HIVI NDIVYO UTAKAVYOJUA ENGLISH KWA UFASAHA NDANI YA MWAKA 2017

Tayari tumeuanza  mwaka mpya  2017. Mwaka huu una siku 365, miezi 12, wiki 52, masaa 8760 na dakika 525600. Kwa wewe mwenye lengo la kujua kuongea na kuandika English bila shaka una muda wa kutosha kabisa kufanya hivyo.  Hata hivyo usione kwamba una siku nyingi sana, usipojipanga vema utajikuta mwaka huu wa 2017 unaisha na bado haujaweza fanya kitu.
Lengo la makala hii ni kukupa mwongozo wa namna gani utahakikisha unaweza kufanikisha lengo la kuongea na kuandika English kwa ufasaha kabla ya mwaka huu wa 2017 kuisha.

Mbinu za kujua tenses za English:
Kujifunza tenses katika kiingereza ni kujiwezesha kujua kwa namna gani utaunganisha vitendo (verbs) na maneno mengine kwa usahihi. Na kwakua mara nyingi tunahitaji kuongelea kuhusu vitendo/matukio , usipofahamu matumizi sahihi ya tenses, unajikuta upo na wakati mgumu sana wa kuongea English sahihi.
Anza kwanza kujua aina za verbs katika English. Kisha zijue aina zote 12 za tenses katika English.

Mbinu za kujua aina za maneno( parts of speech):
Chukulia mfano rahisi wa matumizi ya maneno SAFE, SAFETY, na SAFELY. Safe ni Adjective kazi yake kufafanua kuhushu JINA au Kiwakilishi. Mfano The house is safe.. tunafafanua jinsi nyuma ilivyo-ipo salama. Au waweza sema It is safe.. yaani hicho kitu kipo salama.                        
Safety ni Jina , majina huelezea ili kutambulisha hali, watu, maeneo n.k. Mfano: Your safety is important- usalama wenu ni muhimu. Hapa tunasema hali yaani usalama                        
Adverbs zinafafanua kuhusu matukio(verbs) au adjective au adverbs nyingine. We arrived safely.. hapa tunafafanua kuhusu tukio la kufika. Yaani tumefikaje.
Ukifahamu vizuri aina za maneno hutochanganya kwa mfano matumizi ya YOUR na YOU’RE kwani utajua kuwa YOUR ni adjective, wakati YOU’RE ni muunganiko wa pronoun YOU  na verb ARE.
Jipatie kitabu cha English:Mbinu na Kanuni za Kuijua, utaona nimefafanua vizuri aina zote za maneno tena kwa Kiswahili na mifano ya English ili uelewe vema. Kukipata kitabu wasiliana nami kwa WhatsApp +57 301 297 1724

Namna ya kuunganisha maneno ili sentensi ilete maana:
Ili sentensi yako ilete maana zingatia tenses, zingatia aina ya maneno na pia zingatia mazingira na maana inayokusudiwa kwani wakati mwingine unaweza tumia neno ambalo ni sahihi kwa tafsiri ya Kiswahili ila kwa mazingira yaliyopo neno husika halileti maana iliyokusudiwa.
Mfano: Thanksful for God… ikiwa na maana ya Ashukuriwe Mungu. Sentensi hii ina kosa kwakua Thanksful ina maana ya kuwa na shukrani, ila ktk sehemu hii haijaunganishwa vya kutosha. Ilitakiwa iwe Thanks to God.

Taratibu za kusoma English ili uelewe vema:
Ni muhimu ukapanga namna gani utajisomea ili kweli uelewe vema English. Kuna vipengele vingi katika English vinategemea kwa maana ya kwamba ili uweze kuelewa kipengele fulani, unahitaji kuelewa kwanza kipengele kingine.
Mfano bila kuelewa vizuri TENSES huwezi elewa kwa ufasaha conditional sentences. Bila kuelewa vizuri personal pronouns huwezi kukamata kwa ufasaha mambo ya passive voice.
Mie kama mwalimu wa English nimetoa nafasi chache kwa watu wanaotaka darasa maalum, wanaohitaji kuelekezwa hatua kwa hatua mpaka waelewe English. Nitafute tuanze darasa hilo , utachangia fedha kidogo tuu kama ahsante yako. Na baada ya miezi mitatu, utaona mabadiliko makubwa.

Hitimisho:
Kufahamu English kwa ufasaha isiishie tuu  kuwa ndoto yako. Amini unaweza kabisa kuanza kuongea English kwa ufasaha na hivyo kujifungulia fursa nyingi sana ambazo kwa sasa huwezi kuzifikia kwakua huwezi English.
Kama bado unajiuliza utaanzaje kuweza English kwa ufasaha, wasiliana nami kwa namba +57 301 297 1724 niambie unaitwa nani na unahitaji kujiunga group la JifunzeEnglish. Ni bure kujiunga na utajifunza kila siku mambo mengi na kufanya mazoezi na wanafunzi wengine zaidi ya 180 toka mikoa yote ya Tanzania.

Share:

0 comments:

Post a Comment