Leo niwazungumzie matumizi ya maneno haya ambayo hutumika sana katika mazungumzo ya kiingereza:
Gonna
Gonna hutumika kufupisha maneno GOING TO.. mfano : I gonna catch you.. Nitakukamata (I am going to catch you).
Kumbuka kutumia auxiliary verb husika kuendana na noun au pronoun utakayoitumia. Hivyo basi usiseme tuu I gonna buy a book...Nitanunua kitabu.. Badala yake sema I am gonna buy a book kwa sababu I huendana na AM.
Mfano
Jose is gonna be here… kwakua Jose inatumia IS, usiseme tuu Jose gonna be here.
Inaweza tumika kwenye swali pia mfano : Are we gonna eat tonight ? Je tutakula usiku wa leo ?
Wanna :
Neno hili hutumika kufupisha maneno WANT TO ..
Mfano :
I wanna go now… Nataka kuondoka sasa ( I want to go now)
I wanna love you forever… Nataka nikupende daima ( I want to love you forever)
Ain’t
Neno hili hutumika kama kifupi cha am not, are not, is not, has not, na have not.
Mfano:
You ain’t a soldier- wewe sio mwanajeshi ( You are not a soldier)
I ain’t got what you need - sina kile ambacho unahitaji. (I have not gotten/got what you need). Nimeandika got au gotten kwakua zote ni sahihi.
Age ain't nothing but a number - Umri si kitu ila ni namba (tuu) Age is nothing but a number.
Nataka nijifunze engelish
ReplyDelete