Logo ni sehemu ndogo tuu ya branding. Picha na 5wpr.com |
Kama kuna jambo moja tuu utakalojifunza katika makala hii basi liwe ni utambuzi kuwa bila kujenga kuaminiwa na kupendwa na wale unaokusudia kuwauzia huduma yako, basi lengo lako la kufanya kwa mafanikio hicho unachofanya halitofikiwa. Na kitu cha kipekee kitachokujengea ukaribu, kuaminiwa na kupendwa na wateja unaowakusudia ni brand.
Utajiuliza bila shaka kwa jinsi gani brand inajenga ukaribu , kuaminiwa na kupendwa na wateja au kundi fulani la watu unalokusudia. Jibu ni rahisi na linatokana na maana ya brand. Kabla haujaenda mbali kusoma hili, tafadhali simamisha yale mawazo kuwa brand ni logo au rangi zinazotumiwa na asasi fulani. Katika makala hii ninakueleza maana pana zaidi ya brand, na namna ambavyo ukielewa brand vizuri itakavyokubadilisha namna unavyofanya biashara au shughuli zako za asasi isiyo ya kiserikali.
Bila shaka utakua umeshagundua kuwa sitaji brand kama kitu kinachohitajika tuu na biashara. Ndio maana natumia maneno kama vile brand ni muhimu katika kufanikisha ukaribu wako na walengwa unaowakusudia, au kufikia malengo ya kile unachokusudia kufanya. Brand kwa maana yake halisi inahitajika kwa biashara binafsi, makampuni, asasi zisizo za kiraia, watu binafsi na hata asasi za serikali.
Maana ya brand
Brand ni ule ukaribu wa kifikra na kihisia unaojengwa kwa jamii na asasi au mtu fulani.
Kutokana na maana hiyo hapo juu inakupasa ujue kuwa ingawaje logo, na rangi za asasi au shughuli ya mtu fulani ni muhimu katika kutengeneza brand, hizo rangi au logo hazitokua na msaada katika kujenga brand endapo hazifikii kugusa fikra na hisia za watu.
Na pia kutokana na maana ya brand niliyoeleza hapo juu , utakubaliana nami kuwa haitokuwa na maana kuwa na brand ambayo haikumbukwi na haijengi ukaribu na jamii au kundi linalolengwa.
Na inakupasa mpaka sasa uelewe kwanini tunachagua hisia na fikra katika maana halisi ya brand. Lengo la kufikia na kukaa kwenye hisia na fikra za watu ni kwakua hisia na fikra zina nguvu sana katika ufanyaji wa maamuzi ya watu kuliko kutumia akili na sababu nyingine.
Tunataka katika brand kufikia hisia na fikra za watu ili iwe rahisi kukumbukwa na kutengeneza ukaribu kama alivyowahi sema Maya Angelou :
“I've learned that people will forget what you said, people will forget what you did, but people will never forget how you made them feel.”
kwa Kiswahili tunaweza itafsiri :
“ Nimejifunza kuwa watu watasahau ulichosema, watu watasahau ulichofanya, ila kamwe watu hawatosahau jinsi ulivyogusa hisia zao”
Logo na rangi kama sehemu ya brand :
Kwakua lengo la brand ni kutengeneza upekee fulani katika fikra na hisia za walengwa, logo na rangi za kipekee zinazounda brand zinatakiwa ziwe kweli zenye kubeba maana na kuendana na lengo husika la brand.
blog.bufferapp.com |
blog.bufferapp.com |
Uchaguzi wa rangi inapaswa kuzingatia uchunguzi wa kisayansi kuhusu rangi ili kweli rangi husika ziweze kuvutia watu wanaolengwa na kuwafanya wakumbuke kwa urahisi. Kwa mfano, rangi ya njano itumike kwa uangalifu sana kwani watafiti wanasema wanaume na wanawake wengi hawapendi rangi hiyo kwenye vitu ambavyo wanasoma. Na pia kuna baadhi ya rangi wale wenye matatizo ya kuona rangi hawawezi ziona.
