JINSI YA KUTUMIA NYIMBO KUJIFUNZA ENGLISH: MFANO IT'S NOT EASY BY LUCKY DUBE

Nyimbo ni sehemu nzuri sana ya kujifunza lugha ya kigeni. Hata hivyo usipojua nini cha kuangalia wakati unasikiliza au kuangalia wimbo  unaweza usifaike sana na wimbo husika.
Hivyo makala hii inakupa mbinu za kutumia nyimbo kwa manufaa. Maelezo haya ni kwa mujibu wa kitabu cha ENGLISH : KANUNI NA MBINU ZA KUIJUA.
Kitabu hicho nimeandika mie, na kinapatikana kwa Tshs. Elfu Kumi na Tano. Tuwasiliane kwa WhatsApp +57 301 297 1724.

Mbinu zenyewe ni rahisi sana :
1. Kusikiliza au kuangalia nyimbo bila kujua kanuni za lugha kunaweza kusikusaidie sana kujifunza kumudu vizuri lugha, na wakati mwingine unaweza usielewe kwa nini maneno fulani yana maanisha hivyo yanavyomaanisha katika wimbo husika. Hivyo kwanza mbinu ya kwanza, jifunze kanuni za muundo wa sentensi katika lugha husika. Hapa tuzungumzie English.

2. Wakati unasikiliza wimbo anza kwanza kusikiliza wimbo wenyewe bila kuangalia maneno ya wimbo (Lyrics). Hii itakusaidia kufanya mazoezi ya kusikiliza na wakati huo  huo wewe mwenyewe kuvumbua maana ya maneno kutokana na kutafakari sentensi nzima nzima zina maana gani kwa mujibu wa mazingira ya wimbo. 
Hii ni muhimu sana kwani katika mazungumzo na kusoma mara nyingi hautokuwa na kamusi hivyo njia pekee ya wewe kuelewa kwa haraka maneno mapya ni kufikiria maana ya maneno mapya kwa kuzingatia maneno mengine unayoyafahamu katika sentensi husika.

3. Tafuta maneno ya wimbo husika yaani Lyrics. Kupitia lyrics utaweza kujifunza zaidi maana ya maneno na pia muundo wa sentensi katika English.

Angalia mfano tunapojifunza kwa pamoja maneno ya wimbo IT'S NOT EASY wa marehemu Lucky Dube.
I remember the day I called mama on the telephone
I told her mama I'm getting married
I could hear her voice on the other side of the telephone she was smiling
And she asked me a question that I proudly answered
She said son did you take time to know her
I said mama she's the best
But today it hurts me so
To go back to mama and say mama I
'M getting divorced
Oh I'm getting divorced


This choice I made didn't work out the way I thought it would [x2] it hurts me so mama
Mama said to me



[Chorus:]
It's not easy to understand it son
But I hope you'll make it [x3]
You'll be happy again



I remember in church
When the preacher read the scriptures
You looked so beautiful and innocent
I did not know that behind that beauty
Lies the true colors that will destroy me in the near future



This choice I made didn't work out the way I thought it would be [x2]
Now I'm hurting



I remember when I held you
By the hand preacherman read the scriptures
Putting words in your mouth



Maybe what the preacherman said was not something that was within you
Now I know what they mean when they say



Beautiful woman is another man's plaything
Oh Lord I'm hurting now



This choice I made didn't work out the way I thought it would
Mama said to me



[Chorus]


Kanuni za English zilizotumika katika wimbo It’s not Easy wa Lucky Dube:
Wimbo huu upo kwa sehemu kubwa katika Simple Past Tense (Wakati uliopita katika hali ya kawaida). Mfano “I could hear her voice on the other side of the telephone she was smiling”.
Hapa “I could her… “(Niliweza kumsikia) ni simple past, ila kwakua anataka kuelezea kitendo ambacho mama alikua akifanya wakati huo yeye alipompigia simu, ndio maana ametumia pia past continuous tense anaposema “she was smiling”.
Tunaona pia namna ya kuuliza swali katika simple past, pale anaposema “… did you take time to know her.” Utakumbuka nilikudokeza kuwa kama tunauliza maswali katika simple past tense huwa tunatumia DID.
Pia angalia sentensi hii  “This choice I made didn't work out the way I thought it would”.

Hapa kanuni ya sentensi ya kukanusha katika simple past tense inatumika kwa kusema …”didn’t work out…” 

Pia angalia sentensi hii “But I hope you'll make it “.  Hapa tunaona matumizi ya IDIOM, yaani maneno “MAKE IT” ambayo kwa pamoja yanamaanisha “kushinda, au kufanikiwa”. Yaani mama mtu anamwambia kijana kuwa anatumaini kuwa huyo kijana ataishinda hiyo hali.

Pia sentensi “I did not know that behind that beauty. Lies the true colors that will destroy me in the near future” nayo inatumia IDIOM yaani neno “TRUE COLORS”, tunaposema true colors of someone, au show true colors, tunamaanisha tabia halisi ya mtu ambayo imekuwa ikijificha. Kwahiyo katika sentensi hii Lucky Dube anasema kuwa 
“Sikufahamu kuwa nyuma ya huo uzuri, kumejificha tabia yake halisi ambayo itakuja kunidhuru muda mfupi ujao”.



Hitimisho: Ukiwa unasoma huo wimbo vizuri, jiulize sio tuu maneno gani huyajui, ila pia chunguza muundo wa sentensi uone namna ambavyo kanuni za English tulizojifunza zinavyotumika. Mfano angalia jinsi sentensi za kukanusha zinavyoandikwa, angalia verbs to be zinavyotumika kama zipo, n.k
PATA MAKALA YA KITABU HIKI KWA KUWASILIANA NAMI KWA WHATSAPP : +57 301 297 1724 AU KWA FACEBOOK www.facebook.com/mbuketimes
Share:

0 comments:

Post a Comment