MBINU BORA YA KUJIFUNZA MANENO MAPYA NA KANUNI ZA ENGLISH

Kuna kitu tunaita PATTERN, yaani jinsi ambavyo maneno, mionekano mbali mbali hutokea. Njia rahisi ya kujifunza maneno mapya, kanuni na hata kutamka maneno ya English ni kujua patterns mbalimbali.                        
Mfano: Kwa kuchunguza sentensi nyingi zinazotumia BY, WITH, WITHOUT, OF, ON , AFTER, ABOUT AT... utajionea kuwa kama verbs zikifuata sentensi hizo ni lazima ziwe ktk ING.. mfano : I am tired of hearing excuses.. Nimechoka kusikia visingizio. He came without calling.. Alikuja bila kupiga simu.                        
Hiyo tunaita PATTERN.. yaani umechunguza sentensi nyingi na kugundua ufanano wake.                                                
Chunguza mfano mwingine wa namna tunavyotamka maneno haya:  DECORATION, ORGANIZATION, COMMISSION, PREPOSITION..utagundua kuwa yote yanaishia na "SHEN" ukitamka. Mfano Decoration -- DekoreSHEN, Organization- OrganaizeSHEN.. n.k Kwahiyo kujua neno moja kunakusaidia kufahamu mengine yote yanayoishia na ION..                        
Chunguza pia tunavyotamka maneno  Quality, Unity, University,  na mengine yanayoishia na ITY.. je umeweza kugundua PATTERN ?                        
Mifano mingine jinsi PATTERNS zinavyosaidia ni kwenye kujifunza TENSES. Mfano ukichunguza vizuri tenses zote zina hali ya kuendelea verbs zake ni lazima ziwe na ING.. Mfano: I was eating.. nilikua nikila -Past Continous,  I am eating - Ninakula - Present Continous, I will be eating- nitakua nikila - Future Continous.                        
Hivyo kujua pattern kunakurahisishia kukumbuka na kujifunza mambo mengi kwa pamoja.                        
Je wewe ktk kujifunza kwako English umekutana na pattern gani ?

--Tukutane kwa group la WhatsApp la JifunzeEnglish upate mbinu zaidi, ufanye mazoezi ya kuongea na wengine English, na uulize maswali yanayokutatiza kuhusu English.
Andika meseji ukijitambulisha na kusema unahitaji kujiunga na group la English kwa +57 301 297 1724



Share:

0 comments:

Post a Comment