Hii ndio sababu wengine hushindwa elewa mtu mwingine akiongea kwa sababu pengine anatamka neno unalodhani unaelewa ila kumbe tuu yanafanana matamshi na hivyo wewe ukijaribu kuunganisha maneno hupati maana kwa kua tayari wewe na huyo anayezungumza hamlengi neno moja
REMEMBER na REMIND. Katika sentensi yako umesema "Remind that, Nobody is perfect". Hapo kuna kosa. REMEMBER ni KUMBUKA yaani tukio la mtu mwenyewe kupata kumbukumbu fulani. Mfano : I remember him. He was here with his mother. Namkumbuka yeye, alikuwepo hapa na mama yake. REMIND.. ni kukumbushwa yaani unapata kumbukumbu ila ni KWA MSAADA WA TUKIO au MTU MWINGINE . Mfano : Remind me please, what's your name ? Nikumbushe tafadhali, jina lako nani ? This song reminds me of my days in South Africa. Huu wimbo unanikumbusha wakati nilipokua Afrika ya Kusini.
Poor =masikini, wakati Pour= mwagilia au mwaga. Hear =sikia wakati Here = Hapa
Mfano: HURT na HEART, WEATHER na WETHER , BUY na BY.
Mfano unaweza sema I think my friend HURTS me nowdays. Ukitaka kumaanisha Nafikiri rafiki yangu ANANICHUKIA siku hizi. Hata hivyo neno HURTS linamaana ya KUUMIZA. Ungetumia HATES ambayo kidogo inakaribiana kutamkika na hiyo HURT. Ili usikosee jitahidi uyafuatilie haya maneno kwa ukaribu. Mifano mingine; Piece(kipande) wakati PEACE ni AMANI.
To...inaelezea muelekeo wakati TOO ina maana PIA. Weak=Dhaifu wakati WEEK=juma yaani siku saba. Steal=iba wakati STEEL= chuma
0 comments:
Post a Comment