MAMBO 3 YANAYOWAKWAMISHA WABONGO WENGI KUONGEA ENGLISH KWA UFASAHA


Nina zaidi ya miaka miwili sasa nikiwa mwalimu wa kujitegemea wa English.
Makosa ninayoyaona na ugumu kwa ibaadhi ya wabongo katika kuelewa English ni kuendeleza mazoea na kuiga "English ya mtandaoni" au ya mtaani bila kujua haswa kujua kanuni na taratibu sahihi za uandishi na uongeaji wa English.


Kuchanganya aina za maneno katika English: 
Wabongo wengi hawazingatii utofauti wa aina za maneno mfano ITS na IT'S ni vitu viwili tofauti , AM na I'M ni vitu viwili tofauti na hata YOUR na YOU'RE ni tofauti. Hivyo si ajabu kwa mfano wengi wakiandika AM FINE, au ITS OK , au YOUR WELCOME. Wakati hapo matumizi ya hizo AM, YOUR na ITS ni makosa.

Kutotambua na kuzingatia maana na tafsiri ya maneno katika English:
Kutokutambua na kuzingatia kuwa MAANA na TAFSIRI ni vitu tofauti husababisha wengi kuongea au kuandika English , ila ukiwauliza wanachomaanisha kwa Kiswahili utakuta kwa English walichokisema au kuandika hakina maana hiyo.
Mfano angalia tafsiri ya maneno haya picha toka https://www.facebook.com/tutunatablog/

Angalia baadhi ya tafsiri ya hayo maelezo kwa English kama yalivyoandikwa na baadhi ya wanafunzi wangu wa kibongo:
-- Every day of life is the Class and every problem you are looking is the teacher
--Everyday of life is class,and  every problem which you pass it,is a teacher.
--Everyday of life is a class and every hard time you face to is a teacher
--Every day of the life is the class and every problem which faced you is the teacher.!

Na hapa chini ni maelekezo ya jumla ya marekebisho ya makosa yaliyojitokeza katika kutafsiri maelezo ya hiyo picha hapo juu:
Kila siku YA Maisha ni darasa na kila tatizo unalopitia ni mwalimu.  Hapa nimeona wengi mnasema Everyday OF life..kwa sababu mnatafsiri YA kama OF, hata  hivyo kwenye English mara nyingi huwa tunatumia IN kwenye kuelezea siku za maisha... Hivyo ni Everyday IN life... Kingine ukisema NI DARASA .. ktk English kama unaelezea kitu ambacho ni cha ujumla huwa tunatumia A..kama article na sio THE..hivyo ingekua  Everyday IN life is A class... 
Hapo kwenye  EVERY PROBLEM WHICH FACED BY  YOU.. umesahau IS.. ingekua which is faced by you..

Kutokuzingatia matumizi sahihi ya tenses katika English
Tenses na muundo mzima wa sentensi katika English ni shida kubwa kwa wengi. Wengi huandika tuu kwa kuunganisha maneno na vitendo bila kuzingatia tense sahihi matokeo yake ni kuwa maana wanayokusudia sio ile ambayo kwa English inatakiwa iwe.
Mfano mtu anasema : I saw you. Unamuuliza ana maanisha nini, anasema NIMEKUONA. Kwakua ametumia Simple Past tense ina maanisha NiLIkuona.


Hitimisho
- Tukubali tukatae , kufahamu English kwa ufasaha ni muhimu sana haswa katika ulimwengu huu wa utandawazi. Walioweza English vizuri wamejifungulia fursa kibao katika maisha yao.
-http://mbuke.blogspot.com.co/sea…/label/Jifunze%20Kiingereza
Nimeweka humo masomo ya bure kabisa ya English.
Na pia niandikie message kwa namba +57 301 297 1724 nikuunganishe kwa group la WhatsApp lenye members zaidi ya 156 sasa ili ujiunge na masomo ya kila siku.
Share:

0 comments:

Post a Comment