Je umejifunza English muda mrefu ila bado hauwezi kuongea na kuandika kwa ufasaha kwa hiyo lugha ya kiingereza ? Kama unajiuliza ni kwa namna gani utaweza kuongea English kwa ufasaha basi makala hii itakusaidia.
Epuka vifupi na maneno magumu :
Wakati unajifunza lugha hakikisha unaweka mbele kwanza kueleweka zaidi kuliko KUREMBA maneno. Unachohitaji ni kuwa FLUENT, yaani kuongea au kuandika bila kukwama kwamba. Tatizo la kuweka vifupi au kutaka kuongea maneno magumu ni kujirudisha nyuma maana unaacha kujifunza mambo ya msingi zaidi, na wakati mwingine hata kukosea maneno kwa kutaka kuonekana upo na English ya namna fulani. Mfano ni bora useme I AM.. badala ya kusema AM kwani sio sahihi, labda ungesema I'M kweli, ila kwanini ujilazimishe kukosea ?
Wakati unajifunza lugha hakikisha unaweka mbele kwanza kueleweka zaidi kuliko KUREMBA maneno. Unachohitaji ni kuwa FLUENT, yaani kuongea au kuandika bila kukwama kwamba. Tatizo la kuweka vifupi au kutaka kuongea maneno magumu ni kujirudisha nyuma maana unaacha kujifunza mambo ya msingi zaidi, na wakati mwingine hata kukosea maneno kwa kutaka kuonekana upo na English ya namna fulani. Mfano ni bora useme I AM.. badala ya kusema AM kwani sio sahihi, labda ungesema I'M kweli, ila kwanini ujilazimishe kukosea ?
Ondoa wazo la ushindani:
Lengo la kujua English kwako liwe ni kuweza kufanya mawasiliano ili kufikia malengo mengine ya kimaisha kama mafanikio ya kielimu, ajira , safari au mahusiano. Kujua English kama kujua tuu hakuwafanyi wasiojua English kuwa si bora zaidi yako. Hatari ya kufanya ushindani wa kutaka kuonekana unajua sana English ni kujisikia uoga wa kujaribu zaidi, au kujaribu kujifunza lafughi za hali ya juu kiasi kwamba hadi unaharibu maana ya maneno unayotaka kuongea. Kutaka kuonekana unajua na kukazania ushindani kuna athari ya kudhorotesha juhudi zako za kuijua lugha vizuri kwani utaogopa kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwakua utakua unaogopa kukosea.
Fahamu siri hii:
Tunajifunza lugha ili tuitumie, hivyo njia nzuri zaidi ya kujifunza lugha ni kuitumia. Yaani fanya bidii ya kuandika na kuongea sentensi za English kwa kadri uwezavyo. Kwa maana nyingine basi usiogope kukosea, maana kukosea ni sehemu ya kujua lugha. Hata hivyo sio tuu ukosee na kukosea bila kujua umekosea wapi na namna gani utajirekebisha. Ndio maana kuna haja ya kutafuta mtu anayejua vizuri lugha na kuongea nae au kuandika vitu yeye akusahihishe. Na kwa sasa kupitia group la WhatsApp la JifunzeEnglish unaweza mpata mtu wa kufanya hivyo. Tuma message kwa namba +57 301 297 1724 na jina lako ili uingie katika group hili.
Sikiliza wanaotamka na soma sana makala, au hadithi fupi fupi:
Je wewe unapendelea fashion ? Au unapendelea muziki, au mpira ? Au unapendelea mambo ya kipelelaezi ? Basi tafuta videos , makala na hadithi za kiingereza na uzisikilize au kuzisoma. Hata hivyo kumbuka sio tuu kusoma au kusikiliza hizo makala , videos au hadithi, hakikisha unajua udhaifu wako ktk lugha haswa ni nini, halafu wakati ukipitia hizo makala , hadithi au videos basi hakikisha unachunguza ni kwa namna gani vipengele vya lugha
Jifunze Maana na sio tafsiri tuu ya maneno:
Tafsiri ya neno ni vile unavyolitafsiri neno husika moja kwa moja kwa Kiswahili. Mfano katika sentensi hii I HAVE GOT IT.. maana yake ni NIMEIPATA.
Hata hivyo neno linaweza kubeba maana tofauti kuendana na mazingira lilivyotumika au maneno mengine ya ziada katika sentensi husika. I GOT IT. pia ina maana ya NIMEELEWA, NIMEIPATA, au IPO MIKONONI MWANGU USIHOFU.
Ndio maana basi wewe unaweza kung'ang'ana na kujifunza lugha wee, ila kama huituimii yaani kwa kufanya mazoezi nayo unaweza jikuta unasema huelewi watu wengi wanachoandika au kuongea kwa sababu hufanyi mazoezi ya kutosha kujua MAANA ya maneno, na maana ya maneno utaipata katika mazungumzo iwe ya kuandikiana au kuongeleshana na watu wanaozungumza lugha husika.
black magic
ReplyDeleteblack magic for love
Black magic to get love
Love marriage solutions
Vashikaran Mantra
Vashikaran specialist
Black magic to get your love back
Thanks for this post.
ReplyDeletehttp://www.astrologerhome.com/online-vashikaran-astrologer.html
Nimefurahi Sana kwaushauri mnaotoa ili tuweze kujua kingereza
ReplyDeleteJe nawezaje kujuwa kuongea kwa haraka
ReplyDelete