WhatsApp ,
ni app iliyoanzishwa miaka sita iliyopita huko nchini Marekani, inayowapa
watumiaji wake uwezo wa kuwasiliana kwa ujumbe mfupi wa sauti na maneno, na pia kupigiana simu. App hii inayotumiwa na
watu wengi zaidi kuliko app yeyote ile ulimwenguni, kwani kwa mujibu wa Wikipedia
Mpaka Februari mwaka 2016, WhatsApp ilikuwa na watumiaji wapatao bilioni moja.
Makala hii
inakupasha mambo kadhaa ambayo bila shaka hujui kuhusu WhatsApp na uendeshaji
wake.
WhatsApp
haiifadhi message, picha , video wala audio ambazo tayari umewasiliana nazo na
watu :
Kwa mujibu wa maelezo ya website ya highscalability.com, ni kuwa WhatsApp hutumia simu yako kama kihifadhi taarifa zote hizo
ikiwemo meseji, picha, video na audio. Wao WhatsApp huifadhi tuu kwa muda
usiozidi siku 30 meseji, picha, video, na audio ambazo hazipokelewa na mtu
aliyekusudiwa. Baada ya muda wa siku 30 kupita , kampuni ya WhatsApp hufuta
hizo taarifa ambazo zimeshindikana kufikishwa huko zilipokusudiwa kufika.
Chanzo cha jina la WhatsApp:
Chanzo chake hasa ni msemo wa What’s up ? ambao kwa Kiswahili
unatafsirika kama mambo vipi ? Waanzishaji wa WhatsApp waliona ni msemo mzuri
kuashiria lengo kuu haswa la app hii la kuwafanya watu kuanzisha na kufanya
mazungumzo.
Status na picha ya profile ya WhatsApp: Blogu ya
bintiyesse.blogspot.com katika makala yake WHATSAPP INAVYOANIKA UHUSIANO WAKO WA KIMAPENZI, imeeleza kwa kirefu namna ambavyo status na picha yako
ya profile ya WhatsApp inavyoweza kuweka wazi nini kinaendelea katika maisha
yako. Bofya hapa kusoma hiyo makala ya mapenzi na WhatsApp.
Waanzishaji wa WhatsApp waliwahi kuomba kazi wakanyimwa huko
Facebook na Twitter:
Ni kweli baada ya kufanya kazi miaka 20 kwa kampuni ya
Yahoo, waanzalishi wa WhatsApp bwana Jan Koum na Brian Acton. Hii
inaweza kuwa ni sababu moja ya kuwachochea kutengeneza App yao wenyewe yaani
hii ya WhatsApp, kama kulipa kisasi cha kunyimwa kazi na kuja kushindana na hao
Twitter na Facebook.
Mwanzilishi wa WhatsApp hapa mwaka 2009 akieleza alivyokataliwa na Facebook |
Mwanzilishi wa WhatsApp hapa mwaka 2009 akieleza alivyokataliwa na Twitter |
WhatsApp ilianzishwa mwaka 2009 mwishoni, na Februari 2014
ikauzwa kwa Facebook na sasa hao waanzilishi wa WhatsApp wanatambulika kama
mojawapo ya mabosi wa Facebook. Mtu unaweza sema wamelipa
kisasi.
WhatsApp haina matangazo na unajua kwa sababu gani?
Ni kwa sababu kuweka matangazo katika huduma za kiteknolojia ni jambo ambalo
liliwachukiza sana waanzilishi wa WhatsApp. Inaripotiwa kuwa hadi leo Jan ,
mmoja wa waanzilishi wa WhatsApp anatunza karatasi (Angalia picha hapo chini) yenye ujumbe wa No Ads, No
Games, No Gimmicks aliyoandika mshirika wake Brian akisisitiza kuwa daima
hawatoruhusu matangazo, gemu au ujanja ujanja wowote wa kuwarubuni watu
kimatangazo.
Picha na businessinsider.com |
Na katika website yao www.whatsapp.com , kuna makala nzima inayofafanua kwanini hawaweki matangazo. Bofya Hapa kusoma mwenyewe.
Emoji hii haina maana ile wengi wanadhani
inamaanisha :
Kwa watumiaji wengi wa WhatsApp , emoji inayomuonyesha nyani
akiziba macho inatafsirika kama alama ya kuonyesha aibu. Hata hivyo emoji hiyo
ni moja ya emoji tatu zinazotambulika kama nyani watatu wenye busara –Three Wise
Monkeys.
Na emoji hiyo ya kuziba macho inabeba ujumbe wa See No Evil – yaani usishuhudie
uovu.
Cheki hapo chini nyani wengine na maana wanazobeba.
Picha na richardcassaro.com |
0 comments:
Post a Comment