Idioms kadhaa hutumia ndizi kuelezea maana, mfano : To go bananas, top banana |
Kama umesikia maneno kama piece of cake, cut the chase, last but not least, kick the bucket, egg head, top banana, bad apple n.k hayo ni maneno ambayo tunayaita idioms.
Katika makala hii utajifunza idioms ni nini , umuhimu wake na namna gani utaweza kujifunza , kuzielewa na kuzitumia.
Idioms ni nini ?
Ni kundi la maneno linalowasilisha maana fulani kwa kutumia lugha ya picha. Mfano mtu anaposema John is the top banana of our group - imetumika lugha ya picha ya ndizi iliyo juu kabisa, ili kuelezea kuwa John ni kiongozi wa kundi letu.
Mfano : I have left my friend's book at home, and she needs the book very much. She has gone bananas. Hapa bila shaka unaweza kuotea maana ya to go bananas kwani kama mtu anakihitaji kitabu chake kweli kweli halafu wewe hujamletea mtu huyo atakasirika sana au atapandwa na uchizi kwa hasira.
Umuhimu wa kujua Idioms za English
Kufahamu idioms za English kutakusaidia kuepukana na kukwama kuelewa sentensi za English kwani hata kujua kuwa tuu idioms zipo kunatosha kukuondolea usumbufu mkubwa kwakua hautopoteza muda kutafsiri neno moja moja mfano kwenye top bananas , badala yake utajua kuwa hayo maneno yote yanakusudia kufikisha ujumbe mmoja hivyo wewe utafute tuu huo ujumbe unaokusudiwa.
Kujua idioms kutakufanya uongee na kuandika English itakayoonekana kweli imeenda shule.
Na utaweza kuelewa kwa urahisi mazungumzo mengi , nyimbo nyingi hutumia idioms, mfano wimbo wa Cyndi Lauper - Time After Time, hiyo ni idiom yenye kumaanisha kuwa kitu hutokea mara nyingi.
Jinsi ya kujifunza na kuzielewa Idioms za English
1. Kwakua sasa umeshagundua kuwa idioms ni lugha ya picha, utakua makini pale unapoona kikundi cha maneno ambacho hakina maana ya moja kwa moja na habari husika, hivyo utumie mazingira ya habari unayosoma au kusikia kujua maana ya idiom husika.
2. Hakikisha kila unapokutuna na idiom ambayo huielewi , iandike mahali ili uje ucheki baadae maana ya idiom husika na mfano wa jinsi inavyotumika.
3. Tunga sentensi zako mwenyewe zinazotumia idioms ili uweze kuzifanyia kazi idioms unazokumbuka , kwa namna hiyo hutokaa kuzisahau na itakupa hamasa ya kutaka kujifunza idioms nyingi zaidi.
Kujifunza zaidi idioms, bofya hii link kuna website inaitwa Idiom Site
Na kuendelea kufanya mazoezi na kuuliza maswali , jiunge na group letu la WhatsApp kwa kubofya link ifuatayo au niandikie message kwa +57 301 297 1724
Hitimisho
Nikupe hapa mfano wa mazungumzo yangu na mwanafunzi kule WhatsApp, aliyetaka kujua namna ya kujua kutumia Idioms katika sentensi. Ilikua hivi:-
Usihofu Idioms are just A DROP IN THE BUCKET when it comes to English. But at least you understand them when you read , right ? Or they are ALL GEEK TO YOU ?.
Lots of people who study English as a foreign language ARE IN THE SAME BOAT with you. But trust me idioms are not as high as a kite. So please don't feel like in HIGH WATER in your learning English. TO CUT THE CHASE, you need to work hard. TAKE IT EASY, and if YOU CAN HAVE A CUP OF JOE while learning idioms it will great!
Na kama haujaelewa samahani endelea kujifunza, I hope I DIDN'T DRIVE YOU UP THE WALL kwa habari hii yenye idioms kibao. Keep studying idioms, HOLD YOUR HORSES, it may take time but you will eventually understand them and start using them in your sentences . So in the mean time KEEP YOUR CHIN UP.
Thanks for sharing, nice post!
ReplyDeletePhục vụ cho nhu cầu vận chuyển container bằng đường bộ ngày càng lớn, vận chuyển xăng dầu bằng đường sắt và vận tải, gửi hàng hóa vận chuyển xe máy bắc nam bằng đường sắt cũng đã xây dựng nên những qui trình, dịch vụ vận chuyển hàng hóa bằng các toa xe chuyên dùng chuyên nghiệp và có hệ thống. Đảm bảo mang đến chất lượng tốt nhất cho khách hàng sử dụng dịch vụ.
The point is at home
ReplyDelete