Kuna msemo kuwa wateja ni damu ya biashara, kwa maana ya kwamba bila wateja hakuna jinsi ya kuendelea na biashara. Msisitizo wa umuhimu wa wateja unadhihirishwa pia na msemo kuwa bosi wa kweli katika asasi au biashara yoyote ni mteja, yaani hata mmiliki wa biashara ambaye ndio bosi wa mabosi wa asasi husika, naye ana bosi wake ambaye ni mteja kwa maana ya kwamba bila wateja, hata mmiliki wa biashara atakua kapoteza kazi yake kama mmiliki wa biashara maana biashara haitokuwepo.
Hivyo basi la msingi katika biashara au ujasiriamali ni kuhakikisha kuwa unaweza kupata wateja na kuendelea kuwahudumia wateja uliowapata.
Mie kwa zaidi ya miaka mitano sasa nimekua nikibuni bidhaa mpya na kuuza, mfano nilishauza kitabu cha mambo ya programming, na kwasasa naendelea kuuza kitabu cha kanuni na mbinu za kujifunza English, ukiachilia mbali huduma nyingine kama utengenezaji wa websites na ushauri wa mambo ya ujasiriamali.
Katika makala hii najaribu kukushirikisha mbinu za wewe pia kujipatia wateja wa bidhaa zako na kuendelea kubaki na wateja. Kuna wateja wa aina mbili: Wale ambao tayari wamenunua au wananunua bidhaa zako, na wale ambao bado unawalenga wanunue. Katika makala hii tutacheki zaidi kuhusu wale wateja ambao tayari wamenunua au wananunua bidhaa zako.
Kuwauzia wateja ambao tayari walikwishanunua kwako
Wateja waliokwishanunua kwako wamekwisha kuitambua bidhaa yako na kuonja huduma yako kwa mteja. Je unarudiaje kuwauzia tena bidhaa ile ile au bidhaa yako nyingine ?. Kujibu swali hili soma kwa makini points hapa chini:
Hakikisha unatoa huduma bora mara tuu upatapo mteja:
Huduma bora itakujengea jina na nafasi ya kumfanya mteja atake kuja tena. Hii ni muhimu sana kwani wakati fulani inawezekana usiwe na bidhaa yenye kukidhi haja ya mteja , ila mteja husika akajisikia kukupa nafasi tena ya kujaribu bidhaa hiyo au bidhaa nyingine unazouza kwakua aliona tayari utayari wako wa kuhudumia vizuri.
Onyesha kuheshimu na kushukuru kwako kwa yeye kununua bidhaa husika:
Kuna msemo unaosema kushukuru ni kuomba. Hata makampuni makubwa huwa na tabia ya kusema ahsante mara unapoweka oda ya bidhaa kwao na hata ukinunua bidhaa.
Hakikisha unapata mrejesho toka kwa mteja:
Wasikilize wateja wako wanasema nini. Usipende tuu kupata sifa, jifunze kusikiliza hata kwa wateja ambao wanalalamika na kusema vibaya kuhusu biashara yako. Mmiliki wa kampuni kubwa ya vifaa vya mawasiliano na software , Bill Gates aliwahi sema hivi”Your most unhappy customers are your greatest source of learning.” Yaani wateja wake ambao hawafurashiwi na bidhaa au huduma zako ndio chanzo kikubwa cha wewe kujifunza.
Endelea kujenga mawasiliano na ukaribu na mteja husika :
Hata kama hanunui, endelea kumkumbusha uwepo wako na bidhaa zako. Uwepo wa mitandao ya kijamii kunaweza kutumika kama sehemu ya wewe kuendelea kuwa karibu na wateja wako , kuwapatia habari zenye kuwaburudisha, kuwaelimisha na hivyo ikitokea wanahitaji la bidhaa kama yako , basi wanaweza kukurudia mara moja.
Wafanye wateja wako wajisikie kuwa walifanya uamuzi sahihi wa kufanya biashara nawe, na kwamba bidhaa zako zinaendelea kuwa bora, hivyo hata nao wanaweza kurudi na marafiki au ndugu zao kununua toka kwako.
Hitimisho:
Katika makala hii tumeangalia namna gani ya kuongeza mauzo kwa kuangalia zaidi uhusiano wako na huyo mteja aliyekuja kununua bidhaa yako. La kukumbuka hapa ni kuwa uhusiano wako na huyu mteja ni muhimu sana, kwani pengine umeingia gharama kubwa kujitangaza au umetumia muda mwingi kujitangaza ili kupata mteja, basi usipoteze nafasi ya kumfanya mteja husika ajisikie kweli kafika kwako.
Katika makala itakayofuata, tutaangalia namna gani ya kupata wateja wapya. Tutaanza na uchambuzi wa namna gani unaiandaa bidhaa ili kweli ikupatie wateja.
Kwa ushauri binafsi wa masuala ya ujaasiriamali na teknolojia, tuwasiliane kwa WhatsApp +57 301 297 1724
Na kama unataka kuondokana na tatizo la kuongea English, basi nicheki upate kitabu hiki.
Thanks for sharing, nice post! Post really provice useful information!
ReplyDeleteGiaonhan247 chuyên dịch vụ ship hàng nhật uy tín, giá rẻ cũng như chia sẻ kinh nghiệm cách order taobao về VN giá rẻ.