JINSI YA KUOMBA NA KUULIZA MASWALI KISTAARABU KATIKA ENGLISH

Namna sahihi ya kuomba mtu afanye kitu fulani kwa kutumia lugha ya kiingereza imekua ni tatizo kubwa kwa wengi wanaojifunza English. Usipokua makini katika kuandika au kusema ombi lako unaweza kuonekana hujastaaribika, unatoa amri au si mtu mwema.
Nimekutana nalo hili sana kwa wengi wanaohitaji kujiunga katika group letu la WhatsApp la #JifunzeEnglish kwa kuniandikia tuu "Add me to the group".

Kuna maneno maalum huwa yanatakumika katika English ili kuonyesha kuomba  au kuulizia kitu kwa ustaarabu. Maneno hayo ni Can, Would, Will, Could na May. Tuangalie mifano hapa chini:

1. Kuomba ruhusa ya kuingia ndani :
- Can I come in ?
- May I come in ?

2. Kuomba kuuliza swali:
- Could I ask you something ?
- Can I ask you something ?
- May I ask you something ?

3. Kuomba kuunganishwa kwa group la WhatsApp
- Would you add me to the group, please?
- Will you add me to the group?

4. Kuomba mtu azime sauti ya muziki
- Will you stop the music , please ?
- Can you stop the music, please ?
Share:

3 comments:

  1. Would you add me to the group please no 0693444420

    ReplyDelete
  2. Can you stop ther cryn please baby

    ReplyDelete
  3. Can u add me to the group please by this number 0624973403

    ReplyDelete