HIVI NDIVYO UTAKAVYOJUA TENSES KATIKA ENGLISH


Wengi katika kujifunza English hukwama kwenye matumizi sahihi ya tenses. Utakuta mtu anaelezea habari ya wakati uliopo ila ameieleza kama vile ni habari ya wakati uliopita.
Hivyo basi ili uweze kuwa mzuri kabisa katika tenses inakupasa kwanza kabisa uachane na namna utumiavyo nyakati (tenses) katika kiswahili. Kwa mfano : kwenye Kiswahili ni mazoea kusema hivi : “ Mimi ninafanya kazi katika kampuni X”. Katika sentensi hii kitendo ninafanya, kinaonyesha kuwa tukio ni kama vile linatokea wakati huu, ingawaje ujumbe unaokusudiwa sio kwamba tukio linatokea kwa wakati huu tuu ila hutokea mara nyingi, yaani ipo hivyo kuwa wewe hufanya kazi katika kampuni X.
Hapo ndipo kosa linapokuja kwani wewe kwa tafsiri yako ya moja kwa moja ya Kiswahili utasema hivi : I am working at company X , sentensi ambayo mtu ambaye huongea English vizuri hatokuelewa kuwa unamaanisha huwa unafanya kazi kwa hiyo kampuni, badala yake ataelewa kuwa kwa muda husika tuu ndio upo unafanya kazi hapo.


Hivyo basi ili kutumia vizuri tenses, kwanza jifunze kazi za kila tenses katika English na uachane na namna zisizo sahihi za kutumia tenses katika Kiswahili.


Ukijifunza matumizi mazuri ya tenses katika English kwa mfano utaelewa kuwa
1.Sio sahihi kusema I am understanding you.. Badala yake sema I understand you. Hii ni kwa sababu ukisoma simple present tense utajua kuwa huwa inatumika pia kuelezea vitendo fulani hivi vya wakati uliopo hali ya kuendelea,kwa namna ya upekee. Vitendo hivyo ni kama vile hate, like, love, prefer, want, wish, appear, feel, hear, see, seem, smell, sound, taste,agree, deny, disagree, mean, promise, satisfy, surprise,believe, imagine, know, mean, realize, recognize, remember, understand,be, belong, concern, depend, involve, matter, need, owe, own na possess


2. Utajua pia kuwa ni sahihi kusema “ Tomorrow, I am eating rice “ yaani kesho nitakula wali. Ingawa inaonekana kama vile kitendo kinaendelea lakini kanuni za English zinatuambia kuwa ni sahihi kusema hivyo.


3. Utajua namna sahihi ya kuuliza maswali na kukanusha sentensi kwa kila aina ya verb . Mfano ni kosa kusema  I didn’t went to school. Au Did he cooked rice  ?


Hitimisho: Ninachojaribu kusisitiza hapa ni kuwa kujua English kwa usahihi kunahitaji kujifunza kwa utaratibu, na kujua misingi yake.

Katika group letu la WhatsApp ambapo mpaka sasa tumefika 134 utakutana na watu wengi wanaotaka kujifunza kama wewe. Karibu ujifunze na kupata tips kama hizi kila siku. Ni bure kabisa. Tuma maombi ya kujiunga kwa namba +57 301 297 1724. Tafadhali jitambulishe jina lako , upo wapi na useme unataka kujiunga.

Share:

0 comments:

Post a Comment