WAFAHAMU WATU WANAOITWA SOCIOPATH

Dexter Morgan katika tamthilia iitwayo DEXTER anaonyesha tabia
zinazotambulisha Sociopaths. Itazame hiyo tamthilia kwa kujiongezea
ujuzi kuhusu watu hawa hatari waitwao sociopaths.
Hii ni kwa mujibu wa mtaalamu aitwaye Paul Rosenberg na references nyingine. Atakayetaka makala nzima aniambie email yake ntamtumia.

Kwanza sociopath ni nani ? A sociopath: is an otherwise normal human who has a profound lack of empathy for the feelings of others.  Yaani sociopath kwa asili yeye haoni huruma kwa mtu yoyote yule. Hata hivyo sio lazima ajionyeshe wazi wazi kuwa hana huruma, hujificha ili kutimiza hitaji lao la kumpata mtu wa kumtenda.
Kwakuwa wao hawana hisia zozote za huruma wala mapenzi, inawalazimu hao sociopath kuiga watu wa kawaida wanavyoishi. Na kwakuwa hatutilii maanani jinsi watu wanavyoonekana , ni ngumu kutambua nani haswa ni sociopath, nani siye.
Ni shida kumjua sociopath kwakuwa
1. Wengi wetu tunaamini kila mtu ni mzuri, wakati ukweli kuna watu 100% ni wabaya tuu, ni muda tuu unawasubirisha kufanya ubaya wao.
2. Sio wengi sana inakadiriwa 2% ya watu wote ni sociopath mahesabu ambayo pia yanasemwa kuwa kati ya watu 50 mmoja ni sociopath
3. Lingine kwakuwa wao hawana hisia yoyote wao hawajisikii vibaya kudanganya, jambo linawapelekea kutokutambulika uongo wao hata kwenye LIE DETECTERS, zile mashine za kutambua kama mtu anasema uongo au la.
Baada ya kueleza hapo juu kwanini ni ngumu kwa watu wengi kumtambua sociopath tuone jinsi ya kumtambua.
1. Kama unasoma hii kitu tayari unafaida ya kumtambua sociopath kwakuwa wao hutumia kutokujua kwetu kuwa wao wapo. Ile imani kuwa kila mtu mzuri hutuharibu na kutuweka hatarini kudhurika na sociopath. Hivyo kila wakati tambua kusoma jinsi mtu anavyobehave.
2. Pamoja na kwamba sociopath huiga kuonekana wapo wa kawaida, huwa wanashindwa kwa asilimia 100 kuonyesha huruma na upendo. Ingawa wengine huwa na wenza wa ndoa, na hata watoto, ila chunguza namna wanavyoonyesha hisia zao haswa utagundua utofauti mkubwa. Vitu vya kuangalia ni namna wanavyojali wapenzi wao, watoto, mambo ya misiba na mijumuiko ya kijamii,  pamoja na kuweza kufeki, ila ukia ngalia kwa makini utajua kuna walakini.
3. Kwakuwa sociopath kiasili hujisikia raha kudhuru wengine , chunguza watu ulionao karibu  je hujisikia raha kusingizia wengine, au hufanya matendo  yasiyo ya kihuruma na hawaonyeshi kujutia, n.k .
4. Wazungu wanasema "when the deal is so good, think twice". Kuwa makini na watu wanaojifanya wema sana.
5.Kwakuwa wanahitajika kujificha, hujitengenezea mazingira ya kutokutambulika na kuiaminisha jamii kuwa ni watu safi, kiasi kwamba hata ukija sikia wamefanya hivyo utashangaa. Wengi wa wanasiasa  na viongozi wa asasi mbalimbali inasemekana ni sociopath.
Chunguza maamuzi ya wanasiasa wengi yasivyo na huruma. Mfano wa viongozi maarufu ni Mao Tse-tung ambaye ni baba wa taifa la  CHINA anayedaiwa kubaka na kuua watu wengi kwa njaa. Mwingine ni kiongozi wa zamani wa shirika la utangazaji la BBC anaitwa Jimmy Savile ,yeye alikuwa na genge la udharirishaji wa watoto. Aliendesha genge lake kwa miaka 40 bila watu kujua, mpaka alipofariki.

Baadhi ya maswali ambayo watu wengi huuliza: 

Je unajitambua kama  wewe ni Sociopath ?
Waweza jipima kama wewe ni sociopath au la. Je, unapata ugumu kuwaonea wengine huruma ? Je unapenda kuona wengine wanateseka au haujisikii lolote mtu mwingine anapoteseka ? Je, kwa makusudi umewahi kutaka kumfanyia "kitu mbaya" mtu ?

Je, sociopath kuna kitu kinatokea unakuwa triggered?
Sio lazima kitu kitokee wawe triggered, kumbuka hawa sociopath hawana hisia zozote
Je sociopath ni wazungu tuu kwa kuwa wazungu labda wanakuwa lonely so hawana cha kufanya kiasi kwamba wananyemelewa na hizo hisia?
Sociopath hajisikii lonely. Hajui hizo hisia za kuwa lonely , hajisikii kutaka kupendwa, hajisikii chochote.Huyo ndio real sociopath. Hata hivyo SIO kila mtu mwenye kufanya jambo la ukatili ni sociopath. Kuna wanaofanya jambo baya wakajutia, pengine kwa hasira , au visasi. Ila sociopath yeye , kufanya ubaya ni "hitaji" lake muhimu.

Serial Killers wote ni sociopath. Serial killers ni wale wanaojitengenezea orodha ya. watu wanaowaua. Ni hatari sana hawa watu, kwani sio lazima watumwe kuua. Ni kwamba wanajitengenezea sababu zao kichwani mwao zinazowatosha basi.
Hata hivyo SIO kwamba sociopaths wote ni serial killers.
Share:

0 comments:

Post a Comment