Kwakua unataka kujenga ukaribu wa kifikra kwa unaowalenga, logo na rangi unazotumia zinajenga utambulisho wa kipekee , na kupitia huo utambulisho tayari unajua nini kinazungumzwa. Mfano bila shaka logo zifuatazo bila kusema chochote wewe msomaji unajua zinahusu kampuni gani
Kazi za logo na rangi katika branding
Logo na rangi huwakilisha falsafa na dhamira ya mwenye kutaka kujenga brand.
Mfano wengi mtakua mmeona log ya Mercedece Benz na logo ya Toyota
Logo na rangi
Hiyo logo ya Toyota inaonyesha duara zilizoungana, na zinaashiria falsafa ya Toyota ya kuhakikisha bidhaa zao zinatengezwa kwa kuunganisha uhalisia na kazi za bidhaa na mahitaji ya mioyo ya wateja.
Toyota wenyewe katika website yao wanaeleza hivi kuhusu logo yao :
In 1990, Toyota debuted the three overlapping Ellipses logo on American vehicles. The Toyota Ellipses symbolize the unification of the hearts of our customers and the heart of Toyota products. The background space represents Toyota's technological advancement and the boundless opportunities ahead.
Brand ni zaidi ya logo na rangi
Kuwa na falsafa na kutengeneza utambulisho wa kipekee kupitia logo na rangi ni jambo zuri na ni sehemu ya kutengeneza brand, hata hivyo mafanikio makubwa ya brand huja kwa matendo yanayofanywa na asasi au mtu anayetaka kujenga brand.
Matendo haya ni lazima yalenge kugusa hisia na fikra za watu kwa namna ya kipekee na kuwafanya walengwa watake kweli kuwa karibu na hiyo brand.
Matendo utakayofanya yawe na lengo na muelekeo wa kubeba ujumbe fulani mmoja na wa kipekee kuhusu wewe. Ujumbe huo uweze kuwa uje utakaovutia walengwa wake na kuwashika hisia na fikra zao. Uwe ujumbe ambao kweli watapenda kusikia, na ndio ujumbe ambao utakutambulisha kwa watu kuwa wewe au asasi yako ni ya namna gani.
Hiyo namna utakayoijenga ya watu kufikiria na kupatwa na hisia kuhusu wewe au asasi yako , ndio haswa brand yenyewe unayoijenga.
Brand haijengwi kwa tukio moja au kwa shughuli za msimu. Inahitajika kuwekeza kwa muda mrefu katika kujiweka karibu na walengwa wako, ukiwapatia mambo tofauti tofauti yanayoeleza ujumbe kusudiwa wa wewe au asasi yako ni ya aina gani.
Matukio kama vile namna unavyohudumia wateja, vitu unavyosema, ubora wa bidhaa zako, misimamo ya kiitikadi unayoieleza kua unayo ni baadhi ya mifano ya mambo yanayoweza athiri aina ya brand unayotengeneza, bila kusahau matangazo yako ya biashara unayosambaza kwa jamii.
Kunahitajika umakini kwanza katika kubuni namna gani ya ujumbe na fikra unayotaka kuitengeneza machoni mwa watu. Ujumbe na hisia unazotaka kujenga ziendane kweli na wewe mwenyewe na bidhaa unazotaka kuja kuuza.
Hitimisho
Kunahitajika muda na mikakati mathubuti ili kweli brand yako iweze kutambulika , kukua na kutimiza malengo unayokusudia.
Brand ni jambo zuri sana ambalo lina thamani itakayokulipa endapo utawekeza katika kutengeneza kikweli kikweli brand husika.
Brand itapanua mauzo ya bidhaa yako kwa tayari utapendwa na watu nakuaminika. Tayari itakua rahisi hata walengwa kuwataarifu watu wengine. Brand itakusaidia kupata washirika wa kufanya nao biashara. Brand itakusaidia kupata wafanyakazi hodari na bora.
Karibu tuzungumze. Napatikana kwa WhatsApp +57 301 297 1724.
Kwa muongozo binafsi kuhusu brand, logo na mbinu za kijasiriamali nicheki kwa namba hiyo hapo juu ya WhatsApp. Au niandikie email:
Umeeleza kwa Namna rahisi sana na rafiki kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili. Ahsante kwa Elimu
ReplyDeleteHakika ni elimu inayompa mtu upeo wakutambua Nini afanye kufikia malengo yake
ReplyDelete