Umeshawahi kusikia kuwa unaweza itumia website ya Google kama Calculator ? Au Facebook kama TV na kama duka ? Je simu yako ya mkononi unaitumia kama notebook na kwamba smartphone yako yaweza kuwa remote ya tv ? Au umeshasikia kuwa dawa ya mswaki ina matumizi zaidi ya 30 ? Nimekuuliza maswali haya ambayo najua kama si yote basi mengi kati ya hayo hukujua kuwa yanawezakana na wewe kama wewe hujawahi kufanya hivyo. Ninachojaribu kusema ni kuwa kuna fursa nyingi za kufanya mambo mengi ila bado hufanyi kwa sababu ya kutokujua au kudhani hauhitaji kufanya hivyo.
Kwanini mtandao haukuletei mafanikio ya biashara na NGO
Nazungumzia mabadiliko makubwa katika teknolojia yaliyorahisisha kufanya biashara na kuongoza asasi za kiraia (NGOs), hata hivyo maendeleo hayo ya teknolojia hayanufaishi wengi kwakua wengi wameingia kutumia nyenzo hizo za kiteknolojia bila kuzifahamu vizuri, na bahati mbaya wanadhani tayari wanajua, hivyo kama ilivyo kwenye matumizi ya Google, mtu unabaki kuitumia Google kusearch tuu habari , makala au kitu fulani wakati Google ina matumizi kibao, au unatumia dawa ya mswaki kusafisha tuu meno bila kujua matumizi mengine sahihi ukidhani kusafisha meno ndio umemaliza.
Nikupe mfano rahisi, utaona wengi siku hizi wakipost matangazo ya bidhaa wanazouza. Ila ukiangalia wengi hawana ujuzi wa uandaaji wa matangazo hayo kiasi kwamba wanashindwa kutumia mbinu nyingi za kuhakikisha matangazo hayo kweli yanapata muitikio wanaoukusudia yaani kufanikisha kuuza bidhaa zao. Facebook au Instagram ni mitandao ya kijamii, sio vituo vya kuweka matangazo hivyo basi kama unataka kuuza kupitia mitandao hii inabidi pia na hicho unachosema na wewe mwenyewe ukae kweli kimtandao wa kijamii.
Kuna mengi ya kujifunza kuhusu mitandao ya kijamii.
Mfano mwingine mtu anatengeneza website akiamini atapata wateja kupitia website yake. Ila hakuna juhudi za kutosha za kuwafanya watu wengi wafike kwa website husika, na hata wachache wanaofika hawapewi kweli sababu ya kutosha kwanini wafanye biashara au dili na wewe. Websites sahihi zinazoleta kweli matokeo ya kifedha kwa wenye nazo zimetengeneza kwa kuzingatia misingi ya kumfikiria mlengwa msomaji, kuwa na contents ambazo kweli zinabeba thamani ya mtu kuzisoma na pia website inawezeshwa kupatikana mtu akiwa anatafuta taarifa zinaoendana na website husika, huko kwenye search engines kama Google, Yahoo, n.k Mambo haya kitaalamu tunaita content marketing na SEO.
Ufanye nini ili mtandao ukuletee mafanikio kwa biashara yako
Wewe mwenyewe jifunze matumizi sahihi ya mtandao. Mfano hata matumizi ya hashtag(#) tuu watu wengi hawajui. Cheki hii makala uone namna sahihi ya kutumia Hashtag. Bofya Hapa Kujua hashtag.
Tafuta msaada wa mtaalamu wa mambo ya mtandao ili akusaidie kupanga mikakati na utekelezaji wake kuhusu contents za website yako, ukurasa wa FB na akaunti nyingine za mitandao ya kijamii kwa ajili ya biashara yako. Kama nilivyosema hapo mwanzo, haitoshi tuu kupost vitu huko kwa mitandao ya kijamii halafu ukategemea matokeo. Au kuwa tuu na website ili mradi wewe unadhani ina muonekano mzuri. Juhudi za ziada zinahitajika ili ufanikiwe kutokana na uwepo wa biashara yako mtandaoni.
Anza sasa kupata mafanikio ya kuwepo mtandaoni
-- Kwa ushauri na kuwezeshwa kutumia Facebook kibiashara na kuwa na Website yenye kukuletea wateja , nitafute nikupatie unachostahili ili nawe uanze kufaidika. Nitakupatia huduma za SEO na Content marketing kwa ajili ya biashara yako. Na kukuonyesha namna ya kutengeneza matangazo yenye tija. Kwenye kutengeneza matangazo kuna kitu muhimu tunazingatia kinaitwa kitaalamu copywriting. Nicheki kwa WhatsApp +57 301 297 1724
Asante sana kwa elimu nzuri.
ReplyDelete