ni namna gani wanavyovutiwa kimapenzi na mtu husika, au vile
wanavyojisikia kuwa salama mbele ya mtu fulani.
Utakuta mtu anasema anampenda kaka fulani kwakuwa tuu amevutiwa na
uhodari wa kijana husika katika masomo, kujiheshimu kwa kijana husika, sifa au umaarufu
alionao mhusika. Na kwa upande mwingine, mtu anaweza kuvutia kwa uzuri wa sura
au umbile la mtu fulani. Kutokana na mvuto wa hisia kama hizo na wakati
mwingine hisia hizi za mvuto huwa kali sana, basi mtu akadhani hiyo ndiyo maana
halisi ya Upendo. Wenye tafakari hii ya upendo wengi wao hawana subira na
ukichukua muda mrefu kutafakari hisia hizi, unaweza kukuta ni za muda mfupi
tuu.
Hitimisho: Pamoja
na ukweli kuwa mvuto wa kimapenzi kwa mtu unayejenga nae mahusiano ni muhimu.
Na kwamba kujaliana na kunyenyekeana ni vigezo muhimu katika kujenga mahusiano
yenye furaha, mambo hayo pekee hayatoshi kusema kuna upendo. Upendo ni jambo
lisilo na ubinafsi, haliangii nafsi yako inataka kunufaika kiasi gani, bali
unataka kuinufaisha nafsi ya mwingine kwa kiwango gani. Hivyo kwa upande wetu,
maana ya upendo tunayoipendekeza ni Kujitoa Kafara, kama tulivyoielezea hapo
juu.
Yote katika yote, inakupasa utambue kuwa upendo
pekee hautoshi kujenga mahusiano yenye furaha na yenye kudumu. Katika makala SABABU 5 KWANINI UPENDO HAUTOSHI KUJENGA MAHUSIANO BORA
nilieleza kwa kirefu kuhusu hili. Bofya hapo ujisomee zaidi.
well said thank you .
ReplyDelete